Monday, January 11, 2010

Soggy: Namzidi Joti urefu!


Rapa who deserves to be called galacha in Bongoland, Anselm Ngaiza ‘Soggy Doggy Anter’, ametoa kali kwa kutoa mistari ambayo anajinadi kuwa yeye ni mrefu kuliko staa wa Orijino Komedi, Lucas Mhuvile ‘Joti’.

Soggy alitoa mistari hiyo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya Sugu a.k.a Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ inayokwenda kwa jina la Veto.

Akiwa juu ya jukwaa la bei mbaya ambalo liliandaliwa rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa Veto, Soggy alijimwaga kwa mtindo huru a.k.a free style ambapo alimimina mistari ambayo ilishangiliwa vilivyo.

“Nakubali unaposema mimi ni mfupi, lakini mimi ni mrefu kuliko Joti,” ndivyo alivyorap Soggy na kuibua shangwe ya kiwango.
********************

No comments: