Monday, June 29, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ




Michael Jackson
*Familia
*Kazi
*Uhusiano
*Kifo chake

Dunia bado inazizima kwa majonzi kufuatia kifo cha mfalme asiyepingika wa muziki wa Pop duniani. Keep your head up, tunamzungumzia Michael Jackson a.k.a The Wako Jacko.

Mtu mzima The Jacko ambaye alikamilisha memory zake za uhai duniani usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita alifanya mengi, hivyo kupitia hapa utaona baadhi ya harakati ambazo alizifanya wakati pumzi yake ikiwa on air.

Juni 25, 2009, The Jacko akiwa kwenye nyumba yake ya kupanga iliyopo North Carolwood Drive, mjini Holmby Hills, jijini Los Angeles, Marekani alikumbwa na shambulio la moyo na jitihada za daktari wake binafsi kuokoa maisha yake hazikuzaa matunda.

Wahudumu wa tiba kutoka kikosi cha Los Angeles Fire Department, walipokea emergency call na dakika tisa baadaye walitinga mjengoni kwa The Jacko. Wakati hayo yakifanyika tayari ilikwishaelezwa kwamba alikuwa hawezi kupumua.

Juhudi za kumuokoa ziliendelea kwa kumpeleka kwenye Hospitali ya Ronald Reagan UCLA Medical Center na baada ya saa moja ikaelezwa kuwa mtemi huyo wa mauzo ya muziki duniani amekumbwa na shambulio la moyo na kuvuta.

The Jacko aliripotiwa kuiaga dunia saa mbili baada ya kufikishwa kwenye hospitali hiyo ya Ronald Reagan.

TUKUMBUKE HARAKATI ZAKE
Mtu mzima The Jacko alifanya mambo mengi duniani. Wengi wamekuwa wakisikia na kuongea mambo tofauti bila kuwa na data. Abby Cool and MC George over the weekend inaweza kukupa yafuatayo.

KAZI
Alianza kuonesha maajabu kwenye muziki akiwa na umri wa miaka 11 wakati huo akiwa memba wa kundi marehemu la The Jackson 5 mwaka 1969 na miaka miwili iliyofuata, wakati huo akiwa na umri wa miaka 13 alianza kufanya kazi kama solo artist ingawa alibaki kundini.

Akiwa na kaka zake wa damu ambao ndiyo memba wenzake wa kundi hilo, Jacko alikuwa akionesha ufundi wa hali ya juu katika kuichezea sauti yake kwa ufundi wa hali ya juu, pia akiutumikisha vilivyo mwili wake kwenye kushambulia jukwaa.

Akitambuliwa bila kipingamizi kama King of Pop, albamu yake ya Thriller ambayo aliiachia mwaka 1982 ndiyo inayoongoza kwa mauzo duniani ambapo aliuza nakala zaidi ya milioni 100, wakati kazi zake nyingine kama vile Off the Wall (1979), Bad (1987), Dangerous (1991) na History (1995) zilipiga bao vibaya sokoni.

Anashika nafasi ya nne kwa mauzo jumla kwani inakadiriwa kwamba jumla ya nakala alizouza katika maisha yake ya muziki ni zaidi ya milioni 750 lakini chini ya milioni 999.

Kundi la Beatles la UK ndilo linaloongoza kwa mauzo kwa kuwa limekwishapiga bei zaidi ya nakala bilioni moja, likikaribiwa na msanii Elvis Presley, wakati Bing Crosby akimzidi kiduchu The Jacko.

Singo Sream ambayo Jacko aliifanya na dada yake, Janet Jackson na kuingia kitaani Juni 13, 1995 ndiyo video yenye gharama kubwa zaidi kwenye matengenezo kwani ilimbidi mtu mzima aingie mfukoni na kuchomoa dola milioni 7 sawa na shilingi bilioni 9.1 ili kuikamilisha.

TUZO
Jacko amekwishanyakua tuzo za kumwaga na jumla ya awadi kubwa zaidi ya 197 ambazo amewahi kuzibeba katika utumishi wake wa muziki.

Tuzo hizo na jumla yake kwenye mabano ni kama ifuatavyo; American Music Awards (22), Billboard Awards (40), BRIT Awards (7), Golden Globe Awards (1), Guinness World Records (13), MTV Awards (13), NAACP Image Awards (14), RIAA Awards (56) na World Music Awards (12).

Kama msanii mwenye heshima kubwa duniani alikwishatia maguu Hollywood Walk of Fame, pia mwaka 1984 alipewa mwaliko rasmi wa kutinga Ikulu ya Marekani, White House na kupata fursa ya kupiga domo na rais wa nchi hiyo kwa kipindi hicho, Ronald Reagan.

UHUSIANO
Watu wanachooonga, lakini ukweli ni kwamba The Jacko ingawa alikuwa anaonekana 'namna gani' lakini alikuwa fundi wa kubadili totoz kimtindo.

Baadhi ya wadada alioonja nao urojo ni Maureen McCormick, Shana Magantal, Stacy Lattisaw, Tatiana Thumbtzen, Tatum O’Neal, Stephanie Mills, Brooke Shields, Lisa Marie Presley, Debbie Rowe, Grace Rwaramba na Jessica Barnes ambao jumla yao ni 11.

FAMILIA
The Jacko alizaliwa Gary, Indiana, Illinois, Chicago Agosti 29, 1958. Baba yake anaitwa Joseph Walter “Joe” Jackson na mama yake ni Katherine Esther. Ni wa saba kati ya tisa kwenye familia yake.

Ndugu zake wengine ni Rebbie, Jackie, Tito, Jermaine, La Toya, Marlon, Randy na Janet. Mzee Jackson ni Shahidi wa Yehova pia mara kwa mara alikuwa akidaka MIC na kupiga shoo pamoja na kaka anayekwenda kwa jina la Luther kwenye bendi ya The Falcons ambayo ilikuwa inakita R&B.

Jacko ameacha watoto watatu wa kiume, ambao ni Prince Michael I , Paris na
Blanket.
*********************
Miss Dar City Centre
Watoto watano waliobahatika kupenya hatua ya Tano Bora kwenye shindano la Miss Dar City Centre, usiku wa kamkia juzi walipewa 'halla' na wadau pamoja na audience kwa jumla kwa vile walikamata ile mbaya.

Du’z hao, hata kabla jaji kuwataja tayari dalili zote zilionesha kwamba wao ndio watakaochuana katika nafasi tano za juu just because kila mtu ukumbini aliappreciate kutokana na mvuto wao wa kimisi.

Shughuli kamili ilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam ambapo mahudhurio yalikuwa ya kutosha, hivyo kuonesha kwamba Miss Dar City Centre is now backing to the position.

Katika fainali hiyo, mtoto mzuri Sylvia Shally alivaa crown, duu mwingine aliyedatisha vilivyo, Grads Shao alidaka namba mbili huku Anne Moses akiibuka na nafasi ya tatu.

Mrembo Magreth Peter alifanikiwa kunyaka nafasi ya nne na Fatma Bongi alijificha kwenye namba tano, hivyo kujihakikishia kutinga hatua ya mbele zaidi.

Watoto hao watano ndiyo watakaoungana na wengine wa vitongoji vingine waliopata nafasi za juu na kuchuana kwenye Fainali za Miss Ilala 2009 ambazo mwaka huu zitachukua nafasi kwenye Ukumbi wa Karemjee Hall, Dar.
compiled by mc george

No comments: