Friday, June 26, 2009

SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WA MICHAEL J!

Michael akiwapa 'hi' mashabiki na wanahabari wakati akiongea nao Machi 5 mwaka huu...pengine ndiyo moja ya picha zake za mwisho mwisho kupiga nchini Uingereza!
Picha yake ya mwisho nchini Uingereza aliyopiga wakati wa press
Moja ya mabango ya Onesho lake la Uingereza
Michael akishangiliwa na wanahabari wa Uingereza Machi 5 mwaka huu
Mashabiki wakiwa nje ya hospitali alimokimbiziwa kujaribu kuokoa maisha yake

Bila kujua kwamba amebakiza siku 113 tu za kuishi duniani, Michael Jackson alipokutana na waandishi wa habari mjini London Machi mwaka huu, aliwaahidi mashabiki wake wa Uingereza kuwa onesho lake lililopewa jina la THIS IS IT TOUR lililopangwa kufanyika O2 Arena kuanzia July 09 mwaka huu, lingekuwa onesho kali la kufungia pazia katika historia yake ya maonesho!

Masikini, hilo halikutokea kama alivyotaka, kwani Mungu naye tayari alikuwa na mipango yake isiyobadilika. Inaelezwa kuwa tiketi za onesho lake zilikuwa zikiuzwa kati ya paundi 50 na 75 na zilitararajiwa kumuingizia jumla ya paundi milioni 175!!!! Hii ingekuwa imemaliza kabisa matatizo yake ya kifedha aliyokuwa nayo!

katika press hiyo, Michael aliahidi kwa kusema maneno yafuatayo kwa wanahabari wa Uingereza: “I’ll be performing the songs my fans want to hear. This is really it. This is the final curtain call. I’ll see you in July.” (Nitaimba nyimbo wanazopenda mashabiki wangu kuzisikia, huu ni uhakika. Huu ni wito wangu wa mwisho, tutaonana mwezi wa saba)

HAKIKA KIFO HAKINA HURUMA, REMY ONGALA ALISHAIMBA!

No comments: