Monday, June 28, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ

Tip Top vs Watoto wa THT
Julai 4, 2010 ndani ya Uwanja wa Samora Iringa, atajulikana nani bora kati ya crew ya Tip Top Connection na wana wa Tanzania House of Talent (THT), Barnabas na Lina.
Katika kufanya mambo yaende sawa kwenye shoo hiyo ilyopewa jina la Bado tunapanda, staa wa Hip Hop, Jeezy Mabovu naye atakuwepo ili kufanya mpangop mzima uwe timilifu.

Prezidaa wa Manzese aliyepia Msanii Kiongozi wa Tip Top, Hamad Ally ‘Madee’ alisema nasi kwamba ni shoo ya kawaida lakini wana wa Iringa wataweza kujionea nani mkali wa kupoteza kati ya crew yao, THT na Mabovu.

Kwa sasa, Tip Top wanatawala anga kwa ngoma yao Bado Tunapanda, Barnaba na Lina wanasumbua na kibao SMS, wakati Mabovu anafunika na Mimi.
*******************************
Mkoloni : Agusa topic ya Uchaguzi Mkuu
Mtambo wa Mashairi aliyeng’ara na Kundi la Wagosi wa Kaya, Fred Maliki ‘Mkoloni’ amegonga topic ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, kwa kutoa kionjo cha wimbo wake mpya ambao unaelezea umuhimu wa viongozi bora.

Mkoloni a.k.a Kinega, aligonga ‘akapera’ ya verse moja Ijumaa iliyopita, Makao Makuu ya CHADEMA, mara baada ya kukabidhiwa kadi na katiba ya chama hicho ambacho alijiunga nacho rasmi.

Katika ngoma hiyo, Mkoloni aliwafyatua baadhi ya viongozi ambao wanaendele kutumbua badala ya kuwasaidia wananchi wao.

Mkoloni alikabidhiwa kadi ya CHADEMA pamoja na mastaa wenzake wa Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Gerald Mwanjoka ‘G Solo’.
**********************************
Nicki Minaj: Mjue kidume pekee aliyefaidi penzi lake
Linapozungumzwa suala la mapenzi, kila mtu huchukua utulivu wake. Yap, yanamgusa kila mtu na ndiyo maana ya kuwepo kwa Ebwana Dah! Inaendelea kuchanja mbuga kwa staili ile ile ya kuwamulika mastaa na kucheki idadi ya watu waliowazawadia penzi.

Ni zamu ya Rapa wa kike pande za Obama a.k.a US, Nicki Minanj na kupitia hapa utaweza kujionea kwamba tofauti na mastaa wengine, yeye ametoka na njemba mmoja tu.

Kwa mujibu wa ‘site’ ya kiwanja ambayo ime-specialize majukumu yake katika kufuatilia ‘ishuz’ zinazohusu mapenzi ya mastaa, Aubrey Graham a.k.a Drake ndiye kidume pekee ambaye amethibitika kuonja penzi la Nicki.

Mdada huyo na Graham, walianza ku-date mwaka 2009 na kujenga kibanda hadi leo.
Nicki Minaj ni jina ambalo amelikarabati, lake halisi ni Onika Maraj. Alizaliwa Desemba 8, 1984, Southside, Jamaica Queens, New York, Marekani. Umri wake wa miaka 25, dini yake ni Mkristo, pia alihitimu LaGuardia High School.
****************************************
Sugu: kusimama na CHADEMA Mbeya Mjini
Scoop zenye uzani mkubwa zinaendelea kupatikana Global Publishers (GPL), Abby Cool & MC George over the weekend inayosababishwa na Ijumaa Wikienda, inakuwa ya kwanza kukujuza ‘Mtizedi’ kuwa the Bongo Hip Hop Hero, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ atasimama kugombea ubunge Jimbo la Mbeya Mjini.

Sugu, anasimama Mbeya Mjini kutii wito wa CHADEMA ambacho kinaamini kwamba mwanaharakati huyo ni ngao ya chama hicho kulitwaa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

ShowBiz ya Gazeti la Ijumaa ambalo nalo linafyatuliwa na GPL, Ijumaa iliyopita, ilikuwa ya kwanza kuandika kuhusu Sugu kujiunga CHADEMA ambacho kimemuandalia mambo makubwa kwenye jimbo ‘flani’ na siku hiyo hiyo staa huyo akakabidhiwa kadi ya uanachama.

Kaka mkubwa haingii msituni peke yake na kilichotokea ni kuwa wana Hip Hop wengine, Super Character wa Wagosi wa Kaya, Fred Maliki ‘Mkoloni’ na Gerald Mwanjoka ‘G Solo’ nao kila mmoja alichukua kadi ya uanachama ya CHADEMA, lengo likiwa kumpa sapoti ya nguvu Sugu.

ABC zenye umakini kutoka CHADEMA zinaweka wazi kuwa chama hicho kimeamua kumsimamisha Sugu Mbeya Mjini, baada ya kutembelea jimbo hilo na kufanya utafiti ambao ulionesha kwamba galacha huyo mwenye rekodi ya kupigania haki bila woga, anakubalika kwa wapigakura ile mbaya.

Nyeti zinadondoka kuwa CHADEMA kiliamua kushuka na kukaa meza moja na Sugu baada ya utafiti huo ambao ulifanywa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa chama hicho, John Mnyika.

“CHADEMA tuna malengo mazuri na tunataka kufanya vizuri kwenye uchaguzi ujao. Hatusimamishi ilimradi mgombea, tunaweka mtu ambaye anakubalika kwa wapiga kura. Tunafanya utafiti kwanza kuona wananchi wanamtaka nani.

“Mbeya Mjini wananchi walimzungumzia Mr. II (Sugu) na kwa sababu hatutaki kulipoteza jimbo hilo, tukaamua kuzungumza na Sugu nakukubaliana mambo ya kimsingi kabisa,” alisema ‘insaida’ wetu ndani ya CHADEMA.

Sugu alipozungumza na safu hii, kwanza alicheeeeeka! Kisha akaendelea: “Kila kitu kitakuwa wazi baada ya muda mfupi, hivi sasa mimi nasherehekea kujiunga CHADEMA, nakipenda na malengo yangu ni kukifanya kuwa chama cha wajanja.

“Itafikia wakati mtu anaona kujiunga na CHADEMA ndiyo ujanja. Tutajenga nchi. “
Kwa mujibu wa ‘insaida’ wetu, jana Sugu alitarajiwa kutangaza nia ya kugombea Jimbo la Mbeya Mjini na kuchukua fomu kabla ya ziara yenye afya ya kurudisha fomu Mbeya ambayo itakuwa na msafara wa vingozi wa chama wenye nguvu.
**********************************

compiled by mc george/gpl

No comments: