ROHO SITA: Zimesalia siku 6, idondoke kitaani
Kutoka ndani ya Kampuni ya Tollywood iliyojitoa muhanga kuwapa sapoti wasanii waliojiajiri kunako game ya filamu Bongo tunaambiwa kwamba, zimebaki siku sita tu ili ile muvi, 'Roho Sita' iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na watu wengi wengi idondoke kitaani.
Mkurugenzi wa Filamu za Tollywood Movies, Hamie Rajab alisema na safu hii kuwa, wao kama wasimamizi wa filamu hiyo wameshakamilisha kila kitu kuhusu 'Roho Sita', wanachosubiri ni siku ya kuiingiza sokoni yaani Juni Mosi mwaka huu na kwamba wale wote waliokuwa wanaisubiri wakae tayari.
"Mpaka Tollywood tumeamua kuichukua na kuisimamia ni filamu nzuri ambayo kila atakayepata bahati ya kuiangalia atakubaliana na mimi kwani ni sinema ya kwanza ya kutisha ambayo imeandaliwa kisasa na katika ubora wa kimataifa. Kiukweli sijawahi kuona filamu nzuri kama hii," alisema Hamie Rajabu.
Muvi hiyo ya Roho Sita imewashirikisha mastaa mbalimbali wanaotamba kunako soko la filamu za Kibongo kama Mzee Magari, Thea, Chuchu Hans na wengine kibao. Ni wakati wako wewe Mtanzania kuthamini sanaa za nyumbani zaidi ili kuwapa moyo wasanii wetu.

**************************************
MISS DAR CITY CENTRE: bado siku 25
Zikiwa zimesalia siku ishirini na tano kabla ya kufanyika kwa mpambano wa kumtafuta Miss Dar City Centre, baadhi ya warembo wanaoendelea na mazoezi katika Hoteli ya Lamada, Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na kinyang'anyiro hicho wamesema na safu hii kwamba wanatarajia kufunika vibaya kunako mpambano wa kumtafuta Miss Ilala 2009, Rhobi Chacha anakuhabarisha.
Mabinti hao kwa nyakati tofauti walisema kuwa, wanatarajia kufunika Miss Ilala kwakuwa wengi wao wako poa na wanazo sifa zote za kuwa washindi. "Hata nisiposhinda mimi, mmoja kati yetu anaweza kuibuka na ushindi huo na kutuwakilisha sote, pia inawezekana hata nafasi ya pili na ya tatu tukachukua," alisema mshiriki mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe hapa.
Kwa upande wake muandaaji wa shindano hilo, John Doto aliwataja washiriki hao waliyojitokeza kuwania taji hilo la Miss Dar City Centre kuwa ni Evarin John, Husna Maulid, Elizabeth Ernest, Catherine Rajabu, Brenda Alloye, Emma Gasule, Fatuma Bangi, Bhoke Misiwa, Grace Lyimo, Golder Mwari, Jovina Michael na Mariam Othoman.
Wengine ni Christine Ivan, Anne Mosse, Emma Stelah, Lisa Mashala, Debrah Thomas, Sylivia, Gladyz Shao na Irene Spend (Kijo). Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Amani, Championi, Risasi na Hili la Ijumaa Wikienda, Vodacom, Synco Media na Angaza zaidi kupitia (AMREF).
Msanii aliyepata kuleta mapinduzi makubwa kunako game ya filamu za Kibongo, Steven Kanumba, ameibuka na muvi nyingine inayokwenda kwa jina la 'Fake Smile' akishirikiana na mastaa wengine kibao.
Akipiga stori na Abby Cool & MC George Over The Wekend mwishoni mwa wiki iliyopita, Kanumba alisema kwamba, muvi hiyo ambayo itazinduliwa rasmi June 8, mwaka huu imewashirikisha mastaa kama Anti Ezekiel, Mshindi wa Big Brother Afrika 2007, Richard Bezuidenhout, Neshi Adani na wengine.
"Kwa kifupi filamu yetu inamzungumzia msichana mwenye tabasamu la uongo anayechuma pesa kutoka kwa pedeshee anayemuweka mjini kisha anamuhonga kijana mwingine ambaye hana dili yoyote kimaisha aliyezama katika penzi lake. Ni muvi yenye kuelimisha na kufurahisha ukizingatia kwamba kila mshiriki ameonesha uwezo wa hali ya juu katika nafasi yake," alisema Kanumba.
Mengi zaidi kuhusu muvi hiyo endelea kufuatilia magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers.
Will Smith: KAMPITIA HADI TYRA BANKS!
Staa wa filamu na muziki, Will Smith ndiye tunamcheki leo kunako 'Ebwana Dah!' likiwa ni ombi la wasomaji wengi ambao wamekuwa wakiifuatilia safu hii kwa ukaribu zaidi tangu ilipoanzishwa.
Kama ulikuwa haufahamu, mshkaji amewahi kumpitia hadi mwanamitindo maarufu, Tyra Banks kwenye miaka ya 1993 -94 kabla ya kukutana na Jada Pinkett Smith mwaka 2007 ambaye ndiye mkewe wa ndoa. Hiyo ni kwa mujibu wa mtandao unaodili na ishu za uhusiano wa mastaa wa kiwanja.
Kabla hajafikia huko, Will Smith alianza kujirusha na mwanadada Debbie Allen kabla hajahamishia majeshi kwa Garcelle Beauvais 1992. Mwaka huo huo aliachana na mrembo huyo na kudondokea kwa Sheree Smith kabla ya kumtokea Nia Long 1993.
Aidha, mtandao huo ulisema kwamba mwaka jana, Smith aliisaliti ndoa yake kwa kujirusha na staa wa filamu Charlize Theron kitu ambacho wewe msomaji ulikuwa hukifahamu.
Mchizi ambaye jina lake kamili ni Willard Christopher Smith, Jr. alizaliwa Septemba 25, 1968 yaani miaka 40 iliyopita huko Philadelphia, Pennsylvania Marekani.
Kutoka ndani ya Familia ya Hot Port, safu hii ilipata kupiga stori na msanii Ismail Seif a.k.a Suma G ambaye alisema kwamba, kutokana na ugumu wa game ya muziki ulivyo hivi sasa lazima msanii ukomae na wadau ili uweze kusonga mbele zaidi.
Mchizi ambaye hivi karibuni amerudi upya na ngoma yenye jina la 'Hawakai' alisema kuwa, hivi sasa hatopetea tena kwenye game kama ilivyokuwa siku za hivi karibuni zaidi ataendelea kukomaa na wadau wa muziki (ambao hakupenda kuwataja) mpaka aone mwisho wa sanaa yake.
"Nimegundua kwamba ili niendelee kusonga zaidi sitakiwi nikate tamaa, natakiwa nifanye kazi za nguvu huku nikiendelea kukomaa na wadau wa sanaa yetu na siyo mimi tu wasanii wote wa muziki wa kizazi kipya inabidi wawe hivyo ili ndoto zao ziweze kutimia," alisema Suma.
Zikiwa zimesalia siku ishirini na tano kabla ya kufanyika kwa mpambano wa kumtafuta Miss Dar City Centre, baadhi ya warembo wanaoendelea na mazoezi katika Hoteli ya Lamada, Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na kinyang'anyiro hicho wamesema na safu hii kwamba wanatarajia kufunika vibaya kunako mpambano wa kumtafuta Miss Ilala 2009, Rhobi Chacha anakuhabarisha.
Mabinti hao kwa nyakati tofauti walisema kuwa, wanatarajia kufunika Miss Ilala kwakuwa wengi wao wako poa na wanazo sifa zote za kuwa washindi. "Hata nisiposhinda mimi, mmoja kati yetu anaweza kuibuka na ushindi huo na kutuwakilisha sote, pia inawezekana hata nafasi ya pili na ya tatu tukachukua," alisema mshiriki mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe hapa.
Kwa upande wake muandaaji wa shindano hilo, John Doto aliwataja washiriki hao waliyojitokeza kuwania taji hilo la Miss Dar City Centre kuwa ni Evarin John, Husna Maulid, Elizabeth Ernest, Catherine Rajabu, Brenda Alloye, Emma Gasule, Fatuma Bangi, Bhoke Misiwa, Grace Lyimo, Golder Mwari, Jovina Michael na Mariam Othoman.
