Sunday, October 16, 2011

HATARI!

****Na mwandishi wetu****
Hapo jana, maeneo ya Ubungo, Mwandishi wetu amejionea hali isiyo ya usalama katika maeneo hayo ambapo wafanyabiashara wadogo, maarufu kama machinga, wamekuwa wakifanya biashara katika mazingira hatarishi hasa ukizingatia kuwa eneo hilo limezungukwa na mitambo ya kuzalisha na kusambaza umeme, jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha yao na ya waendao kwa miguu na wanunuzi. Hatari hiyo inatokana na ukweli kwamba watu huwa wengi jioni katika eneo hilo jambo linaloweza kusababisha maafa makubwa sana iwapo janga la moto litatokea.

Daima kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni ombi letu serikali kuliangalia jambo ili kwa upana zaidi ikiwa ni pamoja na kupitia alama za kiusalam ili kuepusha janga lolote kutokea katika eneo hilo badala ya kusubiri janga kutokea ndipo ikumbukwe kuunda tume ya kuchunguza wakati tayari maisha ya watu wasio na hatia yatakuwa yamepotea.

Inatoka; http://www.mkandawilejr.blogspot.com

 

No comments: