WIKI ILIYOPITA TULIANZA MAKALA HAYA KWA KUANGALIA SUALA LA UFANYAJI WA ENEMA KWA AJILI YA KUSAFISHA TUMBO, ZOEZI AMBALO HUSAIDIA KUONDOA SUMU MWILINI NA HIVYO KUEPUSHA MWILI NA MARADHI, ENDELEA... UTAJIJUAJE KAMA UTUMBO WAKO NI MCHAFU?
Ni rahisi sana kujitambua kwamba utumbo wako ni mchafu, lakini kwa bahati mbaya watu wengi huwa hawazitambui dalili hizo na wanaozitambua huzipuuzia. Dalili ya kwanza ni harufu mbaya kutoka mdomoni, licha ya kupiga mswaki kila siku. Harufu mbaya unayoisikia mdomoni haitoki mdomoni, bali hutoka tumboni.
Dalili nyingine ni harufu mbaya ‘unapopumua’, wenye matumbo masafi huwezi kusikia pumzi zao zikitoa harufu mbaya. Dalili nyingine ni kukosa kwa choo kwa siku kadhaa. Katika hali ya kawaida, binadamu anatakiwa kupata choo angalau mara moja kwa siku kama siyo mara tatu. Unapokosa choo kwa siku nzima ili hali unakula mara tatu au mbili kwa siku, tena ‘plate’ nzima, ujue una matatizo.
Lakini dalili nyingine na ambayo imefanyiwa utafiti wa kisayansi, inapatikana usoni mwa kila mtu! Uso wa binadamu unaelezea viungo vyote vilivyomo tumboni kama mchoro wa makala haya unavyoonesha. Kila kiungo kilichomo tumboni, unaweza kujua hali yake kwa kuangalia kiungo kinachofanana nacho usoni.
Kuanzia sasa, anza kujiangalia pamoja na afya yako kwa mtizamo mwingine. Jiangalie ndani ya mwili wako kupitia sura yako, utaweza kujijua ulivyo tumboni mwako kwa kuangalia uso wako tu, kwani kila kitu kinachoendelea tumboni, kinaonekana usoni mwako:
Katika mchoro wa kwanza, viungo vyote vya tumboni (kama mchoro wa pili unavyoonesha mfumo wa tumbo) vimeoneshwa usoni. Napenda kuzungumzia zaidi sehemu ya utumbo mkubwa (Large Intestine) ambao ndiyo mada yetu ya leo na ambao ndiyo huweza kusafishwa kwa kutumia Enema.
Mtu ambaye utumbo wake mkubwa umejaa uchafu, utamjua kwa kumuangalia chini ya macho (kama mchoro unavyoonesha), chini ya macho ya watu hawa huwa yamevimba, na kuvimba huko huwa kunamaanisha utumbo wake umejaa choo au ana matatizo ya figo.
Kama tulivyosema hapo awali, kujaa choo katika utumbo mkubwa ndiyo mwanzo wa matatizo mengine ya kiafya, mifumo mingine ya mwili hushindwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo kusababisha matatizo kama shinikizo la damu, saratani, kisukari, matatizo ya figo na kibofu cha mkojo, magonjwa ya viungo na maradhi mengine hata usiyoyajua.
Baada ya kuanza na utangulizi huu, nafikiri sasa umeelewa Enema ina umuhimu gani katika afya zetu. Kama kweli tunataka kuishi maisha yaliyo huru dhidi ya maradhi, hatuna budi kuifanya enema. Wiki ijayo tutaelezea ufanyaji wa enema hatua kwa hatua, kwani ni rahisi na kila mtu anapaswa kufanya japo mara moja kwa mwaka ili kuondoa na kujikinga na maradhi.
Itaendelea wiki ijayo..