Baada
ya shughuli nzima ya maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend
Special,kinachorusha na redio ya Wapo FM,wageni waalikwa walipata picha
ya pamoja kama ukumbusho muhimu kwao,nje ya jengo la mikutano la Taasisi
ya Maendeleo ya Vijana (UVIKIUTA),iliopo Chamazi-Mbagala jijini Dar.
Keki tuliii safi kabisa.
Mmoja wa wageni kutoka meza kuu,Wakili
wa Kujitegemea Bw. Emanuel Makene akikata keki kwa ajili ya kulishwa
wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho ya kipindi hicho
ambacho kimekuwa kikipendwa na kusikilizwa sana wanajamii.
Mtangazaji
wa Wapo FM,Dada Benedict Mrema akichombeza hapa na pale,huku muasisi wa
kipindi cha Weekend Special,Antony Joseph akitaka kuwalisha wageni
waalikwa keki iliondaliwa maalum kwa maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi
hicho tangu kuanzishwa kwake.
Keki ikigaiwa kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo.
Mmoja wa wasanii kutoka Taasisi ya Maendele ya Vijana (UVIKIUTA) akiwaburudisha wageni waalikwa
Mmoja
wa vijana wajasiliamali akifafanua kuhusiana na matatizo mbalimbali
wanavyokumbana nayo katika shughuli zao mbalimbali za kila siku za
ujasiliamali.
Mtangazaji
wa Wapo FM redip,Dada Ritha Chaula akisoma hotuba fupi kuhusiana na
maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special,mbele ya meza kuu
na wageni waalikwa mbalimbali waliofika.kipindi hicho hurushwa kila siku
ya jumamosi kuanzia saa 8 mchana mpaka 11.30 jioni kikiwa na lengo la
kuelimisha,na kuipasha jamii maovu yanayotendeka,namna ya kukabiliana
nayo na kuyaepuka,sambamba na hayo kipindi hicho pia huibua na kutangaza
matukio ya unyanyapaa,unyanyasaji wa kijinsia,ubakaji na ulawiti,kuwapa
vijana elimu ya stadi ya maisha ili waweze kujitambu,kujiamini na
kujiajiri katika kuyakabili maisha kiuchumi,kuibua migogoro ya
ndoa,kupata elimu ya namna ya kutatua na kupata suluhisho la kudumu.
Wadau wakifautilia kongamano wakati likiendelea.
Baadhi
ya Watangazaji wa Wapo Fm redio wakifuatilia mambo mbalimbali
yaliyokuwa yakijiri ndani ya ukumbi,wakati kongamano la vijana
likiendelea.Sho ni DadaRitha Chiwalo,Benedict Mrema na mdau wa Wapo FM.
Pichani
kulia ni Dada Faines Mwakatobe kutoka Chuo Kikuu Huria cha jijini Dar
akiwatafsiria baadhi ya Walemavu wa kutosikia,ambao pia wameshiriki
katika Maadhimisho ya miaka mitano (5) ya kipindi cha Weekend Special
kinachorushwa na redio Wapo FM, kila siku ya jumamosi.Maadhimisho hayo
yalikwenda sambamba na kongamano la vijana ambalo lilijadili changamoto
mbalimbali zinazowakumba vijana katika nyanja mbalimbali kama vile
uchumi,ajira,elimu na mambo mengineyo.
Baadhi
ya wadau wa kipindi cha Njia Panda cha Clouds FM ambao pia wameshiriki
katika Maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special
kinachorushwa na redio Wapo FM cha jijini Dar, kila siku ya jumamosi.
Wageni
waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini mijadala iliyokuwa
ikitolewa kwenye maadhimisho hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa.
Waimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili kutoka kundi la Double E likitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Mtangazaji
wa kipindi cha Wikend Special kinachorushwa na redio ya Wapo FM,
ambacho leo kinaadhimisha miaka 5 tangu kuanzishwa kwake, Bw. Antony
(kulia), akiwatambulisha viongozi wa vikundi mbalimbali mbele ya wageni
waalikwa (hawapo pichani) waliofika kwenye maadhimisho hayo
yaliyofanyika leo kwenye viunga vya UVIKIUTA-Chamazi jijini.
Mwakilishi
kutoka TYC, Bw. Nyakia Ally akizungumza machache mbele ya wageni
waalikwa (ambao kwa asilimia kubwa ni vijana kutoka sehemu mbalimbali
waliofika kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Special Wikend
kinachorushwa na redio ya Wapo FM, anayefuata ni Wakili wa Kujitegemea
Bw. Emanuel Makene, Dr. Nassoro Ally Matuzya kutoka hospitali ya
Mwanyanyamala, Mmoja wa wakilishi kutoka chuo kikuu UDSM, Bw. Edward Daniel na shoto ni Mwendesha kipindi cha Wikend Special Bw.Antony Joseph.
Kongamano likiendelea kwa umakini kabisa.
Mmoja wa wanaharakati vijana,Dr Nassoro
Ally Matuzya kutoka hospitali ya Mwanyanyamala akifafanua jambo ikiwa
ni sehemu ya kongamano la vijana la kuelimishana kuhusiana na mambo
mbalimbali zikiwemo changamoto wanazokabiliana/kumbana nazo katika mfumo
mzima wa maisha yao ya kila siku.
Mwimbaji
wa nyimbo za Injili,Pius Senyagwa sambamba na wasanii wengine
wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofana
kwa kiasi kikubwa.
Makofi ya hapa na pale yalikuwepo kutoka kwa wageni waalikwa.
Baadhi
ya vijana walioko kwenye Taasisi ya Maendeleo ya Vijana
(UVIKIUTA),kutoka Mataifa mbalimbali wakifuatilia mijadala mbalimbali
iliokuwa ikizungumzwa kwenye kongamano lililoendana sambamba na
maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special kinachorushwa na
redio ya Wapo FM,jijini Dar,maadhimisho hayo yamefanyika kwenye viunga
vya taasisi hiyo huko Chamazi-Mbagala jijini Dar.
No comments:
Post a Comment