Marehemu David Wakati
Frank Mtao, atuma salamu kutoka Autralia
Marehamu Mr. Ebbo (kati) akiwa na wasanii wenzake Jay Moe na Hussein Machozi (kulia).
Kazi ya mwisho kufanya nawe, ilikuwa ni ya uchunguzi juu ya uelewa wa wananchi kuhusu katiba, ambapo tulizunguka karibu nchi nzima vijijini na mijini, hii yapata takribani miaka 8 iliyopita hivi!
Lakini kumbukumbu ya yale tuliyoyaona na kusikia hakika haitonitoka kamwe.
Leo hii tunapozungumzia katiba, ningetamani sana uwepo na tukumbushane safari yetu hiyo iliyokuwa na mengi ya kuelimisha, kufurahisha na kuhuzunisha!
Hakika nilifurahi na kujifunza mengi toka kwako mkubwa wangu na rafiki yangu mpendwa DAVID WAKATI!
Hata wiki haijaisha pigo lingine la kuondokewa nawe Mr Ebbo limeniacha na mshangao! Ebbo tulipenda kutaniana sana, hasa pale nilipokuwa nikikutania "njaa inakufanya uwe mbunifu"!
Ulitoka kwa aina yako ya kipekee ktk muziki wa bongo na hata baada ya kufungua studio yako, nilikupongeza na kuzidi kukutania zaidi na zaidi! Ntacheka vipi utani huo rafiki yangu Ebbo ukiwa hauko hapa tukacheka pamoja!
Ingawaje niko mbali huku Australia, ila naungana na ndugu, jamaa na marafiki ktk kipindi hiki kigumu cha kuondokewa nanyi tuliowapenda ila Mwenyezi kawapenda zaidi.
Ewe Mola, uwalaze mahali pema peponi rafiki zangu Mr EBBO na DAVID WAKATI, Amina!
No comments:
Post a Comment