Katika medani ya afya, kama kuna kitu muhimu zaidi kuliko vyote katika mwili wa binadamu, basi ni maji. Bila maji mwili si lolote si chochote. Mgonjwa anapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hudamu ya kwanza anayopewa kabla ya tiba ni kutundukiwa dripu ya maji. Bila maji hata dawa haiwezi kufanyakazi.
Bila maji hakuna kitu kinachoweza kufanya kazi mwilini. Kwa mujibu wa wataalamu wetu, kati ya asilimia 50-60 ya mwili wa binadamu, umetokana na na maji. Inaelezwa kuwa mtu mwenye afya njema, anakadiriwa kuwa na lita 42 za maji mwilini mwake!
Ili mwili ufanye kazi yake vizuri, mtu huyo anatakiwa ku ‘balansi’ kiwango hicho cha maji wakati wote, upungufu wowote wa maji mwilini huweza kuonesha athari ndogo, za kati na zile kubwa ambazo matokeo yake huwa mabaya.
HUWEZI KUISHI BILA MAJI
Unawe kuishi kwa siku nyingi bila kula chakula, lakini huwezi kuishi zaid ya siku tatu bila kunywa maji, hivyo utaona ni kwa kiasi gani maji ni muhimu katika miili yetu. Kwa bahati mbaya sana watu wengi tunapatwa na matatizo mengi ya kiafya kutokana na kutokuwa na maji ya kutosha mwilini na bila kujijua.
KUNYWA MAJI WAKATI GANI?
Kwa kuwa maji ni muhimu mwilini na ni kitu kinachohitajika kwanza kabla ya kitu kingine, unapaswa kujenga mazoea ya kunywa maji mengi kila siku. Watu wengi wana tabia ya kunywa maji pale wanaposikia kiu, hilo ni kosa!
Inaelezwa kuwa, unapofikia hatua ya kusikia kiu, tayari mwili unakuwa umepungukiwa kiasi fulani cha maji na kiu huwa ni dalili mbaya. Weka mazoe ya kunywa maji kabla hujasikia kiu kwa mpangilio maalum, elewa kwamba kwa wastani kila siku unapaswa kunywa maji kiasi cha lita moja na nusu hadi 3.
Mahitaji yako ya kunywa maji yataongezeka zaidi ikiwa ni mtu wa mazoezi au unayefanyakazi nzito zinazokufanya utoke jasho jingi ambalo hupunguza maji mwilini. Hivyo kiwango cha chini ni lita moja na nusu, usipokunywa kiasi hicho kwa siku elewa utakuwa hujautendea haki mwili wako.
DALILI ZA KUPUNGUKIWA MAJI
Kuna dalili kadhaa ambazo hujionesha pale mwili unapopungikiwa maji, hata kwa kiasi kidogo. Dalili hizo ni pamoja na kusikia kiu, kizunguzungu, kujisikia kuchoka, kukosa umakini na hata kusikia kichefuchefu.
Upungufu wa maji mwilini unapozidi na kuwa mkubwa, husababisha matatizo kwenye mfumo wa hewa na figo ambalo hushindwa kufanyakazi yake ipasavyo, halikadhalika joto la mwili huweza kuongezeka.
ANGALIA MKOJO WAKO
Kigezo kikubwa cha kuangalia kiwango cha maji mwilini mwako kama kiko sawa au kuna upungufu ni rangi ya mkojo wako. Ukikojoa mkojo mzito wa rangi ya njano yenye wekundu ndani yake na harufu kali ni dalili tosha kuwa huna maji ya kutosha mwilini. Mkojo unaopaswa kukojoa kila wakati ni ule wa njano iliyopauka(pale yellow) au mkojo mweupe usio na harufu.
Elewa kwamba, maji ndiyo kila kitu na kma huna tabia ya kunywa maji, bila shaka utakuwa na matatizo mengi ya kiafya ambayo umeshayazoea na kuyaona ni ya kawaida, lakini kadri siku zinavyokwenda yanakuwa sugu na yatakuwa hatari kwa maisha yako pale siku yatakapoibuka kwa kasi.

1 comment:
Maji ndio uhai hata mwenyezi mungu kasema nimewajaaliwa maji kila kitu kiwe hai, bila maji hatuishi.
Post a Comment