Ndugu zangu,
Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog hatunaye tena.
Nimemfahamu Daud Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo, amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli za kijamii kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ni kwa kupiga picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.
Mara
nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake ( Picha ya kwanza juu) akichapa
kazi na huku mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa
mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye
teknolojia ya habari na mawasiliano.
Najua
Daud Mwangosi alikuwa na malengo ya kuendeleza shughuli zake za
ujasiriamali. Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya
kumwongezea kipato ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya
kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote
ni katika kumwongezea kipato kutunza familia yake.
Leo
Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha familia, mjane na watoto wanne;
Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali
Sekondari, Hetzgovina Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria
Mwangosi ( 2)
Namini Daud Mwangosi angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.
Jana
na leo nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko
Tukuyu. Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na
msiba wa Mwangosi na wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata
mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana
kusikia habari hizo.
Kwa
vile tayari ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji
kwa sasa ni kupata photocopy machine ( Used) na kodi ya pango la
ofisi. Jumla yake kwa yote hayo mawili haitazidi shilingi za Kitanzania
milioni mbili na laki mbili. Hivyo msaada anaouomba kwa wenye mapenzi
mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi milioni mbili na laki mbili).
Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.
Kutokana
na hali aliyo nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la
kuratibu michango hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili
tumsitiri mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi.
Napendekeza
ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi hili
kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni msaada
mkubwa.
Mjengwablog
bado tuna rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia wenye kuhitaji.
Itakumbukwa, huko nyuma, kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango
ile ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi
ya shilingi milioni mbili.
Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.
Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.
Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.
Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.
Namna
ya kuwasilisha michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au
NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa
walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid
Mjengwa)
Natanguliza Shukrani.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.com
http://mjengwablog.com
No comments:
Post a Comment