Ukiamua kubishana,tunaweza kufanya hivyo. Lakini endapo mwisho wa
ubishi huo tutaamua kukubaliana,basi sina shaka kwamba sote
tutakubaliana kwamba; miongoni mwa mitandao inayotembelewa na yenye
ushawishi mkubwa na wa aina yake miongoni mwa watanzania wengi,mtandao
wa Jamii Forums au kwa kifupi JF hauwezi kukosa katika orodha hiyo.
Lakini tofauti na mitandao mingine ambayo kimsingi imekuwa
ikiendeshwa na mtu au watu wachache tu, JF ni mtandao unaondeshwa na
watu wengi.Wengi wakiwa watanzania wenyewe. Pengine hiki ndicho
kinachoufanya mtandao wa Jamii Forums kuwa na “upekee” kama nilivyogusia
hapo juu.
Uendeshwaji huu wa jumla unafanyika kwa uhuru wa kila mtu kujiunga na
kuanzisha mjadala,kuchangia au kuupanua zaidi. Kimsingi,hivyo ndivyo
mtandao wa Jamii Forums unavyochanja mbuga hivi leo. Wewe na mimi sote tunaweza kujiunga na kuendeleza mijadala. Ndani ya Jamii Forums
kuna watu wa kila aina.Kuna watanzania.Kuna
viongozi/wanasiasa,wanataaluma mbalimbali na pia kuna wenzangu na
mie,watu wa kawaida wenye mapenzi na tekinolojia,habari,maarifa na wenye
kutafuta mahali pa kutolea maoni yao huku wakiwa na imani kubwa kwamba
kuna mtu atasoma ,kusikia na kuyafanyia kazi.
Ulianzaje? Nini malengo yake?Ni kweli kwamba mtandao huu unamilikiwa na chama fulani cha kisiasa? Mtandao huu una malengo gani?
Ili kupata majibu kwa maswali lukuki niliyokuwa nayo(na bila shaka uliyonayo wewe msomaji) nilimtafuta Maxence Melo Mubyazi(pichani), ambaye ni mwanzilishi-mwenza wa Jamii Forums
na mtu ambaye mpaka hivi leo anabakia kuwa mhimili wa Jamii Forums ili
kupata baadhi ya majibu kwa maswali yangu. Haya hapa ni mahojiano yangu
naye;
BC: Kawaida mtu anapoanzisha kitu cha mtandaoni huwa ana
malengo fulani ingawa inaweza ikatokea kwamba hapo baadae malengo
yakabadilika au kujinyambulisha kidogo ili kwenda na wakati na hali
halisi. Kwa upande wenu, mlikuwa na malengo gani kimsingi mlipoanzisha
Jamii Forums? Je, bado malengo ni yale yale au yamebadilika?
MM: Malengo yetu tangu mwanzo ni yale yale na
hayajabadilika na wala hatudhanii yatabadilika karibuni; kutoa uhuru wa
kujieleza kwa njia mbadala.
Read more: - BongoCelebrity
No comments:
Post a Comment