Wednesday, November 9, 2011

Vodacom yatangaza zawadi za fainali za TIKISA

 Meneja huduma na bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw. Elihuruma Ngowi akionyesha Tablet V9  moja ya zawadi ya zitakazotolewa kwa washindi wawili wa kwanza  katika fainali za shindano la TIKISA litakalofanyika mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Vodacom (kushoto) ni Meneja wa Power House Ndg. Octavian Francis.
 Meneja huduma na Bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi  ya Vodacom Tanzania Bw. Elihuruma Ngowi akiaonyesha zawadi mbalimbali za simu za mkononi kwa washiriki waliofanikiwa kuingia fainali za shindano la TIKISA ambao ni  Helen Mangare, Hawa Mohamed, Hassan Said na Daniel Tobias wakati walipozuru Makao makuu ya Vodacom Mlimani City Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Vodacom Najenjwa Mbaga (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa washiriki wa fainali za TIKISA kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kitengo hicho kwa wateja wake pindi walipopata fursa ya kutembelea Makao makuu ya Vodacom Tanzania (kulia kwake) ni Meneja wa huduma kwa wateja Bi. Edith Ezekiel.
 Meneja wa huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania Bi. Edith Ezekiel akifafanua jambo kuhusu huduma kwa wateja zinavyoendeshwa kwa washiriki waliobahatika kuingia katika fainali za shindano la TIKISA walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi hizo eneo la Mlimani City ambapo Fainali za shindano hilo zitafanyika mwishoni mwa wiki .
 Washiriki wa fainali za shindano la TIKISA wakipata maelekezo kutoka kwa Mtoa huduma kwa wateja wa Vodacom Bw. Nemes Kimati jinsi wanavyohudumia wateja wao pindi walipotembelea Ofisi za Vodacom Tanzania ikiwa ni safari yao kuelekea katika kilele cha shindano hilo mwishoni wa wiki.
Meneja wa Vodashop Mlimani City. Happiness Macha akitoa maelezo kwa  washiriki wa shindano la TIKISA baada ya kuwapatia vipeperushi vyenye kuonyesha huduma mbalimbali zitolewazo na Vodashop ambazo ni pamoja na M-pesa, vifurushi vya internet na nyingine nyingi wakati walipotembelea kujionea na kujifunza huduma zinazotolewa katika Duka hilo.

No comments: