Mshauri
wa Huduma Umoja wa Mataifa nchini Bw.George Otoo akifanya Presentantion
juu ya ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mawasiliano kwa
Maafisa Mawasiliano na Uhusiano waliohudhuria mafunzo hayo.
Bw.
Owaiss Parray kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) akifafanua Mipango
ya kazi na njia za utekelezaji wake na jinsi zinavyohusiana na masuala
ya mawasiliano.
Bw.
Yusuph Al Amin kutoka Umoja wa Mataifa nchini akichambua vipengele
vinavyohusiana na jinsi mawasiliano zinavyoweza kuchangia maendeleo.
Mtaalam
wa masuala ya Teknolojia ya Habari Bw. Ayub Rioba akitoa somo kuhusiana
na mipango na mikakati ya Serikali ya Mawasiliano ambapo pia
alizungumzia juu ya umuhimu wa kufata maadili wakati wa kufanya
mawasiliano katika semina ya mafunzo ya siku moja kwa Maafisa
Mawasiliano wa Idara mbalimbali za Serikali.
Kaimu
wa Mwakilishi Mkazi Dkt. Julitta Onabanjo akisoma hotuba wakati wa
ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Uhusiano wa Wizara mbalimbali
nchini iliyoandaliwa na United Nations Communications Group kupitia
Ofisi ya Rais iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
:Mkurugenzi
wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nchini Tanzania Bw. Salva
Rweyemamu akitoa nasaha na shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuandaa
mafunzo hayo ambayo amesema ni muhimu kwa ajili ya kuongeza ufahamu kwa
maafisa mawasiliano na Uhusiano wa Idara na Taasisi mbalimbali za
Serikali.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Na. Mwandishi wetu
Umoja wa Mataifa umesema Tanzania ni mshirika wake wa karibu
katika jitihada za kukuza na kuendeleza sekta ya mawasiliano ambayo ndio kiungo
muhimu katika kutimiza majukumu ya kila siku ya idara na taasisi mbali mbali za
serikali na hata binafsi.
Akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou, wakati wa warsha ya siku moja ya mafunzo kwa
maafisa uhusiano wa wizara na taasisi za kiserikali ilifanyika leo jijini Dar es
Salaam, Kaimu wa Mwakilishi Mkazi Dkt. Julitta Onabanjo amesema UN inaitambua
Tanzania kama nchi mfano wa kuigwa na itakayonufaika kwa kufuata mikakati ya
kutimiza malengo.
Aidha amepongeza namna ushirikiano baina ya UN na Tanzania
unavyokwenda haswa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya mashirika tofauti ya
Umoja huo na jinsi fedha za misaada zinavyotumika.
Naye Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nchini
Tanzania Bw. Salva Rweyemamu amesema mafunzo hayo yamefanyika wakati muafaka
ambapo taifa linakabiliwa na changamoto mbali mbali katika sekta nyeti ya
mawasiliano.
Amefafanua kuwa mawasiliano ni nyanja muhimu katika utawala
na uongozi wa nchi na pia katika kuimarisha uhusiano wa kimatifa na nchi
nyinginezo.
Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na United Nations
communication Group kwa kupitia Ofisi ya Rais na kuwashirikisha maafisa
uhusiano na maafisa mawasiliano kutoka Wizara, Idara na Taasisi kadhaa za
serikali.
No comments:
Post a Comment