Rais
Jakaya Kikwete akiteta jambo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda huku
Katibu Mtendaji wa Kamati ya Kimataifa ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR)
anayemaliza muda wake Balozi Liberata Mulamula akitega sikio katika siku
ya pili ya mkutano huo wa viongozi wakuu wa ICGLR wa kupinga
unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort
kitongojini Munyonyo, Kampala, Desemba 16, 2011.

Rais
Jakaya Kikwete akimuwekea chaneli ya kupata lugha Rais Mwai Kibaki wa
Kenya katika siku ya pili ya mkutano huo wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji
na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini
Munyonyo, Kampala, Desemba 16, 2011.

Rais
Jakaya Kikwete akichangia mada katika siku ya pili ya mkutano huo wa
ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke
Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, Desemba 16, 2011.

Rais
Jakaya Kikwete akiongea na Rais Michael Satta wa Zambia na mkewa usiku
wa kuamkia leo, muda mchache kabla hawajaelekea Ikulu ya Entebbe ambako
Rais Yoweri Museveni aliandaa chakula cha usiku kwa wajumbe wa mkutano
huo wa viongozi wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia
hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, Desemba 16, 2011.
PICHA ZOTE NA IKULU.
No comments:
Post a Comment