Kuanzia leo, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa
kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina
yake.Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au
host wake ni mwanadada Mboni Masimba.
The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi,Saa 3
Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7
Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi
ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia
kwa muda wa takribani saa 1. Yote hayo ni kupitia kituo cha
televisheni cha EATV(East Africa Television).
Lakini Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa
na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika
stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na
mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu;
BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?
MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?
BC: Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami
mazungumzo haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni.
Lina maana gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita
Mboni?
MM: Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni
Mboni…ile mboni ya Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya
jicho yako. Ukifanya hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha
kuangaliwa sana kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia
kwamba waliamua kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana
hiyo nina thamani kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni
mtoto wa mwisho kwa mama yangu… Ha ha ha haaaaa
No comments:
Post a Comment