Monday, July 26, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Mzee Yusuf Uzinduzi wa My Valentine, PTA hapatoshi!
Zimesalia siku 4 kabla ya kuifika ile siku ya uzinduzi wa albamu mpya ya Kundi la Jahazi Modern Taarab inayokwenda kwa jina la My Valentine huku kiongozi wa kundi hilo Mzee Yusuf akieleza kuwa, ataitumia siku hiyo pia kumtambulisha rasmi dada yake, Khadija Yusuf aliyerejea kundini.

Akipiga stori na safu hizi Mzee Yusuf ‘Mfalme’ alisema kuwa, kila kitu kuhusu uzinduzi wa albamu hiyo yenye nyimbo sita kinakwenda sawia na kwamba, kinachusubiriwa ni siku hiyo ifike ile waweze kuwapa mashabiki wao ile kitu roho yao inapenda.

Iliweka wazi kuwa, mpango mzima utafanyika Julai 30, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa PTA uliopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kwa kiingilio cha shilingi 10,000 tu.
***********************************************

Moracka: Mimi na Diva ni over forever
The Group Leader wa kundi lililopotea katika mazingira ya kutatanisha la The Rackers, Mohamed Hassan ‘Moracka’ anafunua kile kilichokuwa kinanong’onwa kwa muda mrefu kuhusu penzi lake kwa malkia wa Ala za Roho, Loveness Malinzi ‘Diva’.
Katika straight interview na Abby Cool & MC George over the weekend Alhamisi iliyopita, Moracka alisema kuwa Diva alikuwa mshkaji wake lakini kwa sasa its over forever.

“Alikuwa mshkaji wangu kama ambavyo mtu mwingine anaweza kuwa, hatukuwa kimapenzi ila baada ya kutofautiana kila mtu yupo kivyake. Ila sina bifu naye, endapo atahitaji kufanya kazi na mimi sitombania,” alisema Moracka.

Wakati Moracka akiongea hayo, jamii ya wapenda burudani inalo jibu kuwa msanii huyo alikuwa kimapenzi na Diva na walitofautiana pale kiongozi huyo wa The Rackers alipojirusha na mrembo anayetambaa kwa jina la Irene.

Mbali na Diva’s issue, Moracka alisema: “Life yangu haitegemei sana muziki kama ilivyo kwa wasanii wengine. Mimi ninazo biashara zangu ambazo zinaniwezesha kuendesha maisha A Town bila wasi. Nafanya vizuri kwenye game lakini siachi biashara.” Stori na Hemed Kisanda.
********************************

Mkoloni Agoma kuingia studio, kurekodi na Rich One
Super Character wa ile project yenye mzozo ya Anti Virus, Fred Maliki ‘Kinega Mkoloni’ amekataa kurekodi wimbo wowote usiokuwa na maudhui ya harakati za kuikomboa Bongo Fleva na kwa kusimamia hilo, amemtolea nje memba wa kundi jipya la Wanaume, Richard Shauri ‘Rich One’.

The Abby Cool & MC George insider, alisema nasi kuwa hivi karibuni Rich alimfuata Mkoloni na kuomba tafu ya kugonga wimbo pamoja, lakini memba huyo aliyelisimamisha Kundi la Wagosi wa Kaya, alikataa kwa sababu si wakati muafaka.

“Unajua Mkoloni yupo busy sana na harakati. Anaendelea kusimamisha ukweli wa kile alichokifanya kwenye Antivirus, kwahiyo alimkatalia Rich One si kwa nia mbaya, bali kirafiki kwa sababu matunda ya anachokipigania yatavunwa na wasanii wote pamoja na Watanzania kwa jumla,” alisema.

Mkoloni alipozungumza nasi alikiri hilo na kuongeza: “Haikuwa na maana ya bifu, Rich One ni mwenzetu, lakini akili yangu kwa sasa nimeielekeza kwenye harakati.”
******************************
G -Solo: Aianika Bongo Fleva kitabuni
The Front Liner wa harakati za muziki wa kipya, Gerald Mwanjoka ‘G Solo’ameamua kuufafanua muziki wa Hip Hop na tafsiri ya Bongo Fleva katika kitabu ambacho amekiandaa kinachoitwa Harakati za Bongo Fleva na Mapinduzi.

G Solo ambaye ni mwana Hip Hop wa siku nyingi na chanzo cha mafanikio ya Kundi la Unique Sisters ‘Dadaz’, katika kitabu hicho, anaeleza historia ya Hip Hop Tanzania na mwanzo wake nchini Marekani, ukuaji wake na Bongo Fleva.