Wengine ni Christine Ivan, Anne Mosse, Emma Stelah, Lisa Mashala, Debrah Thomas, Sylivia, Gladyz Shao na Irene Spend (Kijo). Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Amani, Championi, Risasi na Hili la Ijumaa Wikienda, Vodacom, Synco Media na Angaza zaidi kupitia (AMREF).
***************************************
KANUMBA: Kutoka na Fake SmileMsanii aliyepata kuleta mapinduzi makubwa kunako game ya filamu za Kibongo, Steven Kanumba, ameibuka na muvi nyingine inayokwenda kwa jina la 'Fake Smile' akishirikiana na mastaa wengine kibao.
Akipiga stori na Abby Cool & MC George Over The Wekend mwishoni mwa wiki iliyopita, Kanumba alisema kwamba, muvi hiyo ambayo itazinduliwa rasmi June 8, mwaka huu imewashirikisha mastaa kama Anti Ezekiel, Mshindi wa Big Brother Afrika 2007, Richard Bezuidenhout, Neshi Adani na wengine.
"Kwa kifupi filamu yetu inamzungumzia msichana mwenye tabasamu la uongo anayechuma pesa kutoka kwa pedeshee anayemuweka mjini kisha anamuhonga kijana mwingine ambaye hana dili yoyote kimaisha aliyezama katika penzi lake. Ni muvi yenye kuelimisha na kufurahisha ukizingatia kwamba kila mshiriki ameonesha uwezo wa hali ya juu katika nafasi yake," alisema Kanumba.
Mengi zaidi kuhusu muvi hiyo endelea kufuatilia magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers.
*************************************
Will Smith: KAMPITIA HADI TYRA BANKS!
Staa wa filamu na muziki, Will Smith ndiye tunamcheki leo kunako 'Ebwana Dah!' likiwa ni ombi la wasomaji wengi ambao wamekuwa wakiifuatilia safu hii kwa ukaribu zaidi tangu ilipoanzishwa.
Kama ulikuwa haufahamu, mshkaji amewahi kumpitia hadi mwanamitindo maarufu, Tyra Banks kwenye miaka ya 1993 -94 kabla ya kukutana na Jada Pinkett Smith mwaka 2007 ambaye ndiye mkewe wa ndoa. Hiyo ni kwa mujibu wa mtandao unaodili na ishu za uhusiano wa mastaa wa kiwanja.
Kabla hajafikia huko, Will Smith alianza kujirusha na mwanadada Debbie Allen kabla hajahamishia majeshi kwa Garcelle Beauvais 1992. Mwaka huo huo aliachana na mrembo huyo na kudondokea kwa Sheree Smith kabla ya kumtokea Nia Long 1993.
Aidha, mtandao huo ulisema kwamba mwaka jana, Smith aliisaliti ndoa yake kwa kujirusha na staa wa filamu Charlize Theron kitu ambacho wewe msomaji ulikuwa hukifahamu.
Mchizi ambaye jina lake kamili ni Willard Christopher Smith, Jr. alizaliwa Septemba 25, 1968 yaani miaka 40 iliyopita huko Philadelphia, Pennsylvania Marekani.
***********************************************
SUMA G: Ntaendelea kukomaa na wadauKutoka ndani ya Familia ya Hot Port, safu hii ilipata kupiga stori na msanii Ismail Seif a.k.a Suma G ambaye alisema kwamba, kutokana na ugumu wa game ya muziki ulivyo hivi sasa lazima msanii ukomae na wadau ili uweze kusonga mbele zaidi.
Mchizi ambaye hivi karibuni amerudi upya na ngoma yenye jina la 'Hawakai' alisema kuwa, hivi sasa hatopetea tena kwenye game kama ilivyokuwa siku za hivi karibuni zaidi ataendelea kukomaa na wadau wa muziki (ambao hakupenda kuwataja) mpaka aone mwisho wa sanaa yake.
"Nimegundua kwamba ili niendelee kusonga zaidi sitakiwi nikate tamaa, natakiwa nifanye kazi za nguvu huku nikiendelea kukomaa na wadau wa sanaa yetu na siyo mimi tu wasanii wote wa muziki wa kizazi kipya inabidi wawe hivyo ili ndoto zao ziweze kutimia," alisema Suma.
No comments:
Post a Comment