Mbunge
wa jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Gullam Dewji akihimiza kilimo
cha Choroko, Dengu na Mbaazi kwa wakazi wa kitongoji cha Mtisi kata ya
Mtamaa. Mbunge huyo ambaye alikuwa kwenye ziara ya kikazi jimboni kwake
ambapo pamoja na mambo mengine,alisema mazao hayo yatawakomboa wapiga
kura wake kiuchumi.(Picha na Nathaniel Limu).
Na.Mwandishi wetu
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini (CCM) Mh. Mohamed Gullam Dewji anatarajia
kutumia zaidi ya shilingi 250 milioni kugharamia mradi wa kilimo cha
choroko, dengu na mbaazi katika msimu ujao wa ujao.
Mh.
Dewji ambaye pia ni MNEC wa mkoa wa Singida, amesema hayo wakati
akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji cha kitongoji
cha Mtisi, kijiji cha Mtamaa.
Amesema
fedha hizo zitatumika kununua tani 60 za mbegu hizo, kutoa mafunzo ya
kilimo bora na ununuzi wa plau za kukokotwa na ng’ombe.
Amesema lengo la mradi huo ni kuwajengea mazingira mazuri wakulima wa jimbo lake, kuboresha hali zao za kiuchumi.
“Mimi,
madiwani pamoja na watendaji, tutawahamasisha wakulima kila kaya ilime
ekari moja ya mazao hayo ya mbaazi, dengu na choroko. Mazao hayo yana
soko la uhakika na bei zake zipo juu zaidi ya zao la mahindi” amesema na
kuongeza;
“Mimi binafsi nitanunua mazao hayo kwa bei ambayo itakuwa na faida kubwa kwa mkulima wa mazao hayo”.
Kuhusu plau, amesema majembe hayo ya kukokotwa na ng’ombe kila kikundi cha wakulima 25, watapatiwa plau moja bure.
Katika
hatua nyingine, Mh. Dewji amesema mtaalam wa kilimo katika ofisi yake
kwa ushirikiano na wataalam wa manispaa, watasimamia mradi huo kwa
karibu, ili wakulima waweze kuzingatia ushauri wa kilimo bora.
“Lengo
ni kwamba mavuno katika ekari hiyo moja ya aidha, dengu, choroko au
mbaazi, yakidhi mahitaji ya kuweza kumkomboa mkulima kiuchumi”,amesema
kwa kujiamni.
Wakati
huo huo, mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wakulima kubadilika
na kuachana na kilimo cha mazoea na kuanza kulima kilimo
kinachozingatia ushauri wa taalamu.
Aidha,
amesema kutokana na misimu ya mvua za miaka hii kutokueleweka vizuri,
njia pekee ya kunufaika na kilimo, ni mkulima kuwahi kuandaa mashamba na
mbegu bora kabla msimu haujaanza.
No comments:
Post a Comment