Kitabu hicho chenye kurasa 150, kinaeleza kinagaubaga tatizo la biashara ya muziki Tanzania, unyonyaji na hali duni ambayo wanakutana nayo wanamuziki wengi wa kizazi kipya kutokana na kutovuna wanachostahili kupitia kazi zao.

G Solo aliiambia Abby Cool & MC George over the weekend Jumamosi iliyopita kuwa ameamua kuandika kitabu hicho ili kutoa uelewa wa kile kinachoendelea kuhusu Bongo Fleva kwa kizazi cha sasa na kijacho, pamoja na kuchochea mapinduzi.

“Kitabu kinakwenda vizuri, kilipitiwa na watu wangu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, kilichobaki ni wahariri marafiki nao watie mkono wao halafu kichapwe ili Watanzania wakisome,” alisema G Solo.
**************************
Monica Arnold: Agawa penzi kwa wanaume watano
Anapotoka mmoja hakosi mwingine wa kuingia. Ni bandika bandua, Ebwana Dah! Utaratibu ni ule ule, yanazingatiwa maoni ya wadau wa safu hii halafu staa anayepita ndiyo anakuwa topic.
Aliyepo leo ni staa wa R&B pande za US, Monica Arnold na inafunuliwa idadi ya wanaume ambao kwa nyakati tofauti, aliweza kutoka nao kimapenzi.

Kwa mujibu wa site ya kiwanja ambayo ipo serious katika kufuatilia uhusiano wa mastaa hasa wa kwa himaya ya Obama, Usher Raymond ndiye anatajwa kuwa mwanaume wa kwanza wa Monica na inaelezwa kuwa walitoka mwaka 1995.

Jarvis Weems anatajwa kuwa wa pili na alichangamka naye kuanzia mwaka 1998 hadi 2003 lakini Monica akiwa kwenye uhusiano huo, mwaka 2000 alimegeka kisela kwa C-Murder.

Young Buck alifaidi penzi la Monica mwaka 2004 na mwaka 2005 akajituliza kwa Rodney Hill.
Jina lake kamili ni Monica Denise Arnold, alizaliwa Oktoba 24, 1980 College Park, Georgia, Marekani. Umri wake ni miaka 29 na ni mhitimu wa High North Clayton High School, Atlanta, Georgia.
****************************************************

2010 ni wasanii na siasa
Uchaguzi Mkuu 2010 unaweka hadharani majina ya watu ambao haikufikiriwa kama wangeweza kuitumikia siasa. Tunaona wasanii mbalimbali nchini, tayari wamekwishaweka silaha begani nao wanawania nafasi za kuingia bungeni na halmashauri.

Mpaka sasa, orodha na maeneo wanayogombea ni hii;

Sugu
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, huyu anatajwa kuwa ni lulu ya mkoa wa Mbeya. Alishawishiwa na CHADEMA baada ya wananchi kumtaja mara kwa mara, wakati walipokuwa wanafanya utafiti wa mgomba ubunge Jimbo la Mbeya Mjini.
Sugu tayari alikwishachukua fomu na kuirejesha. Na atajwa kuwa ana nafasi kubwa ya kuliteka Jimbo la Mbeya Mjini kutokana na jinsi anavyokubalika.

Nakaaya Sumari
Anagombea Viti Maalum Arusha kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kabla ya kujitosa kwenye siasa, aling’ara kwenye muziki na mitindo.

Kalapina
Mr. President wa Kikosi cha Mizinga, Karama Masoud ‘Kalapina’ anawania udiwani Kata ya Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF). Jamaa ni galacha wa Hip Hop na mwanamapinduzi wa muziki huo.

Sharks
Ni miongoni wa wasanii waliyopitia kwenye nyumba ya kukuza na kuendeleza vipaji, Tanzania House of Talent (THT) na kufanikiwa kufanya kazi zilizofanya vyema kwenye muziki wa kizazi kipya. Jina lake kamili ni Shaban Hussein Kichwabutu “Sharks’. Anawania udiwani Kata ya Sinza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mr. Simpo
Aliibuka na Kundi la Love Forever na kutikisa anga ya muziki wa kizazi kipya. Jina lake kamili ni Renatus Pamba ‘Mr. Simpo. Anawania udiwani wa Kata ya Sinza kwa tiketi ya CHADEMA.

Chikoka
Ni msanii wa filamu na jina lake kamili ni Juma Chikoka. Anawania ubunge Jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

compiled by mc george/ijumaa wikienda

No comments: