Friday, August 13, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

NATURE: Kwakweli nammiss Lil Kim
Mfalme wa Temeke, Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, juzi kati aliwadhihirishia wapenzi wake kuwa, ‘anammisi’ msanii kutoka Marekani, Kimberly Denese Jones ‘Lil Kim’ ikiwa ni siku chache tangu alipogonga naye bonge la shoo.

Nature aliyasema hayo katika party ya uzinduzi wa Clouds TV kujumuisha vipindi na muziki kutoa Kituo cha MTV Base iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Much More Bilicanas, Posta, Dar, usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii.

Awali msanii huyo mwenye vituko awapo stejini alikaribishwa kutoa burudani ambapo aliimba wimbo wa Mugambo na alipomaliza, alisema kuwa, amefanya shoo hiyo lakini kiukweli anamiss Lil Lik Kim.

“Nimefanya makamuzi lakini kiukweli hapa nammiss tu Lil Kim,” alisema Nature huku akikabidhi mic na kushuka jukwaani.

Mbali na Nature, wasanii wengine walioporomosha burudani katika shughuli hiyo ni Ali Kiba, Albert Mangwair pamoja na kundi zima la Aladji kutoka Ivory Coast.

Wadau wa burudani watakumbuka kuwa, mwishoni mwa wiki iliyopita, Nature pamoja na Lil walifanya shoo ya pamoja katika Tamasha la Fiesta Dar ambapo wakiwa stejini mwanadada huyo alionesha kumzimia mtoto huyo wa kiumeni, mazingira yaliwafanya washkaji kuanza kumuita Kim shemeji.
********************************************
MUSSA KAMBI:Nilichokiimba ni maisha yangu
STAA wa muziki wa kizazi kipya Mussa Seti a.k.a Mussa Kambi amesema mashairi aliyoimba kwenye ngoma yake inayotamba hivi sasa kwenye vituo vya redio na runinga ni hadithi ya kweli ambayo amekutana nayo kwenye ëhasoí zake za maisha

Akistorisha na safu hii juzi kati, nyota huyo aliyeibukia kwenye chuo cha ‘Zoom Computersí’ cha jijini Dar, ameweka wazi kuwa akiwa kwenye harakati za kutafuta mkwanja huko pande za Kahama Shinyanga, alikutana kisanga cha mshikaji mmoja kuwafyeka ndugu zake ili apate utajiri.

‘Ni stori ya kweli kabisa ambayo nilishuhudia kipindi niko Kahama Shinyanga niki-haso na muziki, kwa kuwa sisi wasanii tunaimba yale yanaoihusu jamii ndiyo nikapata idea ya kuandika songi hili,” alisema Kambi, na kuongeza kuwa, mpango mzima wa ngoma hiyo umekamilika ndani ya mjengo wa Zoom Produaction,
Magomeni chini ya mkali Enock Mwangoto ‘Iki’ .
********************************************
Nitaitoa simba dume baada ya uchaguzi
Bongo Flava King, Seleman Msindi ‘Afande Sele’, ameibuka na kusema kuwa, anatarajia kutoa wimbo mpya unaokwenda kwa Jina la ‘Simba dume’ baada ya uchaguzi mkuu 2010.

Afande Sele aliitonya safu hii kuwa, ameamua kutoa wimbo huo baada ya uchaguzi kutokana na wahusika wengi wa sanaa kuwa kwenye mishemishe za zoezi hilo.

‘Nimeamua kutoa wimbo huu baada ya uchaguzi kutokana na shughuli za kisiasa zinazoendelea kwani wahusika wengi wapo kwenye mchakato huo,’ alisema Afande Sele.

**********************************************
Diamond Musica yakamilisha mbili za moto
Bendi ‘High Quality’ kwa muziki wa dansi Bongo, Diamond Musica ‘Vijana Classic’, wamekamilisha ngoma zao mbili kali, tayari kwa kuzisukuma kitaani.

Akizungumza na Showbiz juzi, kiongozi wa kundi hilo, Mule Mule ‘FBI’ alizitaja nyimbo hizo kuwa ni ‘Supu ya kongoro’ utunzi wake Alan Mulumba Kashama na ‘Power Twenty Ten’ walioitunga kwa ushirikiano.

“Ngoma hizi ni mwanzo tu, kwani kuna nyingine kali zitafuata baadaye, hivyo wanaotaka kuzisikia nyimbo hizo na kuona staili zetu mpya wasikose kufika Meeda pande za Sinza-Mori, Dar, leo,” alisema FBI.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa, ukiacha Meeda eneo lingine watakapoziweka wazi ni Leaders Club kwenye bonanza la wasanii siku ya Jumamosi bila kusahau Jumapili ndani ya Ukumbi wa Golden Bridge.
*******************************************

Adam Mchomvu alinadi wigi la Lil Kim
Lile wigi ambalo msanii kutoka Marekani, Lil Kim alilitupa kwa watu waliohudhuria Tamasha la Fiesta Dar na kudakwa na mtangazaji wa Clouds Redio, Adam mchumvu sasa analinadi.

Akiongea hivi karibuni kupitia kipindi cha XXL, Mchomvu alisema kuwa, imekuwa ni bahati yake kulidaka yeye lakini naye analiingiza sokoni hivyo mwanadada mwenye pesa zake anaweza kulipata.

‘Wigi la Lil Kim liko sokoni una bei gani? Hivi utajisikiaje kuvaa kitu ambacho kimeshavaliwa na staa kama Lil Kim? Kama unalihitaji nitafute,” alisema Mchomvu.

*******************************************
Rich One: Atoboa siri kuondoka kwao TMK Halisi!
Nyota wa zamani wa Kundi la TMK Wanaume Halisi, Richard Shauri ‘Rich One’, ametoboa kilichowaondoka TMK Halisi kwamba ni matatizo ya uongozi wa juu.

Akistorisha face to face na safu hii hivi karibuni, alidai kuwa sababu kubwa iliyowandoa ni ungozi wa juu wa Kundi la TMK Wanaume Halisi kuwazuia kutumia jina hilo pindi kiongozi wa kundi hilo, Juma Nature ‘Sir Nature’ anapokuwa hayupo.

“Jambo lililotufanya tujitoe TMK Halisi na kwenda kuanzisha Wanaume ni kitendo cha kuzuiwa kutumia jina la kundi Nature anapokuwa hayupo na mambo mengine,” alisema Rich One.

Jamaa liongeza kwamba hakuna mtu aliyewafukuza isipokuwa kulikuwa na ‘mbinyo’ wa hali ya juu ndani ya kundi hilo huku baadhi ya wasanii wakipewa nafasi kubwa ya kufanya kazi na wengine kukosa nafasi hiyo hata kama uwezo wao ni mkubwa.

“Hakuna mtu aliyetufukuza bali tulichoshwa na ‘udikteta’ wa viongozi wetu kuzuia tusitumie Jina la ‘Wanaume Halisi’ bila ‘Nature’ kuwepo, hivyo tulijihisi kama hatuna thamani ndani ya kundi,” Rich aliweka wazi.

1 comment:

La Princessa said...

hahhaha hiii kali...dnt knw hw much it will go for!! love this blogspot...jis showing some love..dnt forget to drop by laprincessaworld.blogspot.com