Ally Choki (kushoto) akimtambulisha 'Kimobiteli' kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Wanamuziki wa Extra Bongo wakimsikiliza Kimobiteli kwa makini.
Picha ya pamoja ya waimbaji na wanenguaji wa Extra Bongo..
BENDI ya muziki wa dansi, Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, leo wamemtambulisha mwanamuziki mpya ambaye aliwahi kuwa katika bendi hiyo zamani na sasa ametokea bendi ya Twanga Pepeta -- Khadija Mnoga ‘Kimobiteli’.Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa White House uliopo Kimara jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki, alisema mwimbaji huyo ameamua kurudi kundini, hivyo kuanzia sasa amekuwa ni mwanamuziki wao na tayari ameshaanza kazi na utambulisho rasmi utafanyika wiki ijayo.
HABARI/PICHA: GLADNESS MALLYA
No comments:
Post a Comment