Saturday, January 1, 2011

KARIBUNI KATIKA JUKWAA LA SANAA LA KWANZA KWA MWAKA 2011

Wadau Heshima kwenu na heri ya mwaka mpya kabisa wa 2011.Napenda kuwafahamisha kwamba,Katika Jukwaa la Sanaa litakalofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA Jumatatu hii kuanzia Saa 4.00 Asubuhi,Mratibu wa Tamasha maarufu la Sauti za Busara Bw.Kwame Mchauru atazungumzia ‘Mchango wa Matamasha Katika kukuza ajira na Sekta ya Sanaa kwa ujumla nchini.

Wasanii na wadau wote wa sanaa mnakaribishwa kwa wingi katika Jukwaa hili kwani ni muda mzuri wa kujifunza umuhimu wa matamasha na jinsi ya kujipanga kabla ya kupanda jukwaani.Aidha,Tutapata wasanii wa kujua lini Tamasha la Usiku wa Busara litaanza, litakuwa na sura gani na ni wasanii wa aina gani watapata wasaa wa kupanda jukwaani.

Kutakuwa na fursa pana ya kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu tamasha hili na sekta ya sanaa kwa upana wake katika mwaka huu mpya.Tuanze mwaka kwa maono mapya na mikakati mipya katika kukuza sanaa zetu.
Nyote mnakaribishwa,Sanaa ni Ajira,Tuithamini


No comments: