Thursday, March 31, 2011

KUNDI LA MIZENGWE LAFUNIKA KWENYE JUKWAA LA SANAA


Msanii machachari anayeigiza sauti za viongozi na watu maarufu nchini,Raymond Mushi akionesha vitu vyake mbele ya wadau wa Jukwaa la Sanaa wiki hii.

Hemed Maliyaga aka Mkwere (Kulia) akiliongoza Kundi lake la Mizemgwe kufanya vichekesho mbalimbali vilivyowavunja mbavu wadau wa Sanaa kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.Wengine kutoka kushoto ni wasanii wa kundi hilo,Habibu Mrisho aka Sumaku,Rashid Coster aka Malingo Saba na Jesca Kindole aka Safina.
Wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa linaloandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) na kufanyika kwenye Ukumbi wa BASATA Kundi maarufu la vichekesho la Mizenge linalorusha vipindi vyake kupitia Kituo cha runinga cha ITV lilitoa burudani ya aina yake iliyochangamsha wadau wa sanaa muda wote.

Kundi la Mizengwe likiongozwa na Hemed Maliyaga aka Mkwere lilifanya burudani ya aina yake huku likionesha uwezo na uzoefu mkubwa katika vichekesho mbalimbali ambavyo viliwavunja mbavu wadau wa Jukwaa la Sanaa na kuwafanya muda mwingi wautumie kushangilia na kupiga makofi.

Wadau walivunjika mbavu zaidi pale Muigizaji maarufu wa sauti mbalimbali za viongozi, Raymond Mushi aliposimama na kuanza kuigiza sauti za viongozi na watu maarufu ikiwemo ile ya Katibu Mkuu wa CCM,Yusuph Makamba,Mzee Reginald Mengi,Baba wa Taifa Marehemu Julius Kambarage Nyerere na ile ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu,Benjamin Mkapa.

No comments: