Sunday, October 16, 2011

TANZANIA GIVES BACK yatoa msaada kituo cha wazee waliothiriwa na ugonjwa wa ukoma.

Mwendeshaji wa kipindi cha Njia Panda  kinachorushwa na redio ya Clouds FM,Dr Isaac Maro (kulia) akiutazama mguu wa Mzee Rasmo Kilata ambaye mguu wake ulikatwa mara baada ya kuathiriwa na ugonjwa kansa,ambao ulitokana na kidonda chake alichokipata kwa muda mrefu bila kupona,Mzee huyo wa makamo mwenye watoto 3 na wajukuu wasio na idadi pia ni mlemavu wa ugonjwa ukoma,Shoto ni Mwenyekiti wa Kampeni ya Tanzania Gives Back,Edmond Lyatuu akiwa pamoja na mratibu wa Kampeni hiyo,Dada Susan,kampeni hiyo ya Tanzania Gives Back 2011 inaratibiwa na kituo cha Tanzania House Of Talent (THT).
Mwenyekiti wa kampeni ya Tanzania Gives Back 2011,Edmond Lyatuu pichani kulia akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi mapema leo asubuhi kwa baadhi ya wazee waishio kwenye kambi ya Walemavu na Wasiojiweza ya Nunge,Vijibweni-Kigamboni jijini Dar es salaam.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ditto akiimba moja ya wimbo wa kuwafariji na kutia moyo wazee hao ambao wengi wao wameathiriwa na ugonjwa wa ukoma.Wazee hao wanaishi kwenye kijiji hicho cha Nunge chenye jumla ya nyumba 50,ikiwa na idadi ya familia 72,ambapo kila nyumba inakaliwa na watu 5 mpaka 7.Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mzee Issa Ally ameiomba Serikali na wadau wengine kuja kuzikabarabati nyumba zao wanazoishi kwani kwa sasa zimechakaa sana,amesema na kuongeza kuwa wanahitaji msaada mkubwa wa kupuliziwa dawa ya kuuwa wadudu katika nyumba zao,kwani kumekuwepo na wadudu wengi wakiwemo Viroboto,Mende na wengineo ambao wamekuwa wakiwapa taabu sana.
Wanaharakati wa kampeni ya Tanzania Gives Back wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee hao.
Mwenyekiti wa Tanzania Gives Back,Edmond Lyatuu akizungumza na baadhi ya wazee wenye ulemavu wa mikono,macho na miguu kutokana na kuathiriwa na ugonjwa wa Ukoma,Wazee hao wametoa kilio chao kwa Serikali na wadau mbalimbali kwamba wajitokeze kuwasaidia wazee wao kwa namna moja ama nyingine,kwani kwa sasa wamekuwa wakiishi katika hali ngumu hivyo bado wanahitaji msaada mkubwa wa hali na mali.
Mwanaharakati,Mama Sadaka Gandi kutoka THT,ambao ndiyo waratibu wa kampeni ya Tanzania Gives Back,akizungumza na Wazee waliothiriwa na ugonjwa wa Ukoma mapema leo asubuhi kwenye kambi yao ya Nunge ilioko Vijibweni-Kigamboni jijini Dar es salaam.
Dada Kemi kutoka Tanzania Gives back akiongea na kuwafariji Wazee walioathiriwa na ugonjwa wa Ukoma,Wazee hao ambao wamekuwa wakiishi kwenye kijiji hicho kilichoanzishwa rasmi mnamo mwaka 1975 na kuanza kuhudumiwa na Serikali,wamewashukuru sana wafadhili mbalimbali ambao wamekuwa wakitokeza na kuwapa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiwasaidia kwa kikubwa,ingawaje wanakiri kuwa bado haitoshi hasa kulingana na mahitaji yao ya kila siku.
 Pichani na juu ni wazee wakiwasikiliza wageni wao waliofika kuwatembelea  mapema leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Tanzania Gives Back 2011,Edmond Lyatuu akizungumza na Afisa Kilimo Msaidizi wa kituo hicho cha Walemavu na wasiojiweza kiitwacho Nunge, Bwa. Frank Mnuo mambo mbalimbali yahusuyo kituo hicho pamoja na changamoto wanazozipata.Shoto ni Dada kemi ambaye pia ni mmoja wa waratibu wa kampeni hiyo.

No comments: