Monday, August 16, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Lil Kim Hawa wote kadondoka nao kitandani!
Last week haikusomeka kwa sababu ya kuitendea haki shoo ya Fiesta lakini Blue Monday hii, Ebwana Dah! inakujia tena. Leo anaangazwa mtoto wa kike chakaramu ambaye Jumamosi ya Agosti 7, 2010 alisababisha mzozo alipofanya makamuzi ya kiwango cha juu kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar.

Mtajwa ni Kimberly Denise Jones ‘Lil’ Kim’ ambaye katika kulinogesha Tamasha la Fiesta 2010, alifanya ‘upacha’ jukwaani na Mfalme wa Temeke, Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’ na kutoa shoo ambayo imeacha simulizi kwa Watanzania.

Kinachohusu hapa ni nani kafaidi penzi la staa huyo. Kwa mujibu wa site ya kiwanja ambayo inadili na issues za uhusiano wa mastaa wa kiwanja, kidume Andre Benjamin ndiye anayetajwa kuwa wa kwanza kutoka na Lil’ Kim ingawa haitajwi ni mwaka gani.
Baba Beyonce, Sean Carter ‘Jay Z’ anatajwa wa pili, halafu anaungwa marehemu Christopher Wallace ‘Notorious BIG’, anakuja Damian Hardy na wote hao haielezwi ni lini walianza kumchangamkia Lil’ Kim wala kivipi waliachana.

Mwaka 1997, Lil’ Kim hakuona soo kuachia penzi kwa swahiba wa BIG, Sean Combs ‘P. Diddy’, baada ya hapo alimegana kisela na mdogo wake Brandy Norwood, Ray-J.
Mwaka 2003 alijitoa kwa Damian ‘World’ Hardy, kisha akaamua kwenda sawa kwenye penzi la kisagaji na mkali mwenzake wa Hip Hop, Missy Elliot, alipohisi anahitaji mwanaume na si mwanamke mwenzake, mwaka 2004, alitua mikononi mwa Scott Storch.

Mwaka 2007, alitua kwa Jamie Foxx na penzi lao linasomeka mpaka sasa, ingawa mwaka 2008, alisaliti ‘kiduchu’ na kwenda kuchangamsha damu na Tracy Morgan.
Lil’ Kim ana umri wa miaka 35. Alizaliwa Julai 11, 1975, New York, Marekani. Mbali na kurap, pia anaandika nyimbo na kuigiza. A.k.a yake nyingine ni Queen Bee.
**************************************
Jully Tax: Bongo Movie yaipiga mwereka Nigeria
Director wa filamu mwenye kichwa chenye ‘madini’ ya thamani kubwa, Mfaume Abdul Hassan ‘Jully Tax’ amesema kuwa hivi sasa soko la filamu Afrika linatekwa na Tanzania na nchi nyingi zinakubali ubora wa Bongo Movies kuliko zile za Nollywood, Nigeria.

Katika straight talk to Abby Cool & MC George over the weekend juzi (Jumamosi), Jully Tax ambaye ndiye aliyegundua vipaji vya mwanamuziki Hamis Ramadhan Baba ‘H-Baba’, alisema kuwa baada ya kufanya filamu nyingi nchini, alipata mualiko nchi mbalimbali na kujionea mapinduzi makubwa ya sanaa ya Tanzania.

“Nilikuwa Bukavu, DRC nikajionea maajabu. Kwanza nilikuwa sijui kama tunakubalika lakini nilipokelewa kama kiongozi wa nchi na kupewa heshima zote na ujumbe mkubwa ambao nilipewa ni kwamba Watanzania hatujiamini,” alisema Jully Tax na kuongeza:

“Wakati nafanyiwa mahojiano kwenye televisheni Bukavu, kuna watazamaji walinipiga simu na kuuliza ni kwanini wao wakitazama picha za kutisha za Tanzania wanazikubali kuliko za Wanigeria, lakini Tanzania mpaka leo wanasema wapo nyuma kwa Wanigeria?

Jully Tax aliye pia prodyuza wa filamu, ameendelea kuthibitisha kiwango chake katika kuandika, kutayarisha na kuongoza ‘muvi’ zenye sura ya mauzauza barani Afrika.

Mtayarishaji huyo, pia ndiye ‘injini’ ya filamu ya Chozi la Urithi, Mtemi, Radi Cobra, Saladini, Mama wa Kambo na Kuku Awikia Tumboni.
****************************************************
‘Promota’ ya H-Baba ipo tayari
STAA wa TAKEU, Hamis Ramadhan Baba ‘H-Baba’ amesema kuwa sasa yupo tayari kuidondosha mtaani muvi yake inayoitwa Promota, baada ya kukamilika kwa mpango mzima wa kuitengeneza. Muvi hiyo imetengenezwa ndani ya mjengo wa Movie Galaxy, Mwanza na kusimamiwa na Tollywood Movies yenye mkono wake nchi nzima.

Akistorisha ‘fesi tu fesi’ na Abby Cool & MC George over the weekend juzi, H-Baba aliweka wazi kuwa ana uhakika muvi hiyo iliyosheheni wakali kibao, itafanya mapinduzi makubwa ukizingatia muongozaji wake ni wa kiwango cha juu.

“Muongozaji ni Jully Tax (Mfaume Abdul Hassan) ambaye uwezo wake unakubalika. Kuna wasanii wakali kama Yusuf Mlelana wengineo, ni filamu ya kiwango cha juu. Nataka kuonesha kiwango changu kwenye usanii. Nimetisha kwenye muziki na sasa nataka kufanya kweli katika filamu,” alisema H-Baba na kuongeza:

“Nimefanya hii muvi kwa uhakika na najua mashabiki wangu wataipenda.”
Imeandikwa na Na Jelard Lucas

***************************************************

DIAMOND, TANZANITE ‘BHITA’ NI ‘BHITA’
Harufu ya bifu zito kati ya wasanii chipukizi wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Mwingereza Athuman Mwingereza ‘Tanzanite’ na Nassib Abdul ‘Diamond’ sasa imefika puani kufuatia kukutana ‘laivu’ kwa wawili hao.

Diamond anatamba kitaani na kibao chake cha ‘Mbagala’ huku Tanzanite akidaiwa ‘kuangalizia’ wimbo huo kwa sauti na ‘biti’ katika wimbo wake wa ‘Kafara’.

Katika kipindi cha ‘Saturday Night Live’ kilichorushwa angani na runinga ya Channel Ten (EATV) Ijumaa iliyomalizika, wasanii hao walikutana ‘laivu’ na kidogo ‘pasitoshe’ baada ya Diamond kuonesha wazi hasira zake dhidi ya Tanzanite. Mzuka ulipanda zaidi kufuatia ‘Prizenta’ wa kipindi hicho, Jimmy Kabwe kumuuliza Tanzanite ni kwanini alikopi wimbo huo kwa sauti na biti, ambapo alijibu alikuwa akijaribu lakini akashangaa kusikia wimbo huo unarushwa hewani na vituo vya redio Bongo.

Katika majibu yake, Diamond alisema msanii huyo ni mwongo ‘mkubwa’ na kwamba, tayari yeye ameshampeleka msanii huyo kwenye ‘mahakama’ ya COSOTA licha ya kwamba, hajui ni kwanini mpaka sasa chama hicho cha kusimamia kazi za wasanii hakijamchukulia hatua Tanzanite.
****************************************
Wagosi kuvunjika; Mkoloni atoa tamko
Kundi lenye heshima kubwa Bongo, Wagosi wa Kaya limetajwa kuvunjika baada ya mmoja wa wasanii wake, John Simba ‘Dk. John’ kueleza kuwa hakuna alichobakiza ndani ya kundi. Memba mwingine, Fred Maliki ‘Kinega Mkoloni’ ameamua kutoa tamko lake kupitia Abby Cool & MC George over the weekend.

Mkoloni ambaye ni main character wa project ya Antivirus, ali-speak loudly na kona hii wikiendi iliyopita kuwa Wagosi wa Kaya bado lipo mzigoni na tamko la John halina msingi unaoeleweka.

Mwanaharakati huyo wa CHADEMA alisema, Wagosi wa Kaya bado ni hazina kubwa ambayo inaendelea kuingiza ‘faranga’ kila baada ya kipindi fulani kutokana na kazi nzuri walizorekodi mwanzoni mwa miaka ya 2000.

“Mpaka kuna wakati tunaitwa kwa Mdosi kugonga kopi, kuna kazi zetu Ulaya tulizipeleka na fungu huwa linakuja, kwahiyo siwezi kukubali kundi life halafu haki yangu ipotee,” alisema Mkoloni na kuongeza:

“Wagosi wa Kaya hatukuandika mkataba wa kuwa pamoja, kwahiyo yeye akiondoka basi na afanye hivyo kwa maslahi yake lakini kundi litaendelea kuwepo kwa sababu mimi bado nalihitaji na nina maslahi nalo.

“Kundi likifa, tukiitwa na Mdosi kugonga kopi yeye ataenda kama nani? Nadhani alipaswa kukaa na mimi tushauriane. Ni bora angesema yeye amesitisha kufanya kazi kama kundi na Wagosi wa Kaya kuliko kuzungumza kwamba limekufa. Bado lipo, nitaendelea kulisimamisha.”

Mkoloni alitoa tamko hilo, baada ya Dk John kukaririwa akisema kuwa Wagosi wa Kaya lvimekufa kwa sababu Mkoloni amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
“Hiki ni kichekesho, Wagosi wa Kaya si kundi la siasa, tulikuwa tunafanya muziki na nje ya jukwaa kila mmoja ana itikadi yake, iweje leo kujiunga CHADEMA iwe chanzo? Ningeenda CCM je?” Alihoji Mkoloni.

1 comment:

emu-three said...

Mhhh, nimechanganya manake tunaongea kuhusu Kim, nani vile, ok, let read again. Iko poa,safi kabisa