Monday, August 3, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!


Madhila no. 2: Itawaliza wengi
Nakala ya pili ya muvi inayokwenda kwa jina la Madhila (Part II) inaweza kuweka rekodi ya kuwaliza watazamaji wengi zaidi, Abby Cool & MC George imeichungulia na kujionea tofauti.

Ndani ya Madhila Part II, mateso kwa kijana Salim Mbwana ambaye anabeba uhusika wa jamii ya watu wenye ulemavu ni makubwa kuliko ilivyokuwa kwenye nakala ya kwanza, pia inaonesha jinsi walemavu wanavyoonekana si kitu ndani ya familia zao.

Hata hivyo, pamoja na mateso hayo baadaye Mbwana ambaye ni mlemavu katika hali halisi, anaonesha jinsi ambavyo mdharau mwiba, guu linaweza kuota tende, anafanya ‘wandaz’ kwa kudhihirisha kuwa kumbe inawezekana.

Hili ni dude lingine ambalo limekwenda kidato, na litaingizwa kitaani kwa ufanisi wa hali ya juu na kampuni mkombozi wa vipaji nchini ya Tollywood Movies.

Ndani ya filamu hiyo, pia yumo galacha Riyama Ali, staa wa tangazo la Haki Elimu, Nuru Njaidi (Huba) na wengine kibao wakiwemo Joyce Eliya (Bi. Mashavu), Subira Waziri (Kuluthum), Alfred Malima (Smart), Rahima Salim (Radia, Naima Salim (Nadia) na Jacob Daudi (Sam).
*******************************


The Director ya Kanumba kitaani J5,
Staa wa sanaa za maigizo nchini, Steven Kanumba, ameonesha umakini wa hali ya juu kazini na Jumatano anatarajia kudondosha mtaani muvi ambayo imesimama kwa jina la The Director.

Hii inakuwa ni sinema yake nyingine kucheza na Wanigeria kwa mafanikio makubwa, kama vile ilivyokuwa Dar to Lagos, Cross My Sin ambazo zilifanya vizuri sana katika soko la muvi za kibongo.
**********************************


Wasanii Tears on Valentine Day wakiwa mazoezini kambini

****************************************************8

Tuzo za Channel O
Piga kura kwa Black Rhino, FA
Once again, Mtanzania unaweza kuwa daraja la wasanii wawili nchini, kuibuka na tuzo ya kimataifa. Wanazungumziwa Nicolas Haule ‘Black Rhino’ na Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.

Bila shaka unajua kilichopo kwamba Black na FA ni among the nominees kwenye tuzo za Channel O 2008-09, hivyo unatakiwa kudondosha kura yako kwa wanetu hao.

It easy to make them hero! Black kupitia wimbo wake Black Chata, ametajwa kwenye categories mbili, Video Bora Afrika Mashariki (Most Gifted East Afrika Video) na Video Bora ya Hip Hop (Most Gifted Hip Hop Video).

FA pia kupitia ngoma yake Naongea na Wewe ambayo amefanya kolabo na Ambwene Yesaya ‘AY’ ametajwa kwenye vipengele viwili, Video Bora Afrika Mashariki (Most Gifted East Afrika Video) na Wimbo Bora wa Kushirikiana (Most Gifted Group a.k.a Duo).

Utaona kwamba Black na FA wanakamuana pua kwenye category moja ambayo ni Video Bora Afrika Mashariki; lakini siyo ishu, muhimu hapa ni kuleta heshima home.
Unawezaje kupiga kura? Video Bora Afrika Mashariki, kwa Black tuma SMS yenye maneno 13E kwenda namba +27839208400 au FA, unaandika 13B unatuma kwenye nambari +27839208400.

Video Bora ya Hip Hop, unampigia kura Blak kwa kuandika SMS yenye maneno 10F na unaituma kwenda nambari +27839208400, wakati ili FA ashinde Wimbo Bora wa Kushirikiana, unaandika meseji yenye maneno 4E kisha unai-send namba +27839208400. Inawezekana!
*******************************

TMK family, Tip Top
Almanusura wauwe!
Ishu kibao zimesharipotiwa about muungano wa TMK Wanaume Family na Tip Top Connection, lakini hili linaweza likawashangaza wengi. Do u know which is ringing the bell? Guyz wamethibitisha kwamba Bong Flava is still alive.

Siku chache zilizopita jamaa almanusura wapoteze maisha ya baadhi ya mashabiki wao ambao walifurika kunako shoo yao kubwa iliyochukua nafasi pande za Iringa, wakati washkaji walipokuwa wakiutambulisha umoja wao kupitia pini linalosimama kwa jina la Chama Kubwa.

Mbali na ngoma hiyo, familia hizo mbili kongwe katika industry ya burudani Bongo, zilichukua nafasi kutambulisha albamu za wasanii wake watatu, Amani James Temba ‘Mheshimiwa’, Hamad Ali ‘Madee’ na Said Fella ‘Mkubwa’.

“Tulianza Sumbawanga, tukashuka Mbeya kisha tukamalizia Iringa. Kiukweli shoo zote zilikuwa na mafanikio makubwa lakini Iringa ilikuwa balaa zaidi.

“Mashabiki walifurika Uwanja wa Samora mpaka baadhi yao kuchungulia kifo kutokana na msongamano. Tunamshukuru Mungu ulinzi ulikuwa wa kutosha, askari walilazimika kuwachomoa wale waliokuwa wamebanwa ili kunusuru maisha yao,” alisema Fella.

Mkubwa pia aliongeza kuwa baada ya mafanikio hayo, hivi sasa wanajipanga kwa mashambulizi mengine kwa ajili ya Moro ambako watakita nyama chini kwenye Uwamnja wa Jamhuri na Bwalo kabla ya kutua Dom kwenye Dimba la Jamhuri.
******************************

Lil mama: Alivyochangia penzi la Chriss Brown na Rihanna
She is underage but kwenye malavidavi anaonekana kuyachangamkia kwa sana. Mtajwa hapo ni rapa, Niatia Jessica Kirkland a.k.a Lil Mama.

Oktoba 4, mwaka huu ndiyo atatimiza miaka 20, hivyo bado anajidai na 19, lakini inafunuliwa kuwa miaka miwili iliyopita (2007) akiwa na miaka 17 alikuwa akijikunja kimahaba na mwanamuziki handsome boy, Chris Brown.

Mshangao ni kwamba wakati huo Lil Mama akitoa urojo kwa Chris, dogo huyo ndiyo kwanza alikuwa analinogesha penzi kwa sweet-baby wake, Robyn Rihanna Fenty, kwa maana hiyo alikuwa anawachanganya.

Hata hivyo, Lil Mama hana listi ndefu, kwani katika tovuti inayodili na ishuz za mastaa wa kiwanja, inaonekana kwamba mbali na kuchangia penzi la Chris na Rihanna, pia kipindi cha mwaka 2007 hadi 2008 alijiweka kwa Soulja Boy.

Alizaliwa Harlem, Manhattan, New York Oktoba 4, 1989. Nyota yake Mzani, ana urefu wa futi 5.65, rangi ya macho yake ni Brown-Dark, dini yake ni Mkristo na alibukua Edward R. Murrow High School.

compiled by mc george

No comments: