Monday, April 27, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!


Hoopz

T.I na mwanae
Hoopz: Demu aliyemg’oa rapa T.I kwa mama watoto wake
Kutoka hapa ya ‘Ebwana Dah!’ leo tunadondoka na mchizi T.I ambaye bado anaendelea kufanya vyema kunako game ya muziki wa Hip Hop na ngoma zake kadhaa. Siyo chaguo letu bali ni maombi kutoka kwa wasomaji wa safu hii akiwemo Mary wa Mikocheni, Dar es Salaam.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao unaodili na uhusiano wa mastaa wa Ulaya umebaini kwamba, jamaa amewahi kujirusha na mastaa wa kike wasiopungua wanne akiwemo mkewe, Tameka Cottle a.k.a Tiny ambaye ni mama wa watoto wake watatu.

Kabla ya kutulia kwa Tiny na kupanga familia, T.I alianza kujirusha na LeToya Luckett, ambaye alifuatiwa na mwanadada Paula DeAnda ambaye nyota yake ni Nge, kabla jamaa hajadondokea kwa mama watoto wake huyo memba wa kundi la muziki la Xscape mwaka 1998.

Mtandao huo ulizidi kuweka wazi kwamba, mwaka 2006 T.I alihamishia majeshi kwa mrembo
Hoopz, mwenye hobi ya kuuza sura kunako majarida mbalimbali ya Ulaya likiwemo VHI.

Mwana dada huyo pia hupendelea kutinga viguo vya nusu uchi. Bado mtandao huo haujaweka wazi kuwa mchizi bado anaendelea na demu huyo au karudisha majeshi kwa mkewe.

T.I ambaye nyota yake ni Punda, alizaliwa Septemba 25, 1980, huko Atlanta, GA pande za Marekani na kupewa jina la Clifford Joseph Harris, Jr. Mbali na kupewa jina la T.I pia anajulikana kama ‘King Of The South Rubberband Man T.I.P’, mwenye urefu wa futi 5 na nchi 9.
*************

Jizze Mabovu na skendo ya kupiga mtungi
Wanamuita ‘mtoto wa Kiume’ kwasababu ngoma yake yenye jina hilo ili ‘bang’ kwa sana na kulifanya jina lake liwe ni miongoni mwa mastaa wa game ya muziki wa Hip Hop Bongo.

Namzungumzia ‘Jizze Mabovu’ msanii ambae mwishoni mwa wiki iliyopita alikana kuwa na tabia ya kupiga mtungi hadi kupitiliza baada ya kuulizwa swali hilo na mmoja wa wasikilizaji wa kipindi cha XXL kinachorushwa hewani na Kituo cha Radio, Clouds FM cha jijini Dar es Salaam.

Mbele ya DJ Fetty, aliyekuwa akipiga naye intavyuu siku hiyo, Mabovu alisema kwamba, msikilizaji huyo na wengine wanaoendelea kusambaza uvumi wa yeye kuwa na tabia ya kupiga mtungi hadi kupoteza ‘netiweki’ siyo wakweli na kuhoji kwamba kati ya walevi wote wanaokuwa baa ameonekana yeye tu.

“Watu waache hizo, wajaribu kuuliza ishu za msingi, mimi siko hivyo,” alisema Jizze Mabovu ambaye hivi karibuni anatarajia kutoka na kitabu chenye maneno ya mtaani. Je, ni kweli kwamba mchizi siyo mtu wa mitungi kiivyo au anaua soo tu? Jibu utakuwa nalo wewe msomaji na mpenzi wa game ya muziki wa Hip Hop Bongo.
**************************************
Miguu ya Irene Uwoya bomba
Ile siku iyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa shindano hili, Miguu Bomba imewadia, kama tulivyoahidi wiki iliyopita kwamba wiki hii lazima mshindi apatikane na kutangazwa moja kwa moja kupitia hapa Abby Cool & MC George Over The Weekend.

Kwakuwa tuliahidi hivyo hatuna sababu ya kupoteza muda, moja kwa moja tunatamka kuwa, kwa mujibu wa wasomaji na wapenzi wa mpambano huu ambao ndio walikuwa majaji wetu tangu safari ya shindano hili ilipoanza, miguu namba 3 ya kwake Irene Uwoya ndiyo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa kishindo.

Akiwa ni miongoni mwa mastaa wa muvi za Kibongo aliyetokea kujipatia umaarufu kupitia filamu kadhaa alizowahi kucheza, Irene ameibuka na ushindi wa asilimia 80, huku miguu namba 6 ya mpinzani wake, Nakaaya Sumari ikiambulia asilimia zipatazo 20 tu.

Kwa matokeo hayo hatuna budi kuwashukuru wote waliofanikisha shindano hili kumalizika kwa mafanikio, yaani wasomaji, wapenzi na hata wale waliokuwa wakitutumia meseji za kutukatisha tamaa kwani tuliamini zote ni changamoto. Pia tunampongeza Irene Uwoya kwa kuibuka mshindi japokuwa hivi sasa yuko nje ya Bongo. Msomaji, kumbuka kwamba mwisho wa mpambano hili ndiyo mwanzo wa ishu nyingine kali zaidi, endelea kufuatilia safu hii.
*************************************
Richie, Baba Haji: Wahamishia kisa kwenye Solemba
Baadhi ya wadau wa filamu nchini wamesema, wasanii mahasimu nchini, Single Mtambalike ‘Richie’ na Haji Adam ‘Baba Haji’ kucheza filamu moja ya Solemba huku wakiwa hawaivi ni kuzuga wapenzi wa filamu za Kibongo nchini.

Wakipiga stori na safu hii, wadau kadhaa ambao hawakutaka majina yao yacharazwe gazetini walisema kuwa, inawashangaza watu hao wawili kushiriki filamu moja ya Solemba huku siku za nyuma iliripotiwa kuwa ni maadui wakubwa kiasi cha kuapizana kutokuwa pamoja.

Hata hivyo, wadau hao wamesema kuwa, kinachoshangaza ni kuona kwamba, hadithi nzima ya filamu ya Solemba ndiyo kisa ambacho wawili hao waliwahi kuripotiwa kutofautiana, “au siku zile walikuwa wanafanya lieso?” Alihoji mdau mmoja.

Akiongea na kona hii, Richie alijibu mapigo kwa kusema, “yaliyopita kwangu na Baba Haji si sindwele, kwa sasa tuko pamoja tukiganga yajayo.”

Kwa upande wake, Baba Haji alipopigiwa simu na kuulizwa alisema kuwa, kisa cha filamu ya Solemba ambayo itakuwa ‘kitaani’ mwanzoni mwa mwezi Mei hakifanani na kisa chochote ambacho wadau wamewahi kukisikia; “kinachotakiwa hapo ni kusubiri ununue filamu uione mwanzo hadi mwisho, halafu uniambie kama kweli kisa cha Solemba kinafanana na tukio lolote nyuma,” alisema Baba Haji bila kukiri au kukataa ugomvi wa nyuma.

Alisema filamu ya Solemba imeongezeka kionjo ambapo kwa mara ya kwanza, msanii Rose Ndauka anacheza na Teya na kukamua kama kawa.
*******************************

1 comment:

NURU THE LIGHT said...

nimependa kazi yako..karibu home kwangu at nuruthelight..