Bendi ya muziki wa dansi ya mashujaa muzika ya jijini Dar ves Salaam imewasimamisha wanamuziki wake watatu Mwindo Kissa(Grman Kissa), Mongabanza Monga wa Monga(zidane), Simon Ngosha (Ngosha Mwanamasanja), kutokana na utovu wa nidhamu .
Akizungumzia adhabu hiyo msemaji wa bendi hiyo Shaaban Mpalule alisema kuwa imetokana na kutoheshimu maamuzi ya Uongozi, ikiwa ni pamoja na kutoa Lugha chafu kwa uongozi na Mmiliki wa Bendi.
Aidha sakata hilo lilitokea wakati Bendi hiyo ilipofanya onyesho katika ukumbi wa Woodland kwa Jimmy Lumo Kiwalani siku ya Ijumaa ambapo inasemekana walitenda hivyo kutokana na kulewa pombe iliyowazidi uwezo wao.
Mpalule alisema kuwa wanamuziki hao wamesimamishwa kwa kipindi kiisichojulikana hadi Uongozi wa Kampuni hiyo utakapobaini kwamba wanamuziki hao wamebadili Tabia ikiwa ni pamoja na kuomba Radhi kwa Maandishi.
No comments:
Post a Comment