Dar es salaam 12 Disemba 2012.
Kampeni iliyoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
kuchangisha fedha kupitia Red Alert na m-pesa imewezesha kupatikana kwa
shilingi 11,607,470/=
Kampeni
hiyo iliyodumu kwa wiki tatu kuanzia Disemba 22 mwaka jana hadi Januari
10, 2011 imewezesha kupatikana fedha hizo zilizochanganywa na wateja
kuunga mkono juhudi za Vodacom za kusaidia waathirika wa maafa.
Kampuni
ya Vodacom ilitangaza kuwashwa kwa nambari ya Red Alert na kuweka
nambari maalum ya kuchangia kwa m-pesa saa chache baada ya kutolewa
taarifa rasmi za kuwepo kwa athari kubwa za mvua zilizonyesha kwa siku
tatu mfululizo Dar es salaam.
“Kila
mtu alikuwa na nafasi ya kusaidia kuokoa na kusitiri maisha ya wenzetu
waliothiriwa na ndio maana tukawasha nambari ya Red Alert na kuruhusu
uchangiaji kupitia m-pesa” Amesema Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa
Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba.
Nambari
ya Red Alert hutumika na Vodacom wakati wa maafa kuwezesha wateja
kuchangia fedha kusaidia waathirika na hakuna makato yanayofanywa katika
ujumbe mfupi unaotumwa katika nambari hii ili kiwango kinachopatikana
kiwanufaishe waathirika moja kwa moja.
Maafa
yaliyotokana na mvua kubwa zilizoonyesha sehemu mbalimbali nchini
ikiwemo Dar es salaam Disemba mwaka jana yaligharimu maisha ya watu huku
maelfu ya familia yakiachwa bila makazi.
“Ni
jambo la faraja kwamba tumeweza kusimama kama familia moja ya
Vodacom.Wafanyakazi, wateja wetu na wadau na kuonesha upendo wetu wa
dhati dhidi ya wenzetu waliopatwa na maafa hayo”. Aliongeza Mwamvita.
Kampuni
ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii – Vodacom
Foundation inaandaa utaratibu wa michango hiyo kuwanufaisha walengwa
kama ilivyokusudiwa.
Awali
Vodacom Tanzania ilichangia vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi
milioni thelathini vikiwemo vyakula, magodoro na mablanketi kwa
waathirika wa maafa ya Dar es salaam waliokuwa wakiishi katika kambi
maalum kwa wakati huo.
Ujumbe
mmoja wa maneno kwenda nambari ya Red Alert 15599 uligharimu Tzs 500/-,
na kwenda m-pesa nambari 155990 uligharamu Tzs. 1,000/- na kwamba
hakukuwepo na ukomo wa kutuma ujumbe na kuchangia.
No comments:
Post a Comment