Friday, June 5, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Top Band Full mademu
Galacha wa Bongo Flava, Khaleed Salum Mohamed ‘TID’ akiwa na wanaye wa Top Band, wamehamishia mizuka yote kwenye Ukumbi wa Sanaa Pub, uliopo ndani ya Hoteli ya Movenpick, Richard Bukos ndiye ameleta mnuso huu.

Meneja wa Top Band, Hamis Dakota aliiambia Showbiz kuwa wamepata mkataba wa kupiga shoo kwenye hoteli hiyo kila Alhamisi na kwamba wanaichukulia ‘chansi’ hiyo kama vile ni ya dhahabu hivyo watailinda kwa nidhamu ya hali ya juu.

Dakota alinena: “Ni shoo ya kipekee kila Alhamisi, mbali na burudani ya Top Band ikiongozwa na TID, pia wanamuziki mbalimbali wanaowika, wakifika watakuwa wanapata nafasi ya kusema na jukwaa hivyo shoo zetu zitakuwa na sura ya aina yake.”

Apati ofu zati, ShowBiz imegundua kwamba Top Band ndiyo inayoongoza kwa kuwa na dadaz wengi (kama wanavyoonekana pichani) kuliko nyingine zinazofanya Bongo Flava zikiwemo B-Banda ambayo haina ‘du’ hata mmoja huku Machozi Band ya Jide ikiwa na wasichana wawili tu.

****** **********************************


Zay B

Sister P


Zuhura


Besta

Warembo wetu kupotea kwenye game
Hii ni siri kiduchu
Haijapita hata miongo miwili tangu kizazi kipya kianze ‘kushaini’, lakini tayari watendaji wakuu wameanza kuchoka, wanaingia mitini. Gents wanapotea lakini ladies fani inawashinda, kumbe tatizo ni washikadau wa kiume.

Nini siri, hawajui kuimba au kuna kilichopo nyuma ya pazia? ShowBiz ndiyo yenye jeuri ya kuweka kila kitu kweupe! Uchunguzi makini tulioufanya unabainisha kuwa upo unyanyasaji mkubwa wa ngono kwa wasanii wa kike.

Intavyuu tuliyofanya na baadhi ya dadaz ambao hawavumi kitaani kama ilivyokuwa zamani, inafichua kwamba wasanii wengi wa kike wanaona game ni ‘tafu’ kwa sababu kila hatua wanayopita ni lazima waombwe rushwa ya ngono ili kutambulika.

Hatua ya kwanza, mtu anayemshika mkono kumpeleka studio hutaka fidia ya penzi, kabla ya kuingiza voko prodyuza naye huanza makeke akitaka aonjeshwe kiduchu ndiyo kazi iendelee, redioni nako DJ hachezi wimbo kabla ‘hajamcheki’.

Kote huko tisa, kumi ni promota ambaye yeye hutaka mawili, kwanza ni ‘kumpromoti’ kimwili halafu muziki ufuate, ndiyo maana warembo kwa kuficha miili yao huingia mitini.

Kuna wale ambao bila kujua, lakini wakiwa na kiu ya kutoka waliamua kujirahisi na kukubali kutoa penzi, lakini walikuwa used na baadaye wakawa abused. Baada ya kutumiwa walipigwa teke, hawana ujanja tena.

Dada zetu wengi wanapotea, ukiwauliza wanajibu muziki mgumu. Gents wanatoweka na kurudi lakini ladies kimyaaaaa! ShowBiz inawanyaka wadau wanaoendekeza ngono, inawataka waache kuwanyanyasa dadaz wetu, otherwise itataja majina.
************************************

Bushoke kwa Voko safi, pamba x
Stadi wa Bongo Flava, Ruta Maximilian Bushoke ni mmoja wa mastaa nchini ambao wanachechemea katika suala zima la milipuko ya mavazi a.k.a bling bling, zat minz hawajui kupigilia pamba.

Bushoke ambaye zama za kale alikuwa anajiita Ruta B, enzi hizo akiwa na Kundi la Makole Hexagon, tathmini inaonesha kuwa jamaa ni mkali asiyepingika katika voko lakini kwenye pamba ni sifuri kubwa.

Hapa juzi-kati, tulizidaka picha ambazo Bushoke alipozi pamoja na ‘makachaa’ wenzake, Heri Samir ‘Blu’ na Albert Mangwea ‘Ngwair’, lakini ndani yake ‘mchizi’ wa Makole alipotezwa vibaya na wanaye hao ambao walipendeza si kitoto.

Showbiz inamkumbusha mshikaji kuwa ni lazima ajue ‘kukop’ katika tabaka la wana-sanaa. Ni hayo tu!
************
Moro mpo tayari kwa prodyuza?
"Nimetia maguu Moro, hapa nitashirikiana na wanangu kuinua muziki, si unajua hii ndiyo ajira ya wazi kwa vijana wengi siku hizi Bongo?” Ni maelezo kisha swali kutoka kwa ‘handsome boy’, Robert Frank, ambaye ni prodyuza anayemudu zaidi Bongo Flava.

Robert ambaye hana a.k.a kama ilivyo kwa wanamuziki wengi, alitoa maelezo yake Showbiz kwamba ameamua kujikita Mji Kasoro Bahari akitambua fika kuwa mzuka wa muziki mjini humo upo juu ila unataka msukumo wa wadau.

“Kwa sasa nimeachia dude moja, nimekamua mwenyewe na ‘nimeprodyuzi’ kwa mikono yangu, linaitwa “Shujaa Wangu”, nitafungua studio hapa hapa Moro, pia tuna klabu itazinduliwa mwezi ujao itaitwa Four Stars, kwahiyo tutakuwa tunapika nyimbo studio na kuyarusha klabu, lazima tutoke,” alisema Robert.
******
compiled by mc george

No comments: