Kijana Edwin Dossantos na mkewe waliojaliwa kupata watoto watatu mapacha mwezi wa 7 mwaka huu ametoa shukrani zake za dhati kwa wasamaria wema wote waliomsaidia kwa hali na mali kutoa michango kwa ajili ya malezi ya watoto hao kutokana na halisi ya kipato chake kuwa cha chini na maisha kuzidi kuwa magumu.
Akizungumza na MO BLOG ilipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kimara jijini Dar es Salaam, Dossantos amesema ni msaada wa wasamaria wema ndio umemuwezesha kumudu gharama za matumizi kwa ajili ya watoto hao haswa ukizingatia hakuwa na kazi.
Aidha Dossantos licha ya kuwashukuru wanao onekana katika orodha hii, pia amewashukuru na wale ambao hawakutaka kujulikana waliomsaidia kupitia mawakala wa M-Pesa pasipo kujitaja majina yao, ambao licha ya kuwashukuru amesema hawakumtendea haki kwa kuwa wamemnyima fursa ya kuwashukuru kwa majina yao wala namba zao.
Dossantos ametoa shukrani kwa watu waliosaidia kwa namna mbalimbali kama wanavyoonekana katika orodha ifuatayo.:-
Mr. Frank wa DSM, Mrs. Norah wa Silver Boutique, Mama Sige wa KIBAMBA, Mrs.Pamela wa USA, Mr. Sagday wa DSM, Mrs. Caroline Kazinza wa AZANIA BANK-Tegeta, Mrs. Emakulata wa UK, Miss Nyota Omary wa NORWAY, Mr. Joshua wa DSM, Mrs.Pamela wa DSM, Mrs.Mosha wa ARUSHA, Mrs. Lestituta wa DSM, Mrs. Theresia na Mrs Zahara wa Hisense DSM, Mr. Shabiby wa GAIRO Morogoro, Mrs. Fane wa DSM, Mrs. Ikupa wa AZANIA BANK-Tegeta DSM, Mrs. Vale wa AZANIA BANK-Tegeta DSM, Miss Hoyce Temu wa Channel Ten DSM, Mrs. Mercy Mariale wa DSM, Mr. Rongen Kambugu wa Kigali RWANDA, Advocate Komba wa NSSF-DSM, Miss Jehn wa DSM, Mr. Freya Mahinya wa Zanzibar, Mr. Chube wa DSM,Mr. Yusuph Mdoe wa DSM, Mr.Emmanuel Messo wa WORLD BANK-DSM, Mr. Deogratius Rweyunga wa ITV-DSM, Mr. Iddi Kibwana wa TTCL-DSM, Mr. Hashim Lundenga wa DSM na Bi. Asia Waziri Moyo wa Zanzibar.
Hata hivyo amesema watoto hao ambao kwa sasa wanaumri wa miezi 5 bado wanahitaji msaada angalau hadi wafikishe umri wa miezi 6 ambapo watakuwa wanaanza kula vyakula vya kawaida.
Katika hatua nyingine Edwin Dossantos ametoa ombi kwa msamaria mwema atakayekuwa na uwezo wa kumpatia nafasi ya kazi yoyote itakayompatia kipato cha kuweza kumudu gharama za malezi ya watoto hao.
Amesema bila ya yeye kuwa na kazi ya kumuingizia kipato anaweza kuja kwa wasamaria kuomba misaada kila mara, hivyo ameshukuru kwa kumpatia kile alichokiita samaki na sasa anaomba nyavu (Kazi) ili avue mwenyewe.
Edwin Dossantos anapatikana kwa simu ya mkononi namba 0719 909085 na 0767 646599.
No comments:
Post a Comment