Friday, October 29, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Nicole kidman Kufunika Bongo, kiingilio bure
Nicole Kidman
Mwanadada mcheza filamu nyota, mwanamitindo na presenta mwenye mvuto wa aina yake kutoka Hollywood, Nicole Kidman anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa jijini Dar es Salaam wikiendi hii, ambapo muvi aliyoicheza ya Los Otros itaoneshwa katika Ukumbi wa New World Cinema leo jioni na kesho kuhamia Mnazi Mmoja, ikiwa ni sehemu ya tamasha linaloendelea la European Film festival ‘EFF ambapo kiingilio kitakuwa bure.


Katika muvi hiyo ambayo mwongozaji wake anaitwa Alejandro Amenabar, Nicole Kidman anatumia jina la Grace, mama wa watoto wawili ambaye mume wake aliondoka siku nyingi zilizopita kwenda kushiriki katika vita kuu ya pili ya dunia na kumuachia watoto wawili wakiwa bado wadogo. Kutokana na ugumu wa maisha, Grace (Nicole) anaishi na wanae katika hali ngumu huku watoto hao wakishambuliwa na ugonjwa wa ajabu, ambao unawazuia kutoka nje kwenye jua.


Jamii inawatenga, hakuna anayewaonea huruma, wanamsubiri baba yao kwa hamu kubwa lakini hata baada ya vita kumalizika hawamuoni akirejea, hali inayoongeza simanzi katika familia hiyo duni. Wanatekwa mara kadhaa lakini Grace (Nicole anakuwa jasiri na anapambana vilivyo kuilinda familia yake.

Filamu hiyo imetawaliwa na matukio ya kusisimua na kusikitisha yanayowaonesha jinsi mama na wanae wanavyopitia kipindi kigumu cha maisha.

Licha ya hali ngumu inayowakabili, Grace (Nicole Kidman) hakati tamaa na anaendelea kuwahudumia na kuwalinda wanae ili wasidhuriwe na chochote hadi mwisho. Mfululizo wa matukio ya kutisha na kutia uchungu unainogesha filamu hiyo kiasi kwamba unaweza kujikuta ukitokwa na machozi.


“Hii ni muvi ambayo watu hawapaswi kuikosa kwani ina mafundisho makubwa kwa watu wa kawaida na wasanii wa filamu nchini. Nawasisitiza watu waje kwa wingi New World Cinema kujionea wenyewe kwani kiingilio ni bure kabisa,” alikaririwa Tayana Tibenda, Msemaji wa Tamasha la European Film Festival linaloendelea kwa wiki tatu mfululizo.

Aidha, Tayana amewataka Watanzania hususan wapenzi wa filamu kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo filamu kali zitaoneshwa kama ilivyo ada kwa siku za wikiendi huku burudani kabambe kutoka kwa Bendi ya muziki ya Extra Bongo chini ya usimamizi mkali wa Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ ikiwaweka sawa mashabiki wa filamu nchini.

Filamu nyingine zitakazooneshwa leo ni Kirikou and the wild Beast na l’Ultimo Pulcinella, na kesho filamu ya Los Otros itarudiwa, filamu ya Wallace and Gromit, na filamu ya Kiswahili ya Vita.

***********************************************

Saa 48 kabla ya uchaguzi mkuu 2010: Mastaa hawa wanasemaje?
SINZA DAR
A.Y
“Novemba 1, mwaka huu natarajia kupanda ndege kwenda Marekani kwa ajili ya kufanya kolabo na mwanamuziki Sean Kingston na mambo mengine.
Kuhusu uchaguzi mkuu wa keshokutwa, Watanzania tuweni wazalendo, twendeni tukapige kura tuwachague viongozi wanaofaa na tuzingatie amani, utulivu na kuheshimu matokeo.”

MWANZA
BETRIACE WILLIAM

“Uchaguzi wa mwaka huu una changamoto sana kwa sababu vijana na wananchi wengi wamepata elimu ya kutosha kuhusu kupiga kura. Ombi langu kwao wajitokeze kwa wingi na kuwachagua viongozi wanofaa, zaidi tuwe wavumilivu ili tumalize zoezi hili salama, nina amini Watanzania tunaweza kwani amani ni jadi yetu.”

MISUFINI MORO
AFANDE SELE

“Mimi kama Mtanzania, kioo cha jamii naomba uchaguzi uwe wa amani na utulivu, wagombea wote wakubali matokeo hata kama watakuwa hawajashinda, wasiwe kigezo cha kuleta machafuko na kumwaga damu katika nchi yetu yenye historia ya amani.”


MWANZA
Philly Kabago
“Nikiwa nawakilisha game ya Bongo Fleva pande za Mwanza hivi karibuni natarajia kukamilisha video ya ngoma yangu mpya yenye jina la Wameshikika.

Kuhusu uchaguzi mkuu wa 2010 Watanzania tusisubiri kuchaguliwa viongozi halafu baadaye tunalalamika, tujitokeze kwa wingi tukawachague viongozi bora ambao watatuletea maendeleo katika nchi yetu, pia Watanzania tusikubali ahadi hewa wala tusiuze kura zetu.

Kikubwa ni kwamba, kabla na baada ya uchaguzi tuzingatie amani na upendo. Pia ushauri wangu kwa wagombea wote wawe tayari kukubaliana na matokeo baada ya uchaguzi, wakienda kinyume na hapo wanaweza kuhatarisha amani yetu.

KINONDONI DAR AUNT LULLU
“Mimi kama Mtanzania, kioo cha jamii naomba uchaguzi uwe wa amani na utulivu, wagombea wote wakubali matokeo hata kama watakuwa hawajashinda, wasiwe kigezo cha kuleta machafuko na kumwaga damu katika nchi yetu yenye historia ya amani.”

TEMEKE, DSM
MHE. TEMBE

“Jumamosi ya wiki hii, mimi na kundi langu, TMK Family kwa kushirikiana na wasanii wengine akiwemo Bi. Kidude tutakuwa na tamasha la kuhamasiaha vijana kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, litakalofanyika pale Kata ya 14 Temeke.
Kuhusu uchaguzi mkuu kama wewe ni mzalendo wa TZ unapaswa kupiga kura na kumchagua kiongozi ambaye una imani kwamba ataleta maendeleo katika taifa letu. Kupiga kura ni haki ya msingi ya kila mtu na tuepuke kurubuniwa na viongozi wasiokuwa waaminifu.”

TANGA
Q CHILLER

“Leo Ijumaa ndani ya Tanga Beach Resot mimi na wasanii wengine kama Domokaya na Bob Junior tunatarajia kufanya tamasha kubwa kwa ajili ya kuongea na vijana ili siku ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi. Mgeni rasmi katika shoo hiyo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Kalembo.
Kuhusu uchaguzi mkuu wa keshokutwa Watanzania wapige kura kwa amani na viongozi wakubaliane na matokeo.

Nakumbuka wakati uchaguzi mkuu wa Kenya unafanyika miaka ya hivi karibuni nilikuwa nchini humo, nilishuhudia vizuri yale machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi, kwa hiyo nisingependa yatokee nchini kwetu.”
compiled by mc george,ijumaa newspaper

No comments: