Saturday, June 9, 2012

AFRICAMAGIC ENTERTAINMENT LAUNCHES CHIC DAILY SHOWBIZ PROGRAMME - STAR GIST!

Africa Magic Entertainment is launching STAR GIST, the continent’s very own answer to showbiz buzz, up-to-the-minute entertainment and trend news. This glamorous new show, with equally hip presenters, 25-year-old Vimbai Mutinhiri who hails from Zimbabwe and South African Lawrence Maleka, 22. STAR GIST is all about giving viewers exclusive star profiles, BTS (behind-the-scenes), features, and continental and international headlines – on the daily. Think: red carpet glam, inside info and unprecedented access into the world of African and international celebrity royalty.

Don’t feel left out because you can also join the STAR GIST viewer paparazzi by uploading content onto the site. For news and information on STAR GIST, log onto www.africamagic.tv. Don’t miss the first episode of STAR GIST on Monday 11 June at 19:30 CAT on AfricaMagic Entertainment (DStv
Channel 129). Continues every weekday at 19:30 CAT.

Friday, June 8, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI FURSA YA WASANII WA TANZANIA KUSHINDA EURO 5,000 KATIKA SHINDANO LA KUTUNGA WIMBO RASMI WA KUNDI LA MATAIFA YA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP GROUP OF STATES)


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo limepokea mwaliko wa Wasanii wa Tanzania kujitokeza kushiriki shindano la kutunga wimbo utakaokuwa unatumiwa kama wimbo rasmi wa mataifa ya Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP Group of States).

Shindano hili ambalo litahusisha mataifa 79 wanachama wa umoja huu limeandaliwa na Sekretarieti ya ACP kwa lengo la kupata wimbo ambao utabeba dhana ya mataifa ya Afrika, Karibiani na Pasifiki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya ACP, shindano hili linamhusu msanii mmoja-mmoja au Kikundi cha wasanii ambao watapaswa kutunga wimbo huo kwa kuzingatia lengo kuu la umoja huo ambalo ni Maendeleo Endelevu na Upunguzaji Umaskini sambamba na Ushawishi mkubwa kwenye Uchumi wa Dunia.

Aidha, wimbo huo utatakiwa uwe wenye kujenga moyo, fikra na kutangaza malengo ya kundi hili la mataifa ya Afrika, Pasifiki na Karibiani.

BASATA inatoa wito kwa wasanii wa Tanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano hili kwani ni heshima na fursa pekee tumepewa kama taifa kuonesha vipaji na uwezo wetu kimataifa katika eneo la utunzi wa nyimbo.

Ni wazi kuwa, kujitokeza kwa wasanii wetu wengi kushiriki katika shindano hili si tu kutaonesha utayari wa sisi kama taifa katika kushindana na mataifa mengine wanachama bali utakuwa ni mwanya wa kuitangaza Sanaa yetu ya muziki nje ya mipaka yetu.
Ikumbukwe kuwa, ushindi wa Msanii kutoka Tanzania kwenye shindano hili kutamjengea heshima msanii husika na taifa kwa ujumla.
Maelekezo kuhusu Wimbo utakaotungwa
•    Tungo zote lazima ziandikwe katika moja ya lugha rasmi za ACP ambazo ni Kiingereza, Kifaransa, Kiispaniyola na Kireno.
•    Wimbo huo uliokamilika lazima uambatanishwe na tunzi (lyrics) zilizoandikwa na zitumwe katika mfumo wa MP3/DVD/WAV Format
•    Tungo ziguse maeneo yafuatayo
i)    Fikra ya umoja ambayo itaunganisha nchi wanachama wa ACP
ii)    Utajiri na tamaduni mbalimbali zilizo katika nchi wanachama wa ACP
iii)    Mataifa wanachama wa ACP na kuheshimu Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora.
iv)    Nchi wanachama wa ACP na msisitizo katika maendeleo yenye usawa pia kusimamia mikataba ya kimataifa ya Haki na Amani.
Jinsi ya Kushiriki
Nyimbo zilizotungwa kwa kufuata mwongozo huo wa ACP zitumwe kupitia anuani ifuatayo ;-
Josephine Latu-Sanft (Press Office)
Avenue Georges Henri
451,1200 Brussels, Belgium
E-mail : latu@acp.int.


Mwisho wa kutuma
Agosti 31, 2012

Imetolewa na;
Ghonche Materego
Katibu Mtendaji - BASATA

Thursday, June 7, 2012

Emirates offer special fares to its Tanzanian Customers

Dar-es-Salaam: June 7, 012: Emirates customers in Tanzania can now enjoy up to 20% off their airfares while travelling to a wide range of destinations across the Middle East, Asia, Europe and Americas, following the launch of a special fare campaign which runs until the end of June, 2012.

Emirates' special Economy Class fares to the Americas now start from US $1791 to Seattle in the United States and US $1669 to Sao Paulo, Brazil. The special fares offer also applies to Seoul from US $1857, Osaka from US $2267, Muscat from US $546, Frankfurt from US $916, Dusseldorf from US $896, Hamburg from US $889, and Munich from US $902.

Unveiling the new fares and stopover offer, Emirates Country Manager for Tanzania, Abdulaziz Al Hai said the offer was part of the airline’s mission to make travel as comfortable and affordable as possible for its Tanzanian customers this summer.

“As an airline we are committed this market and we shall continue to provide our customers in Tanzania outstanding value for money proposition as we offer the most attractive travel experience available. Our special fares to some of Emirates’ most popular destinations represent a very significant saving, meaning that there has never been a better time to book a holiday, business trip or to visit friends or relatives overseas,” said Al Hai.

He continued: “In addition to offering value for money, we continue to link Tanzania to its key markets across the world as we enable the country to continue to build on its historical and trade relations with some of its major trade partners like the Germany.”

The bilateral trade volume between Germany and Tanzania grew by 51 per cent to 294 million Euros in 2011, according to preliminary data from German Embassy in Dar-es- Salaam. The Tanzanian imports doubled to 161.5 million Euros in 2011, while the German
exports to Tanzania rose by 16 per cent to 132 million Euros. Tanzania is ranked 9th among the sub-Saharan countries trading with Germany.

The fares are valid for ticketing on or before June 30th 2012 for travel on or before August 15th 2012. All fares are quoted on a return basis, are inclusive of all taxes and can be purchased from Emirates sales offices or through authorized travel agents.

More information on the promotions, terms and conditions can be found by visiting the local Emirates sales office located at Haidery Plaza, 6th Floor Ali Hassan Mwinyi Road in Dar es
Salaam, or online at www.emirates.com

About Emirates
Emirates now fly to 124 destinations in 74 countries. The airline has a fleet of 174 aircraft
and is the world’s largest Airbus A380 and Boeing 777 operator. With an order for 50 new
Boeing 777-300ER aircraft placed at the Dubai Airshow, Emirates now has 230 aircraft on
order, worth over US$84 billion at list prices.

Operations on Emirates connect Tanzania to the world through the airline’s route network,
with extensive connections to Europe, the Americas, the Far East and Asia, Australia and
India Subcontinent.

Since its launch in 1985, Emirates airline has received more than 500 international awards
in recognition of its efforts to provide unsurpassed levels of customer service. For additional
information, please visit www.emirates.com

Mr Blu In Dubai - Post Event Video...

 
A day in Mr. Blu's time when he visited Dubai, in the United Arab Emirates, for a performance.

Clouds FM Dj Fatty Will be on One & two at BBA

FATUMA HASSAN AHMED / DJFETTY
PERSONAL PROFILE

 Mobile: 0713 33 33 43, 0757 33 33 43, 0777 77 77 66
Twitter: @fettythebest
Face book fan page: djfetty
Location: dare s salaam, Tanzania

 Famous as Dj Fetty, My name is Fatma Hassan born and raised in Tanzania, started deejaying in 2006 as an employee at Clouds Fm radio station in Dar-es-salaam on a very popular afternoon show (Dr Beat) by then, playing mostly hip hop, r&b, bongo fleva and a little bit of pop, while on the show I joined Clouds dj group (Nyuki dj’s) in a phenomena show at the time (Saturday night live) every Saturday, performing in different regions every weekends including Mwanza, Tanga and Dodoma it is this time I started gaining popularity becoming the only female best dj in Tanzania to date. Performed at the biggest yearly musical event (Fiesta) three years in a raw 2009 – 2011 as well as on MTV VJ search 2007 in Arusha. Still working with Clouds Fm Radio as dj, presenter (clouds top 20) and producer.

HELP FOR THE DISABLED


KCB TANZANIA YAZINDUA HUDUMA MPYA YA DISPORA BANKING....

Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania DK Edmund  Mndolwa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya KCB DIASPORA BANKING uliofanyika leo  Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akizindua rasmi huduma mpya inayotolewa na KCB DIASPORA BANKING, Katikati ni Mmoja wa Mameneja wa benki hiyo SHOSE KOMBE. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo MOEZ MIR.


Michuano Airtel Rising Stars yaanza Dar, Mbeya na Arusha



 Mchezaji Tyson Lyoka (kushoto) wa timu ya soka ya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa akichuana vikali na Goodluck Mabiki (kulia) wa shule ya Msongola katika moja ya mechi za ufunguzi wa michuano ya 'Airtel Rising Stars', uliofanyika katika uwanja wa Airwing. Msongola ilishinda 4-0. (picha na mpiga picha wetu)

Michuano ya vijana ya wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2012 imeanza rasmi jana ngazi ya mkoa kwa shule ya Sekondari ya Msogola kuisambaratisha bila huruma shule ya Benjamin Mkapa 4-0 kwenye mchezo uliocheza kwenye uwanja wa shule ya Airwing, jijini Dar es Salaam.

Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa ni ufunguzi kwa mkoa wa kisoka wa Ilala, magoli ya Msogola yalifungwa na Dickson Alphonce dakika 62, Abdul Saidi 67, Hanica Seleman 86 na Goodluck Mabiki akapigia msumari wa mwisho dakika ya 87.

Kwa Mkoa wa kisoka wa Temeke, shule ya sekondari ya Tirav ilitoka sare ya 2-2 na shule ys Kurasini, mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Twalipo na kufuta mamai ya mashabiki huku wengi wao wakiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kurasini. Mchezo huo ulianza taratibu huku kila timu ikitaka kusoma mbinu za mwenzake na kuongeza kasi ya mchezo kadri muda ulivyokuwa unasonga
Shule ya Tirav ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao, ambalo lilipatikana kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya sita ya mchezo baada ya kipa wa Kurasini kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Tirav Paul Balama kwenye eneo la hatari. Paul Balama ndio alifunga penati hiyo huku akimwacha golikipa wa Kurasini akiwa hana la kufanya.

Baada ya goli hilo, Kurasini ilifanya mashambulizi mfululizo na kwenye dakika la nane, Justin Macha aliizawazishia timu yake baada ya kazi nzuri kati yake na Awadh Mtawamba na Muhalami Ally. Goli hilo iliamsha shangwe na vishindo kwa mashabiki wa shule ya Kurasini huku wengi wakiwemo wanafunzi wenzao.

Shule ya Tirav ilipata goli ya pili kupitia kwa Paul Balama ambaye alikuwa ni mwiba mkali kwa ngome ya Kurasini kwenye dakika ya 19 huku Kurasini wakizawashisha kwenye dakika ya 85 na kufanya uwanja wote kulipuka kwa shangwe na nderemo.

Kwenye mechi nyingine ya ufunguzi kwenye mkoa wa Kinondoni, Shule ye sekondari ya Twiga iliifunga shule ya Mpiji Magohe 1-0 huku goli la kipekee likiwekwa kimiani na Louis Andrew kwenye dakika la 35 la mchezo.

In Mbeya, Mbeya Day Secondary had a bright day on Tuesday when they thumped  Wenda Secondary 2-0 in a match that was played at Sokoine Stadium while in Arusha, Kaloleni Secondary reduced Sinoni secondary school to novices by humiliating them 5-0 in a one-sided match.

Mkoani Mbeya, Shule ya sekondari ya Mbeya Day ilikuwa na kila sababu ya kufurahi baada ya kuichapa Wenda Sekondari 2-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, huku katika mkoa wa Arusha, shule ya Kaloleni ikiisambaratisha bila huruma Sinoni Sekondari kwa 5-0.

BONDIA JAPHET KASEBA AZUNGUMZA NA MO BLOG KUHUSU 'FREEMASON'.

 MO BLOG: Kaseba kuna ukweli wowote kwamba kabla ya kucheza pambano ni vyema siku moja kabla mtu unapaswa kufanya mapenzi.?.

KASEBA: Kwa kweli kwa kuwa mimi nilianzia kwenye mchezo wa ‘Martial Arts’ , hicho kitu kilikuwa kinapingwa sana na sidhani hata katika michezo mingine kinakubalika. Sana sana ningewaasa watanzania kujituma katika mazoezi na kuacha kudanganyana.

MO BLOG: Hebu izungumzie familia yako kwa sababu mengi yamesemwa na hatupendi kuyarudia.

KASEBA: Nampenda sana mke wangu, nawapenda ndugu zangu, pia nawapenda sana wazazi wangu na siku zote namshukuru mwenyezi mungu na naamini hiyo ni moja wapo ya mafanikio yangu, kwa kuwa kila ninachohangaikia nahaingikia kwa sababu ya familia yanguKusoma mahojiano yote Bofya hapa

Wednesday, June 6, 2012

DIAMOND KUZINDUA MAGIC FM 101.7 MWANZA

Mpango mzima kutakuwa na usakaji vipaji Mwanza, Burudani kusanukishwa na Diamond Platnum & on the One + Two  Pro 24 Dj.
Video Habari.

Dj Tass wa Magic Fm na Pro 24 Djs ...mapemaaaa ndani ya Rock City
 D Mango ambaye ni mratibu wa Uzinduzi Magic Fm jijini Mwanza (aliyevaa miwani )akizungumzia uzinduzi huo mbele ya waandishi wa habari (walioketi kulia) huku Dj Tass toka Magic Fm na Pro 24 Djs (kushoto) akisikiliza kwa umakiini.

D Mango ambaye ni mratibu wa Uzinduzi huo jijini Mwanza akizungumzia uzinduzi huo mbele ya kamera ya blog hii.
Magic Fm Mwanza kuzinduliwa rasmi Ijumaa hii ya tarehe 8/06/2012 ndani ya Villa Park Mwanza. Shindanola kusaka vipaji kufanyika mshindi kurekodi Studio za Combination Sound chini ya Producer Man Walter aka Man Maji.
 Diamond Platnum kutoa burudani..
Ngoma zitaanza kugengeshwa kuanzia saa 2 usiku kiingilio ni shilingi 10,000/=

MBUNGE WA SINGIDA MJINI MH. ‘MO’ ATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH. MILIONI 6 KWA SHULE 20 ZA JIMBO KWAKE

Msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini na katibu mwenezi wa CCM manispaa ya Singida Bw. Hassan Mazala (kulia), akimkabidhi Afisa wa idara wa shule za sekondari jimbo la Singida mjini Bw. David Bulala jezi 300 zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji. Wa kwanza kushoto ni katibu muhtasi wa Mbunge.
Nathaniel Limu
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa vifaa vya michezo jezi jozi 300, zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sita kwa shule 20 za sekondari jimboni kwake.

Msaidizi wa mbunge huyo Bw. Hassan Mazala amesema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi jezi hizo, iliyofanyika kwenye ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Saidia Singida yetu iliyopo mjini Singida.

Amesema jezi hizo zilikuwa ni sehemu ya msaada ambao ulikuwa utumike kwenye ligi maalum ya kombe la 'Mo' ambayo shule zote za sekondari jimbo la Singida mjini zingeshiriki.

"Lakini baada ya ninyi kuandaa bajeti kubwa mno na wakati huo huo mbunge wetu Dewji akikabiliwa na majukumu makubwa ya kutekeleza ahadi zake nyingi, ligi hiyo tumeisitisha kwanza",amesema Mazala ambaye pia ni katibu mwenezi wa CCM manispaa ya Singida.

Amesema kwa sababu ligi hiyo tarajiwa maandalizi yake bado, sasa maamuzi ni kwamba jezi hizo zitumike katika maandalizi ya michezo ya shule za sekondari (UMISETA).

Akifafanua zaidi, Mazala amesema wanafunzi na vijana walio nje ya shule, wahamasishwe kupenda michezo ili pamoja na mambo mengine, waweze kujijengea mazingira mazuri ya kujiajiri na kuajiriwa.

Kwa upande wake Afisa elimu taalum shule za sekondari manispaa ya Singida Bw. David Bulala, alitumia fursa hiyo kumshukuru mbunge Dewji kwa kuipunguzia ofisi yake makali ya gharama ya ununuzi wa vifaa vya michezo.

YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBA YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013


Ndg. Waandishi wa Habari
Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadala ambavyo vilikuwa:

1.    Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%

2.    Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei

3.    Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).

4.     Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopo ya  elimu ya juu.

Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.

Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa  lakini Serikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.

Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa. Halikadhalika Kambi ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).
Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahiri kwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezaje kutekeleza Bajeti ya 15trillioni?
Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo na kuishinikiza Serikali kuyatekeleza.

1. Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa. Hivi sasa misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% ya Pato la Taifa.

2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.

3. Kuelekeza fedha za kutosha  kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.

4. Kuongeza wigo wa kutoza  tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3 itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto ya mikopo kwa wanafunzi.

5. Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.

6. Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani yanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidi kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi.

7. Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.

8. Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa bei.

9. Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa elimu kwa ubora zaidi, ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory authority)

10. Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchni hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.

Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa deni la Taifa amabalo limefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.

Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa kwenye  magari na posho mbalimbali na Kwamba  fedha nyingi zitumike kwa miradi  mikubwa ya maendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano

Asanteni sana!
…………………………….
Zuberi Kabwe Zitto(Mb)
Waziri Kivulu-Fedha na Uchumi.
.

A CANDID INTERVIEW WITH COMEDIAN EVANS BUKUKU

Just a couple of years ago, stand-up comedy were not very popular in Tanzania. In fact, it was almost non-existing. If it was, then it was done in very informal settings such as in the streets or local bars and not so much in prearranged settings whereby the audiences are well seated and eagerly waiting to be entertained and laugh to the point of shedding those tears of a good laugh. I am talking about the laugh that makes your entire body vibrate like a Samsung’s hand held gadget!

However, the above scenario of lack of organized stand-ups is changing or has changed. Thanks to one man who, according to his own words, he is almost on a “crusade” to change how and where we can go and have a good laugh. His name is Evans Bukuku.

He is now, by far, the new face or our own definition of Stand-Up comedy in Tanzania. He is best known for his once a month(every last Tuesday of the Month) smart and hilarious stand-up comedy routines  that features him making funny of almost everything in simple and  unique ways that makes everyone in the audience laugh hard (and I mean real hard).

He is also gifted with using a plethora of different voice impressions from the Jaluo, Sukuma, Chagga and you name it…all in the name of bringing real entertainment to his audience.

If you have never attended one of his events, mark your calendar. His next appearance is on Tuesday 26th June 2012 at Nyumbani Lounge which is located near Best Bite in Namanga area.

But before going to see him and even if you have seen him before and just can’t get tired of him, I thought we’d all like to know a bit more about him. I therefore tracked him down and he granted you (through me) this exclusive interview. Below are the excerpts;

Hi Evans! It feels great to have you on BC. Welcome. How is it going?

EB: Hey Jeff, thanks for having me. I’ve heard of your work and I am humbled to have this opportunity. I’m doing well (Thank God) but it’s still a rough road ahead. . .

BC: Since this is your first time on BC, I have to ask you this otherwise some of our own fans will be pissed. Where were you born and where did you grow up, schools you attended and anything you like to share with us about your history.

EB: I was born in Shinyanga, Tanzania; my father was in the mining business. I did pre-school there in Shinyanga, but at the age of four my dad was posted to London UK. I then studied there in South East England (really good schools) up until my O-levels, whereby my Dad was recalled to Tanzania. Then I studied in Iringa (really bad govt. school) and had the biggest cultural shock ever! (It just wore off last month!)

BC: Comedy is art. How has your life influenced your art? What influenced you to get into comedy? Is this what you wanted to do since childhood or you are one of those people who got themselves doing what they are doing by “accident”?

EB: Life hasn’t influenced my art, rather life IS my art, especially when it comes to Standup Comedy. All the anecdotes, jokes, observations and impromptu are just reflections of my life. My friends influenced me to get into comedy; at a young age (11yrs) I was told “you should be a comedian’ but I could never get enough courage to tell my dad (knowing African dads, that would be a short conversation) so ended up buffooning around friends, but having a different kind of persona when with family. I never got into comedy by accident, and ever since I officially signed up, my vision has never been clearer.

BC: How was your first experience as a stand-up comedian? Were you nervous? How did you prepare yourself for such an experience?

EB: My very first stand-up experience was in a church ;) . My aunt thought I could make a few people laugh, and I could do a good Onyango impression (Jaluo accent), so she ‘pushed’ me to standup and make people laugh. I tied a handkerchief on my hand then tried to make a joke about how I tried to wash my TV with soap and water. Precisely; it wasn’t funny, I mumbled a few things then went to sit down and forget about the whole episode . . .

Read more: A CANDID INTERVIEW WITH COMEDIAN EVANS BUKUKU - BongoCelebrity

MISS CHANG'OMBE 2012


UN YAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUTUNZA MAZINGIRA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Mratibu  wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD Bw. Ralf Ernst akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari yenye lengo la  kujenga ufahamu miongoni mwao katika kuelekea kufanyika mkutano wa Maendeleo endelevu Rio+20 utakaofanyika kuanzia Juni 20-22 nchini  Brazil kwa niaba  ya Mwenyekiti wa Kikundi cha Mazingira ambaye pia ndio Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bi.Louise  Chamberlain. Kulia ni Gertrude Lyatuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "THE FUTURE WE WANT".
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro akizungumza kuhusu umuhimu wa mkutano wa Rio+20 na maana yake katika kuipeleka dunia pale inapotaka kwenda. Katikati  ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi na kushoto ni Aifsa Mkuu wa Utafiti wa Masuala ya Mazingira katika Ofisi hiyo Dkt. Constantine Shayo.
Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo akimkaribisha Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi (hayupo pichani).
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akifafanua kuwa Tanzania kama mwanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi amesema Tanzania imeandaa  Rasimu ya Ripoti ya Rio+20 itakayojadiliwa na mkutano huo.
Bw. Muyungi alitumia fursa hiyo kuwakilisha mada kuhusiana na maendeleo endelevu ya Tanzania katika miaka 20 tangu mwaka wa kwanza kufanyika mkutano wa kwanza wa RIO iliyohusu "wapi tulipokuwa na wapi tulipo sasa". Bw. Muyungi ameongeza kusema kuwa Mkutano huu utaainisha hatua zitakazoangalia utekelezaji na kuhuisha nguzo zote tatu za maendeleo endelevu (mazingira Uchumi na Jamii) kwa kufuata  kanuni za usawa huku tukitambua  tofauti katika uwajibikaji na uwezo.
Upatikanaji wa njia mpya, za  ziada, thabiti, zinazotabirika za kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za usimamizi wa mazingira na maendeleo endelevu kwa nchi zinazoendelea.
Washiriki kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wakiwa katika warsha inayohusiana na mkutano wa Rio+20 iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa katika kusheherekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.

Monday, June 4, 2012

LAMECK DITTO: ALIPOTOKA,ALIPO NA ANAPOOTA KUFIKA(INTERVIEW)

Historia inaonyesha kwamba wanamuziki wengi hupitia vikwazo vingi mpaka kufikia mafanikio. Ni hali halisi ambayo bila shaka inaeleweka ukizingatia utitiri wa vijana wenye vipaji vya kuimba na hata kutunga au kuandika nyimbo. Wapo wengi.Katika sanaa ya muziki kuna kukataliwa, kuna kuambiwa huwezi, hujui kitu na huwezi kufika mbali.

Pamoja na ukweli huo, kuamua kuendelea au kukubaliana na “maoni” ya wadau na kuachana na muziki, kunategemea mambo kadhaa ikiwemo imani binafsi kama unaweza au huwezi. Ukiambiwa huwezi na wewe ukakubaliana na hoja hiyo,bila shaka utakuwa umefikia mwisho wa ndoto.Unaamka.

Lameck Ditto ni miongoni mwa wanamuziki ambao wamepitia vikwazo vingi mpaka kufikia hapo alipo hivi leo. Bila shaka tunakubaliana kwamba Ditto  ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye vipaji, nidhamu na juhudi za hali ya juu katika sanaa ya muziki.

Kufikia hapo alipo, alipitia mengi. Alistahimili mengi. Aliwahi kuambiwa hawezi. Aliwahi

Read more: - BongoCelebrity

Msanii Roma akikamua kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel

huduma ya Airtel yazinduliwa kwa kishindo mjini Morogoro

Burudani...
Wateja wa Airtel wakiwa na zawadi zao za simu aina ya Sumsung mara baada kununua moderm za Airtel zenye kasi ya 3.75G,shoto ni Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Morogoro,Aluta Kweka.


Msanii wa hip hop ROMA akighani jukwaani kuburudisha umati wa wakazi wa morogoro waliofurika uwanja wa shule ya msingi uwanja wa ndege
Msanii wakundi maarufu nchini la Tip top connection lenye makazi yake jijini dare s salaam Manzese, Madee akiimba jukwaani kuburudisha umati wa wakazi wa morogoro
Wasanii wa kundi la Mashujaa band wakiongozwa na raisi wa band hiyo (pichani kati) Charles Baba a.k.a Kingunge wakiwasha moto jukwaani
Sehemu ya umati wa wakazi wa morogoro uliofurika kwenye uwanja wa shule ya msingi uwanja wa ndege kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5
Mkazi wa Morogoro Sarafina Millak akikabidhiwa simu aina ya sumsung na Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Pwani,Aminata Keita mara baada ya kuibuka kinara wa kucheza ‘sebene’ la bendi ya Mashujaa,
Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Morogoro,Aluta Kweka akimkabidhi simu aina ya sumsung mmoja wa wateja wa Airtel,Mbesa Baraka