Friday, March 27, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Ali Kiba
Dully Sykes
Dar es Salaam Hands Up
Shindano lako la kijanja zaidi, ‘Dar es Salaam Hands Up’ (Dar es Salaam Mikono Juu) limeingia kunako hatua nyingine, baada ya wiki iliyopita kuwapata wakali wa Bongo Flava watakaoiwakilisha vyema Wilaya ya Kinondoni, leo tunadondoka na wasanii kutoka pande za Ilala waliyotajwa na wasomaji kuiwakilisha wilaya yao.

Wasanii hao kutoka Wilayani Ilala ni Dully Sykes, Blue, Ali Kibba, Chidi Benz (La Familia), Soggy Dog, Suma G, Zay B na Akili The Brain. Kabla sijaendelea mbele zaidi nakukumbusha kwamba, shindano hili linazihusu Wilaya tatu za Dar es Salaam, Kinondoni, Ilala na Temeke ambapo wewe msomaji na mpenzi wa burudani hii utatuambia ni ipi ina wasanii wakali.

Baada ya kuwapata wasanii hao kutoka Ilala, sasa tunaelekeza macho yetu pande za Temeke ambapo wewe msomaji na mpenzi wa mpambano huu unatakiwa utuambie ni msanii gani anastahili kuiwakilisha wilaya hiyo.

Hivi sasa unatakiwa ututumie ujumbe mfupi ukimtaja msanii wa Temeke ambaye unadhani anastahili kuiwakilisha wilaya hiyo kunako shindano hili, si msanii ambaye unamuona hapa pichani. Baada ya kufanya hivyo tuma kwenda simu namba 0787-110 173. Mwisho wa kupokea kura zenu ni siku ya Jumanne mchana.
*************************************
Blue
Bushoke: Sasa ni zamu ya Bukoba
Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kuifikia Sikukuu kubwa ya Pasaka, msanii Rutta Maximilian Bushoke anatarajia kujirusha na wakazi wa Bukoba, Mkoani Kagera katika kuadhimisha siku hiyo.

Ndani ya ShowBiz msanii huyo ambaye bado ni memba wa kundi la Makole Hexagon lenye maskani yake pande za Dodoma, alisema kwamba baada ya kuzunguka sehemu mbalimbali nchini akiitambulisha albamu yake mpya, ‘Dunia Njia’ sasa ni zamu ya Bukoba.

“Nikiwa na baadhi ya wasanii wengine wa Bongo Flava, kama Ngwea, Blue, Maunda Zorro na wengine kibao tutapiga shoo ya kwanza ndani ya ukumbi wa Linas Club, siku itakayofuata tutajitupa ndani ya Uwanja wa Kaitaba na kuendelea na uzinduzi huo,” alisema Bushoke.

Aidha, mchizi aliweka wazi kwamba, viingilio kunako shoo hiyo vitakuwa ni shilingi elfu kumi (VIP) na elfu tano kawaida, huku uwanjani ikiwa ni shilingi elfu moja kwa kila mtu.
******* **************
Miss EA 2008 kuanzia A-Town
Shindano la kumtafuta mrembo wa Afrika Mashariki (Miss East Africa) ambalo mwaka jana lilimalizika kwa binti kutoka Burundi, Claudia Noyimana kuibuka na ushindi, mwaka huu linaanzia pande za Arusha ambapo litawakutanisha zaidi ya warembo 20.

Akipiga stori na ShowBiz, mratibu wa mpambano huo, Nicodemus Ngogo wa Kampuni ya Tanzania Full Moon Entertainment alisema kwamba tayari zoezi la kuchukua fomu kwa washiriki limeshaanza, linaendelea hadi Aprili 15, mwaka huu kisha warembo ishirini na tano watakaopatikana wataingia kambini kabla ya kukutana kunako jukwaa moja kwa ajili ya kumpata mshindi kutoka pande hizo za Kaskazini.

“Fomu zinaendelea kutolewa katika sehemu mbalimbali Arusha na Dar es Salaam, baada ya hapo warembo wataingia kambini kwa muda wa wiki mbili kabla ya kupambana jukwani ambapo mshindi ataondoka na gari jipya aina ya Toyo Nadia, huku mshindi wa pili na wa tatu wakijipatia pesa taslim ambazo tutazitaja hivi karibuni,” alisema Ngogo. Naye Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Omari Mawamba alisema kila kitu kuhusu shindano hilo kinaendelea vizuri.
**************************************************

No comments: