Sunday, October 23, 2011

ARUSHA YATAMBA MBIO ZA”Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge 2011"

Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Mwanza na Shinyanga Elisha Eliasi akizindua mbio za Vodacom Mwanza Openi Cycle Challenge 2011,katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Ephraim Mafuru na Meneja Mauzo wa  Vodacom kanda ya Ziwa Amos Vuhahula,Mbio hizo zilianzia mjini Shinyanga na kumalizikia Bugando Jijini Mwanza,Mbio hizo ziliandaliwa na Vodacom Tanzania na kudhaminiwa na kinywaji cha Malta Guinness. 
Washiriki wa mbio za”Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge za Kilometa 196  wakichuana vikali wakati wa kumaliza  mbio hizo zilizoanzia Shinyanga na kumalizikia Bugando jijini Mwanza,Mbio hizo ziliandaliwa na Vodacom Tanzania na kudhaminiwa na kinywaji cha Malta Guinness. 
Mshindi wa pili wa mbio za baiskeli za”Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge 2011.Mindi Mwagi(Shinyanga) akimaliza mbio hizo alipotumia Masaa 5:02:29  katika mbio hizo,zilizoanzia Shinyanga na kumalizikia jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Serengeti Breweries Ephraim Mafuru,akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa mbio za walemavu ambazo pia zilikuwa moja ya mbio hizo katika mbio za”Vodacom Mwaza Open Cycle Challenge 2011 kudhaminiwa na kinywaji cha Malta Guinness. 
 Mkurugenzi wa Serengeti Breweries Ephraim Mafuru katikati,akiteta jambo na Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa   mbio za”Vodacom Mwaza Open Cycle Challenge 2011,kulia Meneja wa kinywaji cha Malta Guinness Mauruce Njowoka.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Hatimaye Richard Laizer wa mkoani wa Arusha ndiye ametegua kitendawili cha nani anayepaswa kuwa mshindi wa mbio za wazi za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge baada ya kuwashinda washiriki wengine zaidi ya 400 walijitokeza kushiriki kwenye mashindano hayo kwa upande wa wanaume.

 Kutokana na ushindi huo amejinyakulia zawadi ya shilingi Milioni Milion Moja na Nusu na kuvikwa taji lililokuwa likishikiliwa na Hamis Clement wa Shinyanga baada ya kutumia muda wa Masaa 5:02:28 kumaliza mbio hizo za kilometa 196.

 Mshindi wa pili wa michuano hiyo kwa wanaume ni Mindi Mwagi kutoka mkoani Shinyanga aliyetumia saa 5:02:29 ambaye amezawadiwa shilingi Milioni Moja akifutiwa na mshindi wa tatu Said Jumanne aliyezawadiwa kiasi cha shilingi Laki saba yeye akiuwakilisha mkoa wa Arusha.

 Kwa upande wa  wanawake Mkoa wa Arusha  uliibuka kidedea baada ya mshiriki wake Bi Sophia Hussein kuwabwaga washiriki wenzake zaidi ya zaidi 60 na kunyakua nafasi ya kwanza katika mashindano hayo ya kilometa 80 baada ya kutumia muda wa Masaa 2:25:13 kumaliza mbio hizo.

 Hivyo kwa ushindi huo Bi Hussein amejishindia kitita cha shilingi Mil1,100,000 na kushikilia taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Sophia Adison wa Arusha huku akifuatiwa na mshindi wa pili Bi Mwajuma Musa kutoka mkoani Arusha aliyetumia Masaa 2:25:40 na kujinyakulia zawadi ya shilingi Laki nane.

Hata hivyo mkoa wa Shinyanga nao haukuwa nyuma katika mashindano hayo baada ya Bi Salome Donard baada ya kushika nafasi ya tatu ambapo alizawadiwa kiasi cha shilingi 600,000 baada ya kutumia Masaa 2:26:21 kuhitimisha mbio hizo za kilometa 80 kwa wanawake.

Akizungumza baada ya mashindano hayo,Richard Laizer alisema kilichomsadia ni mazoezi  na maandalizi ya mara kwa mara aliyokuwa akiyafanya ingawa mlima wa Bugando wa kumalizia mbio hizo ulimsumbua katika mashindano hayo.

 “Nashukuru kwa kumaliza salama na kuwa bingwa katika michuano hii, kutokana na zawadi hii niliyopata kutoka Vodacom Tanzania na wadhamini Wenza Serengeti Breweries kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Malta Guinness nitajiendeleza zaidi ili kufikia viwango vya uendeshaji baiskeli kimataifa,” alisema Laizer.

 Kwa upande wake Bi. Sophia Hussein alisema mashindano ya mwaka huu kwake yalikuwa na upinzani mkali kwa sababu ushindani ulikuwa ni wa hali ya juu hasa wenye baiskeli za Phoenix ambao walikuwa hawampi nafasi.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa Bw Steven Kingu,ambae ndiye alikuwa mgeni rasmi aliwapongeza washiriki wote hususani washindi na kuahidi kwamba kampuni yake itaendelea kuratibu, kuandaa michuano hiyo ili kuifanya kufikia michuano ya kimataifa.

“Nimefarijika kwa mbio hizi za wazi za Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge kuendelea kuwa bora kila mwaka na hili linatupa changamoto za kuendelea kuandaa na kudhamini katika mikoa mingine kama sio Tanzania nzima,” alisema Kingu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) Ephraim Mafuru ambao ni wadhamini wenza kupitia kinywaji kisicho na kilevi cha Malta Guinness alisema hawajutii kudhamini michuano hiyo kutokana na hadhi iliyonayo.
“Tumeshuhudia kupitia udhamini wetu washindi wamejipatia zawadi ambazo kama watazitumia vema zinaweza kuwa mitaji itakayowawezesha kujiletea maendeleo katika ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla,” alisema Mafuru.

No comments: