Monday, July 2, 2012

Fwd: MASHABIKI WA TIMU YA MANCHESTER UNITED WAIBUKA MABINGWA WA SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA JIJINI MBEYA

Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Jonathan Maselea akikabidhi zawadi ya kreti la bia kwa nahodha wa timu ya mashabiki wa Manchester United ya Uingereza mara baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa shindano la Serengeti Fiesta  Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Uhasibu jijini Mbeya TIA, ambapo washindi hao wameondoka pia na shilingi laki 500.000, huku mshindi wa pili timu ya Barcelona wameibuka na shilingi laki 300,000.
Meneja Msoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Kanda ya Kusini Jonathan Maselle akimsikiliza Mkuu wa mauzo kanda ya kusini na Nchi Jirani Freddy Richard akizungumza mara baada ya timu hizo kukabidhiwa zawadi zao.
Mratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza Shafii Dauda akizungumza mara bada ya kumalizika kwa bonanza hilo kutoka kulia ni Jonathan Maselle Meneja masoko wa Serengeti Kanda ya nyanda za juu Kusini, Mkuu wa Mauzo kanda ya kusini na nchi njirani Freddy Richard na kutoka kulia ni kapteni wa timu ya mashabiki wa Machester United Willy Maisara na Kapteni wa timu ya Barcelona Zefania Bitwale
Mmoja wa wachezaji wa mashabiki wa timu ya Manchester United akiwa amebebwa juujuu na mashabiki wake mara baada ya timu yao kuibuka mabingwa wa tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza mkoani Mbeya.
Wadau wa mkoani Mbeya wakishoo love mbele ya kamera ya Fullshangwe.
Kutoka kulia ni Mkuu wa mauzo Kanda ya Kusini na nchi Jirani wa kampuni ya bia ya Serengeti Freddy Richaer, Alex Lwambano kutoka Clouds, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi tamasha la Serengeti Fiesta Sebastian Maganga, Mtangazaji wa Clouds Antu Mandoza na Mratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza Bw. Shafii Dauda wakishoo Love/
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa Manchester United na Barcelona wakichuana vikali katika mchezo wa fainali ya bonanza hilo.
Mchezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Manchester United akiukokota mpira wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya timu ya mashabiki wa Barcelona kwenye viwanja vya TIA jijini Mbeya leo.
Mashabiki wa Manchester United wakishangilia kwa nguvu mara baada ya timu ya kutinga fainali ya bonanza hilo.
kutoka kulia ni Freddy Richard wa SBL Mbeya, Alex Lwambano, Sebastian Maganga na Jonathan Maselle SBL Mbeya wakifuatilia jambo katika tamasha hilo.
Mashabiki wa tamasha la serengeti Fiesta Soccer Bonanza wakifuatilia matukio mbalimbali katika tamasha hilo.
Akiana Meku wanapokutana ni kupanga dili ya hela tu hebu wacheki akina Meku hawa wanapanga dili za hela au wanafurahia maisha.
Mashabiki wa Bonaza hilo wakiwa wamefurika katika viwanja vya TIA jijini Mbeya.
Mtangazaji wa Clouds na mratibu wa tamasha la serengeti Fiesta Soccer Bonanza akimhoji mmoja wa mashabiki wa timu ya Iner Milan ya Italia mabayo mwaka huu haikushiriki katika bonanza hilo.

No comments: