Maafisa masoko nchini wametakiwa kuwa wabunifu ili kuyawezesha makampunia yao kuendelea kufanya vizuri katika mazingara ya sasa ambayo yanaushindani mkubwa wa kibiashara.
Akiongea katika usiku maalum wa maafisa masoko uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Chiruyi Walingo (Pichani kabisa) ambaye in Afisa Biashara Mkuu wa kampuni ya Airtel Tanzania, alisema fani ya masoko ina changamoto nyingi ambazo zinahitaji ubunifu ili kukabiliana nazo.
"Idara ya masoko ni moja ya idara nyeti sana katika kampuni yoyote ile. Idara hii naweza kusema ndiyo roho ya kampuni kutokana na ukweli kuwa kufanikiwa kwa kampuni yoyote kunategemea sana juhudi za watu wa masoko ," alieleza
Walingo aliwaeleza washiriki wa usiku wa wanamasoko kuwa ushindani mkubwa ni moja kati ya changamoto ambayo inamuhitaji afisa masoko afikiri sana na kuwa mbunifu ili aiwezeshe didhaa ya kampuni yake iendelee kuwepo na kufanya vizuri sokoni.
"Ni muhimu sana kwa afisa masoko kuwa mbunifu na kuwa tayari kupambana na changamoto za kimasoko. Unaweza katumia muda wa mwezi mmoja kufikiria na kugundua bidhaa mpya lakini mshindani wako akaikopi kwa dakika moja tu. Lakini hii ni changamoto ya kukufanya wewe ufikiri zaidi," alieleza.
Alisema maafisa masoko wanakiwa kuwa na washauri ambao wamekuwa kwenye fani kwa miaka mingi kwa ajili ya kuwapa ushauri na kupitia uzoefu wa siku nyingi wa watu hao wanaweza kujikuta wakijifunza mambo mengi amabayo yatazidi kuwajenga kitaaluma.
"Wakati mwingine unaweza kujikuta hujafikia lengo ulilojiwekea au kuwekewa na inaweza kukufanya ukate tamaa. Mshauri ni muhimu sana kwa vile atakusaidia kwa kukupanua mawazo kupitia uzoefu wake wa siku nyingi na hivyo kujikuta unazimudu vyema changamoto na kuwa mwenye mafanikio katika kazi yako," alieleza

No comments:
Post a Comment