Monday, May 10, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Madee Ubongo wake ni tofauti tangu Kifo cha Pendo
Rais wa Manzese na super character wa Tip Top Connection, Hamad Ali ‘Madee’, hayupo sawa tangu aliyekuwa intimate wake, Pendo, kufariki dunia.

Madee aliiambia Abby Cool & MC George over the weekend kuwa tangu Pendo afariki dunia kwa ajili ya gari, hivi sasa ubongo wake umebadilika.

Alisema: “Tangu afariki Pendo naogopa sana mabasi, siyaamini kabisa.” Hata hivyo, wakati anazoza nasi, Madee alikuwa safarini kwenda Kahama, Shinyanga kwa ajili ya shoo iliyochukua nafasi wikiendi iliyopita. Alisema: “Napanda basi kwa sababu sina jinsi, kitu ambacho huwa nafanya ni kulazimisha tiketi ya upande wa dereva, pia napanda na vidonge vya usingizi. Huwa nameza na kulala mpaka mwisho wa safari. Najihami tu ila Izraeli hakwepeki.”
************************************
Kylie Minogue
Ni mzuka mpya katika siku, dakika na wiki nyingine but still 2010. Ebwana Dah! Concept ni mapenzi katika angle ya staa gani katoka na yupi kwa staili gani! Mwanamuziki Kylie Minogue yupo ndani ya aquarium of discussion.

Site ya kiwanja ambayo ipo busy katika kufunua nyendo za mastaa, inamuanika Jason Donovan kuwa wa kwanza kudondoka in bed na Kylie kuanzia mwaka 1984 lakini ilipofika 1989 kila mmoja akashika 50 zake.

Michael Hutchence akaunga kuanzia 1989 – 91, akaja mwanamuziki Lenny Kravitz 1991, alipoachia mchuma, akashika Nick Cave kati ya 1996 – 97, akafuata James Gooding 1999 – 02 halafu akamegana kisela na Jay Kay 2003. Olivier Martinez alijiweka 2003 – 07 na kuanzia 2008 mpaka sasa Kylie yupo mshazari na Andres Segura. Jina lake kamili ni Kylie Ann Minogue, alizaliwa Mei 28, 1968, Melbourne, Victoria, Australia. Umri wake ni miaka 41.
*******************************************************
H. Baba Akumbuka alipotoka!
Dogo aliyetohoa TAKEU somewhere na kuitawala, Hamis Ramadhan Baba ‘H’, anaonesha uungwana wake, anakumbuka alipotoka na hilo analithibitisha ndani ya filamu yake inayokwenda kwa jina la Promota. H. Baba, alisema nasi wiki iliyopita kuwa ndani ya filamu hiyo anajaribu kuonesha njia mbalimbali ambazo alipita katika safari yake ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio ya muziki.

Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, imekumbukwa ndani ya filamu hiyo ambapo kuna kipande ambacho H. Baba amekirekodi kwenye ofisi zake. “Global ni mlezi wangu, nilipotoka Mwanza, ilinipokea na kunipa sapoti ya nguvu mpaka nikafanikiwa kimuziki, siwezi kuisahau na ndiyo maana sehemu ya filamu yangu nikairekodi kwenye ofisi za Global,” alisema.
*******************************


Sugu: Veto inatambaa kimya kimya!
Albamu ya mwana Hip Hop mwenye ‘aka’ nyingi kwenye game, Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ haitajwi sana lakini kasi yake kitaani ni kubwa kutokana na jinsi ambavyo wadau wanavyoinunua.

Mr. II a.k.a Sugu, alichonga nasi wiki iliyopita kuwa Veto ipo sawa, wadau wanajua kazi zake ndiyo maana wanainunua bila hata kupigiwa kelele nyingi kitaani. “Yeah man, Veto ni ujumbe wa taifa, kilio cha wasanii na harakati za vijana na Watanzania kwa jumla. Ni albamu ambayo imewakilisha mengi,” alisema Sugu na kuongeza: “Kama kawaida babu, Veto inauzwa na wamachinga, tunafanya hivyo ili kujitahidi kudhibiti wezi.”
******************************
Dudu
Vita ya Afande, Dudu mwisho wake nini?
Kwa wadau wafuatiliaji, watakuwa wanaunyaka ukweli kwamba big names on Bongo Hip Hop industry, Godfrey Tumain ‘Dudubaya’ na Suleiman Msindi ‘Afande Sele’ wapo kwenye vita ya maneno na wale ambao wanadai ni wanyonyaji.

Guys hao wanawagonga fatuma some DJ’s ambao wanadai ni wanyonyaji wasio na aibu, kwamba miaka nenda rudi, zao ni kuishi kimjini mjini kupitia migongo ya wanamuziki ambao wanahenyeka kutoka kimaisha bila mafanikio.

Dudu, ameachia CD ambayo ndani yake anawasaga ile mbaya wote ambao wanaishi kwa kudandia jasho la wasanii, DJ’s ambao wanadaiwa kuweka utaratibu no money no your song on air. Kwa upande wa Sele, yeye analaani kitendo cha DJ’s na some presenters kuwawekea kauzibe wasanii wenye misimamo, kuwabania nyimbo zao na kuwapa chati underground ambao hawauziki, hawana vipaji na hawalipi. Kwa kifupi ni kwamba Sele na Dudu wana hoja moja, ila uwasilishaji ni tofauti.

Ngumi Jiwe yeye ameamua kuingia studio na kuingiza vocal kwa lengo la kuwapaka anaowadisi, wakati Mzungu wa Roho yeye anafunua mambo kwa SMS.

Tunajenga hoja kwa staili hii; Bila shaka Sele na Dudu wana hoja za msingi lakini pengine haziwezi kuwa na maana yoyote ikiwa kilio chao kitabaki kujadiliwa kama pointi za kujadili vijiweni. Ni muda wa mabadiliko, wasanii ni lazima wawe pamoja ikiwa wanataka kufanikisha harakati zao.

Kinachosemwa na Sele au Dudu ndiyo kile ambacho kipo kwa wengi lakini wapo kimya kwa sababu ya kusumbuliwa na nidhamu ya woga. Ni vizuri kushirikiana ili kupata mafanikio ambayo kila msanii anayakata. Unyonyaji ni mwingi. Kukataa dhuluma ni hatua namba moja ya kuelekea kwenye malisho mema. Hatahivyo, kumbuka; Akili za kuambiwa changanya na zako!
****************************
ompiled by mc george/ijumaa wikienda

No comments: