Friday, April 23, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!


A.Y, Marlaw Na tuzo za kimyakimya
Artists wawili wa Muziki wa Kizazi Kipya wenye heshima tele Bongo, Ambwene Yesaya, A.Y na Lawrence Malima Madole a.k.a Marlow, wamekomba tuzo za TEENEZ zilizotolewa pande za Nairobi, Kenya. Aprili 17, mwaka huu.

Story iliyotua kunako meza ya ShowBiz imeweka kweupe kwamba, ishu hiyo ambayo kwa hapa Bongo imekuwa kama ‘sapraizi’ kwakutokuwa na promo ya kutosha ilichukua nafasi pande hizo weekend iliyopita ambapo A.Y aliibuka na ‘awadi’ ya Msanii Bora wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Marlaw aliondoka na tuzo ya the most downloaded song kupitia ngoma yake ya Pipi. “Kwangu mimi ni heshima inayoendelea kuwepo, inanipa moyo ili niongeze bidii katika kuandika ngoma kali,” alisema A.Y
***********************************************
G5CLICK.COM kuboresha maisha ya wasanii
Kile kilio cha muda mrefu cha wasanii kulalamikia kulizwa na mdosi katika usambazaji wa kazi zao kinaelekea kutatuliwa, na watatuzi si wengine bali ni vijana wadogo ambao ndiyo wakurugenzi wa site ya wajanja ya G5 Click.

Blogu hiyo ambayo ni namba moja nchini kuanzia layout, ripoti za muziki wa kiwanja na ndani ya nchi, wametangaza kuwa hivi sasa wanajipanga ili waweze kusambaza kazi za wasanii online.

Madogo wanaounda G5 ni Mustapha Suleiman, Ombeni Phiri, Desy Ernest na Nelson Kisanga ambao kupitia ubunifu wao, wameweza kuitengeneza G5click.com ambayo inavuma anga za kimataifa kiasi cha wengine kuifananisha na Facebook. Usipime!
Akigonga matamshi kwa niaba ya wenzake, Mustapha alisema:

“Tunajipanga kwa ajili ya kutambulisha njia mpya ya kutangaza, kusambaza na kuuza kazi za wasanii ili waondokane na kilio plus lawama kwa mdosi.”

Mbali na hilo, mzozo wa XXL Teen extra Awards unaendelea na G5 Click inawania tuzo ya Music Website of the Year ambayo ni category iliyopewa herufi D.
Katika category hiyo, vichwa kadhaa vimesimamishwa, DJ Choka (D2), Bongo5 (D3), DJ Fetty (D4), Babkubwa (D5) na G5 Click (D1).

Jinsi ya kupiga kura kwenye category hiyo, unaandika SMS yenye neno TN unaacha nafasi ikifuatiwa na namba yake ya utambulisho (code) halafu unatuma kwenda 15551.

Unaikubali G5? Gonga SMS yenye maandishi, TN D1 halafu unaitupa kwenda namba 15551. Pia unaweza kutembelea Nipe5.com ili uweze kupiga kura kwa internet.
****************************************
J Martins
Kutoka pande za Nigeria mchizi aliyepata kupiga mzigo na vijana wa P-Square kama prodyuza, mtaalamu wa sauti na mwandishi wa mashairi, J. Martins katikati ya wiki hii alidondoka Bongo na kusimama stejini kwa saa moja akisababisha shangwe ndani ya ukumbi uliyopo makao makuu ya Kampuni ya simu za mkononi ya Zain, pale Moroco, Dar es Salaam.

ShowBiz ambayo ilikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye ishu hiyo maalum ilipata kushuhudia J. Martins akionesha uwezo wa kutosha kupitia ajira yake hiyo ya muziki kwakuwa aliwafanya wageni waalikwa na wafanyakazi wengi wa Zain kusimama na kumpa sapoti kwa kuiweka mikono yao juu.

IKiwa ndani ya ukumbi huo, safu hii ilizunguka huku na kule na kufanikiwa kukutana na msanii Ambwene Yesaya ‘A.Y’ na kumgonga maswali mawili matatu kuhusiano na shoo ya mchizi ambayo kwa upande mwingine ilionesha kuwafunika wana Bongo Flava. Swali lilidondoka kwa Ambwene lilikuwa ni “Kwanini wasanii wa Bongo tunaonekana kupotezwa na Wanigeria hasa stejini?

“Unajua wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya Bongo wanashindwa kuandika nyimbo za kucheza na mashabiki ambazo zitazingua katika klabu mbalimbali za usiku, zaidi tumejikitia zaidi kwenye nyimbo za kusikiliza redioni tu kitu ambacho kinatufanya tushindwe kufanya vizuri hasa jukwaani,” alisema Ambwene.

Baada ya shoo hiyo J. Martins ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yenye jina la ‘Iva’ anatarajia kupiga tour katika mikoa kadhaa nchini kabla ya kurejea Dar kwa ishu moja kisha atasepa kurudi kwao, Ingweeeeeee!!.
*****************************************
Kalama
Kikosi Mtakubali kushindwa?
Siku chache baada ya Kiongozi wa Familia ya Kikosi cha Mizinga, Kalama Masoud a.k.a Kalapina kutangaza fainali ya Mkali wa steji itakayowashirikisha mastaa kadhaa wa muziki wa Hip Hop Bongo wakiwemo wao, baadhi ya wadau wa burudani wamekuwa na wasiwasi juu ya hilo.

“Napata wasiwasi, kama Kikosi ndiyo waandaaji wa ishu hiyo wakishindwa watakubali kwa ubabe waliokuwa nao?” Alihoji mdau mmoja wa burudani ambaye hakutaka kuandikwa hapa.

Ili kuweka sawa kila kitu, ShowBiz ilimuendea hewani Kalapina ambaye alikanusha ishu hiyo kwa kusema kuwa kila kitu kuhusu mpambano huo utakaochukua nafasi pande za ufukwe wa Coco Beach Dar, Aprili 30, mwaka huu kitasimamiwa na majaji wa ukweli na mshindi atapatikana kihalali na kukabidhiwa zawadi zake.

“Lengo kubwa ni kuendeleza harakati za muziki wetu kwa kujitoa kuandaa ishu sisi wenyewe badala ya kusubiri watu waje watufanyie. Mbali na sisi, wasanii wengine watakaopanda stejini siku hiyo ni pamoja na TMK Wanaume Halisi, Imam Abasi, Rado,Mansul, LWP na wengine kibao.
*******************************************
NATURE: Tuliowamwaga ni wavivu
King wa Miondoko ya Kwaito Bongo, Juma Kassim Kiroboto a.k.a Nature ambaye juzikati aliwapa shiti washkaji zake waliokuwa wakiunda Crew ya Wanaume TMK Halisi, amewadisi jamaa hao aliowaacha yatima baada ya kula mkataba na Kampuni ya DLC ya nchini China.

Nature aliwachana jamaa hao alipokuwa akigonga interview na stesheni moja ya redio jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mtu mzima alieleza chanzo cha kuwatosha kwenye shavu hilo.

“Tumewaacha kwa sababu ni wavivu wa kuandika na pia tulijua mwishoni watajiondoa wenyewe kundini. TMK Halisi hii mpya ni kazi kwa kwenda mbele, hatutaki tena watuma meseji,” alisema Nature bila kufafanua ni meseji za aina gani.

Wasanii wanaoendelea kuwakilisha TMK Halisi na Nature ni pamoja na Dolo, Baba Levo, JB wa Mabaga Fresh na KG Son. Waliotoswa ni Luteni Kalama, Mzimu, Malipo, D Chief, Bob Q, BK na Richie One ambaye alikuwa ni mshkaji wa karibu wa Nature.

Compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments: