Saturday, July 25, 2009

MREFU KULIKO HASHIM THABIT?

Kama ulifikiri Hashim Thabit ndiye mrefu peke yake Bongo, ulikosea....kuna kijana mwingine ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko hata Hashim..yuko maeneo ya Gongolamboto/Banana jijini Dar es salaam. Juzi kati alilleta kizaa zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey Kariakoo...alikuwa kivutio kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa na kumgombania kupiga nae picha..kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa Buku..jamaa aliondoka na kama fote hivi! Hapo unapomuona yumo ndani ya saluni moja na alikuwa anakaribia kugusa siling! mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini...tunaendelea kumfuatilia ili kuwaletea data zake kamili, kwani watu wanasema urefu wa jamaa ni DILI!

No comments: