· Yashusha Gharama za m-pesa kwa 75%
· Kiwango cha kuongeza salio kwa m-pesa nacho chaongezwa hadi 25%
Kampuni
ya huduma za simu za mkononi inayoongoza nchini leo imetangaza kwa
mpigo kwa wateja wake nchini jumla ya ofa 4 zitakazowafanya kuzidi
kufaidika, kuwezeshwa na kufurahia zaidi huduma za Vodacom m-pesa.
Wateja
wa m-pesa sasa wamepunguziwa gharama za kufanya miamala kupitia huduma
hiyo ambapo sasa kila muamala utagharimu Shilingi 50 ikiwa ni punguzo la
asilimia 75. Wakati huo huo Vodacom ikiongeza kiwango ambacho mteja
anaweza kununua muda wa maongezi kupitia huduma hiyo ya m-pesa hadi
asilimia 25 kutoka asilimia 10 ya sasa.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw.
Rene Meza amesema”Tunatambua ni kwa kiwango gani huduma ya m-pesa
imekuwa ya umuhimu kwa maisha ya kila siku ya Watanzania, hivyo ni jambo
la muhimu pia kwetu kuwapatia ofa zinazoakisi matumizi yao na kuyafanya
kuwa rahisi na nafuu zaidi.” “Hii ndio dira yetu kwa mwaka huu na
kuendelea” Alisema Bw. Meza.
Ofa
nyengine iliyotangazwa na kampuni ya Vodacom Tanzania ni inayomwezesha
mteja wa m-pesa sasa kuweza kutuma kiasi cha chini zaidi cha fedha cha
shilingi 500 kupitia simu yake ya mkononi. Bw. Meza ameielezea ofa hii
kuwa inalenga kuhakikisha kila Mtanzania bila kujali hali yake ya
kiuchumi anafaidika na huduma bora,salama, ya uhakika na kuaminika ya
m-pesa.
Aidha,
pamoja na ofa hizo, kampuni ya Vodacom imezindua pia promotion ya
m-pesa ambapo jumla ya Shilingi 480 Milioni zitashindaniwa na wateja
kadri ambavyo wanavyotumia huduma ya m-pesa.
Katika
promosheni hii wateja 100 watakuwa wakijishindia zawadi ya fedha
taslimu za kitita cha Shilingi 50,000 kwa kila mshindi kupitia droo
zitakazochezeshwa kila siku huku droo kuu ya kila mwezi kwa miezi mitatu
ikitoa mshindi wa Shilingi 10 Milioni. Promosheni hiyo itadumu kwa siku
tisini kuanzia Februari 13, mwaka huu.
“Dhamira
yetu ni ya dhati kuhakikisha wateja wetu wanakuwa na furaha wakati wote
na huku tukiwawezesha kadri wanayotumia huduma ya MPESA. Tutaendelea
kuboresha mfumo wa m-pesa sambamba na huduma zinazopatikana katika MPESA
ili izidi kuendana na mahitaji halisi ya maisha ya kila siku ya
wateja.” Alisema Bw. Meza.
Kupitia
huduma ya m-pesa mteja anaweza kufanya malipo kwa huduma mbalimbali za
kijamii ikiwemo kununua umeme – LUKU, kulipia DAWASCO na DSTV. Aidha
huduma ya m-pesa inaweza pia kutumika kulipia tiketi za usafiri wa ndani
wa anga kwa mashirika ya ndege ikiwemo Precision Air na Coastal Air,
kulipia ada za shule, kuweka na kutoa fedha katika akaunti ya benki ya
CRDB na huduma nyengine nyingi.
Hakuna
shaka huduma ya Vodacom m-pesa ndiyo huduma ya kibenki kupitia simu za
mkononi inayoongoza nchini ikiwa na mtandao mpana wa mawakala zaidi ya
18,000 walionena nchi nzima mijini na vijijini na inayokua kwa kasi.
Ubora na umashauri wa huduma hii unaifanya kampuni ya Vodacom kuzidi
kung’ara na kuongoza soko la huduma za simu za mkononi nchini.
No comments:
Post a Comment