Sunday, December 25, 2011

Clouds Media Group yatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko jijini Dar!

 
Kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Clouds FM/TV, Shafii Dauda, alipokuwa akiwafanyia mahojiano mafupi kwa wachezaji wa mpira wa miguu wa zamani ambao wameathirika na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni, anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh.Idd Azan, Mwanamtwa Kihwelu (aliyewahi kuichezea timu ya Simba na Yanga), Robert Damian (mwenye kofia-Simba), Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Clouds Fm/TV Ibrahim Masoud, Dua Said (Small Simba & Simba S.C),Maalim Salehe a.k.a Romario (Yanga),  Shaaban Ramadhan (Simba, Yanga, Mlandege & Mtibwa) pamoja na Mke wa Marehemu Nico Bambaga ambaye alikutwa akijishughulisha kutoa tope zito lililokuwa limenasa kwenye nyumba yake aliyokuwa akiishi na familia yake. Wachezaji wote hao akiwemo Peter Manyika ambaye hayupo pichani nyumba zao zote zimeathiriwa vibaya na mafuriko.

 
Aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Yanga na Simba, Mwanamtwa Kihwelu, akifafanua namna adha ya mafuriko ilivyowakumba, mbele ya Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Mh Idd Azan, wakati kampuni ya Clouds Media Group ilipokwenda kutoa misaada kwa waathirika na pia kujionea maeneo mbalimbali yalivyoharibiwa na mafuriko hayo, pichani kati ni mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group, Bw.Ruge Mutahaba ambaye pia aliongozana na baadhi ya wafanyakazi wa kampun hiyo mpaka eneo hilo la tukio na kujionea hali halisi.

.Mmoja wa wachezaji waliowahi kuwika miaka kadhaa nyuma,Dua Said akionesha nyumba yake ilivyoathiriwa na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar.
Mkurugenzi wa Biashara Clouds Media Group, Dada Sheba, akitoa salamu za pole kwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni,Mh Idd Azan kwa niaba ya baadhi ya Wananchi wake walioathiriwa na mafuriko.

 
Mbunge wa jimbo la Kinondoni,Idd Azan akizungumza na baadhi ya wananchi waliothirika na mafuriko kwenye kambi yao ya muda iliyopo shule ya msingi ya Lutihinda,Kigogo jijini Dar.
 
Pichani juu na chini ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Dogo Ditto pamoja na AT wakiwaimbia baadhi ya watoto walioko kwenye kambi ya muda ya waliothirika na mafuriko.
PICHA: Hisani ya Michuzi Jr.

No comments: