Thursday, June 14, 2012

WAFANYAKAZI WA MASHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA (UN) WASHIRIKI ZOEZI LA KUCHANGIA DAMU.

Mshauri Mkuu wa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Christopher  John Ozga (kushoto) akiwa katika zoezi la kuchangia damu ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya uchangiaji damu duniani. Aliyesimama ni Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Bw. Deochris Kaimukilwa.
Mshauri Mkuu wa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Christopher  John Ozga akifanyiwa vipimo na  Bw. Deochris Kaimukilwa baada ya kujitolea damu.
Wafanyakazi wa Shiirika la Afya Duniani (WHO) wakionyesha ushujaa katika uchangiaji damu. Kutoka kushoto ni Richard Banda, Bw. Christopher John Ozga na Hashim Mahige.
Charles Lutandula wa WHO akifanyiwa vipimo vya awali na Mtaalamu kutoka mpango wa Taifa wa Damu Salama Bi. Edith Senga kabla ya kuchangia damu.
Charles Lutandula wa (WHO) katika zoezi la uchangiaji damu.
Mtangazaji wa Radio France International (RFI Kiswahili) Emmanuel Makundi akifanya mahojiano na  Bw. Hashim Mahige wakati wa zoezi kuchangia damu lililofanyika katika Ofisi za shirika la Afya Duniani (WHO) jijini Dar es Salaam ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya uchangiaji damu duniani.
Ramadhani Ndimba kutoka NASP .

No comments: