Monday, January 2, 2012

Diamond aswekwa rumande Iringa

 MSANII  maarufu    wa  muziki  wa  kizazi  kipya  Naseeb  Abdul  a.k.a Diamond na  wacheza  show wake  wawili  wamejikuta  wakifunga  mwaka  vibaya  baada ya  kutupwa  rumande  kwa kosa la  kumshambulia na kuharibu  mali  za mwandishi  wa  habari  wa   mkoani  Iringa Francis  Godwin.

Sakata  la  Diamond  kumshambulia  mwanahabari  huyo  maarufu  hapa  nchini  lilitokana na hatua utata  uliokuwa  umejitokeza katia  uwanja  wa  Samora  mjini  Iringa ambako  Diamond  alipaswa  kufanya  onyesho  lake ya  kuuanga na kuukaribisha  mwaka 2012 .

Hata  hivyo  onyesho  hilo  lilionyesa kuwa na kila aina ya utapeli  baada ya ratiba  kuonyesha  kuanza saa 8 mchana na kumalizika  mida ya saa 12  za jioni na baada ya hapo uwanja  huo  ulipaswa  kutumiwa na umoja wa Makanisa  mkoani  Iringa kwa  ajili ya mkesha  wa kufunga mwaka na mkuu wa mkoa  wa Iringa Dkt  Christina Ishengoma ndie  alikuwa mgeni  rasimi.

HIvyo  kutokana na msanii  huyo kushindwa kuonekana hadi mida ya saa 11.50 jioni  mashabiki  kiduchu  ambao  walikuwa  wameingia katika  uwanja  huo  walilazimika  kumvaa mmoja kati ya  wahusika katika onyesho  hilo ambaye  alikuwa akichukua  fedha  za kiingilio mlangoni na kuanza kuhoji  sababu ya onyesho  hilo kukwama na msanii  Diamond na Afande  Sele  ambao  walipaswa  kupagawisha  kutoonekana  hadi mida  hiyo na kuhoji  sababu  ya tiketi  za chama cha  soka mkoa  wa Dar e s Salaam (DRFA)  ambazo  zinaonyesha   kuna mchezo  wa  kirafiki kati ya Asante  Kotoko ya Ghana na Marafiki  wa Uhuru  mchezo  uliochezwa 12/11/2011 uwanja  wa Taifa na kiingilia  ni shilingi 5000 huku  wao   wamefika  kuona  wasanii na sio mechi.


Hata  hivyo  haikuchukua  muda  ghafla  Costa  ambayo  ilikuwa  imembeba Diamond  na  wacheza  show  wake  bila Afande  Sele  iliwasili  uwanjani hapo na  kufanya mashabiki  kupunguza jazba.


Kutokana na  hali ya utulivu  kurejea uwanjani hapo  mwandishi  wa habari huyo ambaye ni mmiliki wa blogu  maarufu nchini ya  www.francisgodwin.blogspot.com
  na makampuni  ya New Habari LTD alimfuata na  kwa nia ya  kutaka  kufanya nae  mahojiano na kujua  sababu za kuchelewa katika  show  hiyo hapo ndipo Diamond  alipogeuka mbogo na kupokonya kamera  ya  kuirusha  chini baada ya  kufuta picha .

Baada ya hapo  mashabiki  walimlazimisha  Diamond  kupanda jukwaani  kuimba vinginevyo  wangemchapa hivyo  kulazimika  kupanda jukwaani  huku akisimamiwa  kwa  bakora na mawe ,pamoja na kupanda  jukwaani  bado  alishindwa  kuimba baada ya wale  waliokodisha  vifaa vya muziki  kugoma kupiga muziki kwa madai  muda  wao  umekwisha  huku  watu wa mkesha wa makanisa  nao  wakipinga  jukwaa la ibada ya mkesha  kutumika kwa mambo ya kidunia hali  iliyozua  utata .


Hali  hiyo  ilimfanya Diamond  kuchanganyikiwa  zaidi na kushindwa kushuka  jukwaani kwa kuhofia  kichapo toka kwa mashabiki kutokana na hali  hiyo mwandishi  alianza  kufanya mahojiano na  kuchukua  picha  za mashabiki kusubiri na  kumsimamia  msanii  huyo kabla ya  kuruka  jukwaani na kikosi  chake na kuanza  kumchapa  mwandishi  huyo  ambaye  pia  alionyesha   kukabiliana nao kwa kiasi na kusaidiwa na mashabiki .

Kutokana na  tukio  hilo  mwandishi  huyo  wa habari  Godwin  alipoteza camera  yake yenye thamani ya  shilingi milioni 1.5, simu moja  yenye  thamani ya shilingi 300,000 huku Laptop yake ndogo aina ya Acer  ikiharibiwa  na msanii  huyo.


Tukio  hilo  lilifikishwa  polisi na Diamond  kufunguliwa  mashtaka ya  kushambulia   kwa RB namba  IR/RB/ 7700/2011 na baada ya  muda  mida ya saa 1.30 usiku  jeshi la  polisi  lilikwenda  kumkamata msanii  huyo na vijana wake  wawili ambao  walikuwa katika  Hotel ya Staff Inn Anex mjini hapa wakijipumzisha  na kupelekwa mahabusu hadi  asubuhi .


Mratibu  wa  show  hiyo Mike T akiomba msamaha  kwa  mwandishi  huyo  alisema  kuwa  msafara  wa Diamond ulikuwa  ukitokea  Mbeya  katika uwanja  wa Sokoine ambako  pia  Show ilikwama  kutokana na mvua  kubwa  kunyesha na baada ya  hapo  walianza  safari kwa ajili ya kuja  Iringa na  kukwama kufika kwa wakati  kutokana na basi  lao la kwanza  kuharibika na kulazimika  kukodi  Costa na kufika kwa mida mibaya  Iringa na  kuwa  baada ya  Iringa  Msafara  huo  ulitaraji  kwenda jijini Dar es Salaam  kuzindua Albam yake .

No comments: