Sunday, September 4, 2011

Mrembo Rose Albert anyakua taji la Vodacom Miss Talent 2011

odacom Miss Talent 2011 Rose Albert akiwapungia mkono watazamaji  mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo, hapo jana katika hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam.
Warembo tano bora waliofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha Vodacom miss talent 2011 ambapo Rose Albert watatu toka kushoto alifanikiwa kunyakua taji hilo hapo jana katika hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam.
Mrembo Rose Albert akionyesha kipaji chake katika siku ya kumtafuta Vodacom Miss Talent 2011 ambapo alifanikiwa kunyakua taji hilo,Jana katika hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakipozi kwa picha 
 Majaji wa shindano la Vodacom miss Talent 2011 wakiwa kazini,kutoka kushoto Jacqueline Walper,Rachel Sindbard na Bosco Majaliwa.
Na Mwandishi Wetu
Mrembo Rose Albert anaeshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, Jana aliwabwaga baadhi ya Washiriki wenzake  aliochuana nao vikali na kunyakua taji hilo katika siku ya kuonyesha vipaji”Vodacom Miss Talent” iliyofanyika kwenye hotel ya Giraffe iliyopo Mbezi  jijini Dar es Salaam.

 Wakiadhimisha siku hiyo washiriki hao wa shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo nchini walichuana kwa kuonyesha vipaji vyao  mbalimbali ikiwemo kuimba, kucheza miziki mbalimbali ya Bongo flava,nyimbo zetu za kiutamaduni,maigizo. 

Akizungumzia siku hiyo Meneja Uhusiano na Habari za  Mtandao Matina Nkurlu alisema lengo la siku hiyo ni kutaka kutambua vipaji mbalimbali walivyonavyo  warembo  wakiwa tayari kuelekea kwenye hatua ya mwisho ya shindano hilo lenye hadhi ya kimataifa litakalofanyika mlimani city  tarehe septemba 10.

Akifafanua Nkurlu alisema kwamba mbali ya kutaka kujua vipaji vyao pia imesaidia kuibua vipaji vya warembo hao mbali na fani ya urembo wanayojihusisha nayo.

“Tukiwa kwenye siku ya  Vodacom Miss Talent  warembo wameonesha vipaji vyao vya kipekee  jambo lililowafanya pia kuendelea kuwa pamoja kama ilivyo tasnia hiyo kwamba inawaunganisha watu wote bila kujali dini rangi au kabila.

Nae  mrembo Rose Albert alienyakua taji hilo amesema siku hiyo ni ya faida kwake kwani ameweza kuonyesha vipaji vyake mbalimbali alivyonavyo na kujifunza mengi toka kwa washiriki wenza. 

Akifafanua Rose alisema mbali ya kuonesha viapaji vyake  pia amepanua mtazamo wa kiakili kwani ni moja ya fani zinazoenda kushindaniwa katika shindano la Miss World kwa atakayebahatika kuliwakilisha Taifa letu.

“Vipaji  ni moja ya vipengele kwenye shindano la urembo la dunia, hivyo kwa atakayebahatika atafanya vizuri kwani  vipaji kitu muhimu  tayari kwa kwenda kushiriki michuano hiyo ya urembo ya dunia.

Nae Mkuu wa kitengo cha Itifaki wa Kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye alisema ari waliyonayo warembo inaonesha utayari wao katika kuliwakilisha Taifa katika medani za kimataifa.

“Mmejionea wenyewe baadhi ya washiriki wetu walivyochuana katika shindano hili la Vodacom Miss Talent 2011 katika kuadhimisha siku ya vipaji  kwa warembo. Hili tu linadhihirisha kwamba shindano la mwaka huu litakuwa na changamoto kubwa ikilinganishwa na mengine yaliyopita,” alisema Makoye.

Nawaomba watanzania wenzangu waendelee kuwapigia kura  washiriki hao wanaoishi ndani ya jumba la Vodacom na watazame vituo vya televisheni  Star tv na Clouds TV baada ya maisha yao ndani ya nyumba kuoneshwa moja kwa moja na vituo hivyo.

No comments: