Friday, May 7, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Kilimanjaro Music Awards
imebaki siku moja tu!
Kura yako ni muhimu but imebaki siku moja tu kukamilisha mpango mzima wa kupiga kura. Yap, Mei 8, 2010 (kesho) ndiyo itakuwa mwisho na baada ya hapo, wadau watangoja matokeo ambayo yatawekwa plain ifikapo Mei 14, 2010.

Sean Kingston atakuwa ndani ya nyumba ya Diamond Jubilee siku hiyo na kushiriki kutoa tuzo kwa wasanii waliofanya vizuri Bongo kwa mwaka 2009, halafu siku inayofuata (Mei 15), atagonga bonge la shoo pamoja na washindi wa Kili 2009.
Changamka changamka basi kuwahisha kura yako. Hapa chini kuna baadhi ya categories na utaratibu wa kupiga kura.

Wimbo Bora wa R&B (G)
Belle 9 - Masogange 11
Diamond - Kamwambie 22
AT ft Stara Thomas - Nipigie 07
Maunda Zorro - Mapenzi ya Wawili 52
Steve - Sogea Karibu 72

Wimbo Bora wa Hip Hop (J)
Johmakini - Stimu Zimelipiwa 34 Quick Racka - Bullet 67
Chid Benz - Po Pom Pisha 15
Ngwea - CNN 46
Fid Q - Im a Professional 26

Wimbo Bora wa Afrika Mashariki (Q)
Blue 3 ft Radio & Weasel (Goodlife) - Where you are 12
Kidumu ft Juliana - Haturudi Nyuma 38
Cindy - Na wewe 18
Radio and Weasal (Goodlife) - Bread and Butter 68
Kidumu - Umenikosea 37
Kupiga kura, unatuma SMS ukianza na neno KILI unaacha nafasi halafu unaambatanisha na herufi ya kipengele (category) kisha namba ya msanii baada ya hapo unatuma kwenda namba 15723.
Mfano, kuchagua Sogea Karibu wa Steve kuwa Wimbo Bora wa R&B. Unaandika KILI G72 kisha unatuma SMS yako kwenda namba
15723.
*********************************************
Mvua yawatibulia Kikosi
Shoo ya mkali wa steji ambayo ipo organized by Kikosi cha Mizinga, ilitibuliwa na mvua, so that haikufanyika, kwahiyo wana wanajipanga ili kulitenda libeneke kama ilivyokusudiwa.

President wa Kikosi, Karama Masoud ‘Kalapina’ alisema: “Ngoma tumeahirisha mpaka Mei 9 (Jpili inayokuja), eneo la tukio ni lile lile, Coco Beach na watu waje ili kumjua nani mkali wa kumiliki jukwaa.”
*********************************


Exclusive SMS kutoka kwa...
AFANDE SELE

Mfalme wa Rhymes, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, wiki iliyopita ‘aliisapraiz’ Showbiz ya Ijumaa baada ya kuidondoshea SMS kali kuhusu Bongo Fleva. Unaweza kuisoma hapo chini;

“Hivi sasa kila mtu anajidai anaijua Bongo Fleva kuliko hata wajuzi na wazoefu wa game hili, Bongo Flava inakua upande wa uimbaji lakini marapa wapya hakuna anayeishika jamii. Wengi wana mashairi dhaifu sana na idea ni za kitoto.

“Wengi wanabebwa na ma-Dj wenye maslahi nao. Kuna Ma-Dj wanawaumiza makusudi wakongwe hata kazi zao za ukweli wanazibana wakidhani wanaua wakongwe kumbe wanaliua game zima. Wanakata nguzo kuu ambazo ni mashairi na ujumbe bora toka kwa wakongwe ambao wanatambua haki zao.

“Walionyonywa ni wengi, wanaharakati wa ukweli! Sasa jamii inapaswa kuamka na kudai kile cha ukweli na si kuamini kila wanachokisema ma-Dj walioanza kazi juzi wakati game imetolewa mbali tena kwa machozi, jasho na damu.

“Watu wanapaswa kujua kwamba Watanzania ni walewale na si wajinga kama baadhi ya Ma-Dj na watangazaji wanavyofikiri kuwa kila wanachotaka wao basi Wabongo wataamini. Leo hii kuna artists wanapewa promo kila siku kwa kulazimisha lakini bado ukija huku mtaani watu bado hawawajui kwakuwa mchango wao katika game haufanani na sifa wanzopewa.

“Shabiki wa Afande, Prof. Jay, Daz Nundaz ndiyo huyo huyo atakayemkubali na artist mpya anayetoka vyema katika game, sasa kama kutoka kwa wasanii wapya dhaifu ndiyo kunasababisha kuwaua wakongwe wa ukweli, basi mashabiki hawatoendelea kuamini game na matokeo yake hadhi ya muziki inashuka.

“Katika jamii, kitendo cha watangazaji fulani na ma-Dj kutowapa nafasi waasisi, basi na jamii haitokubali au kumtambua msanii mchanga anayekuzwa kwa uongo na ufisadi unaofanywa na ma-Dj pamoja na mameneja uchwara wanaoshinda wakihonga na kuleta fitina ya wasanii na watangazaji, lakini ukweli unatashinda.”

Unasemaje kuhusu SMS hii ya Afande? Tuambie kupitia mcgeorge2008@gmail.com au tembelea www.ebwanadaah.blogspot.com
***************************************
R.O.M.A, AY, FA, Tip Top
& Mike T
Still wanakamua
Wanasema Bongo Fleva hailipi. Wanadai imepotea njia lakini guys wanaendelea kusimamisha topic ambazo zinawapa ushujaa kitaani ikiwemo kuendelea kuipa heshioma game hiyo.

R.O.M.A, A.Y, FA, Tip Top Connection na Mike Tee wote wameachia ngoma mpya recently ambazo zimesimama inavyotakiwa.

Roma amedondoka na kitu Pasta Watatu, Tip Top wapo na ngoma Bado Tunapanda, Mike Tee yeye anayo Tujiibe tukiweza wakati FA na A.Y wamesimama pamoja katika dude linalopatikana kwa jina la Usije Mjini.
****************************************************
Zay B
Sote tuhuzunike naye!
Super girl ambaye ali-claim to fame kwa ngoma yake Nipo Gado mwaka 2000, Zainab Thabit Lipangile ‘Zay B’ yupo kwenye msiba mzito, kwahiyo tunaweza kuhuzuka naye kwa kipindi hiki kigumu alichonacho.

Zay B, amefiwa na baba yake mzazi, Thabit Nassor Lipangile wiki iliyopita kabla ya mazishi kufanyika Iringa mjini Jumatatu ya wiki hii.

Hata hivyo, mpango mzima wa msiba huo ikiwemo matanga, unachukua nafasi Tabata, Kinyerezi, Dar es Salaam.

Enzi za uhai wake, Lipangile alikuwa bonge la mhandisi na ndiye aliyebuni njia ya kusafirisha maji kwa kutumia mianzi, badala ya mabomba ya chuma au plastiki, hivyo kuipunguzia serikali gharama.
***********************************************
Jitta, Dudu
warudi home Mwanza
The Bongo Hip Hop Legend, Godfrey Tumain ‘Dudubaya’ na Raga icon, Jittaman wameamua kurudi nyumbani kwao Mwanza ili kusindikiza shoo ya Miss Magu ambayo itachukua nafasi Mei 12,2010.

“Yap maze, hii ni nafasi ya dhahabu, kuitwa nyumbani kupiga shoo ni kitu kikubwa. Kwa kifupi nitasimama na Dudu, yaani mamba wawili, nyumbani Magu,” alisema Jitta.
**************************************************
compiled by mc george/ijumaa newspaper

1 comment:

Anonymous said...

rekebisha hiyo mada hapo juu, Zay B baba yake hajafa, ni uongo, yuko hai. nani amekuambia kuwa amekufa?