Thursday, January 16, 2014

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA MAREHEMU GEORGE LIUNDI KARIMJEE JIJINI DAR

Rais Jakaya Kikwete akiwasili Viwanja vya Karimjee kuaga mwili wa marehemu Jaji George Bakari Liundi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Bakari George Liundi likiwa mbele ya waombolezaji.
Rais Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (kulia) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wiliam Lukuvi (kushoto).
Wa kwanza kushoto (mbele) ni mke wa marehemu Jaji Liundi akiwa na wanafamilia wengine wakati wa kuaga.
Jeneza lenye mwili wa marehemu George Liundi.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa (katikati) akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) na Salim Ahmed Salim (kushoto) nao walikuwepo kuaga mwili wa Jaji Liundi.
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria kuaga mwili wa Jaji Liundi.
Ibada ya kumuombea marehemu.
Mtoto wa marehemu Taji Liundi akitoa shukrani za familia kwa waliohudhuria tukio hilo.
Mjukuu wa marehemu, akisoma wasifu wa George Liundi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wiliam Lukuvi akitoa salamu za rambirambi kutoka serikalini.
Rais Kikwete akitoa heshima kwa mwili wa marehemu Liundi.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal akiaga mwili.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiaga mwili wa marehemu.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akiaga mwili wa Liundi.
Mama Anna Mkapa akiaga mwili wa marehemu.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiaga mwili.
Waombolezaji wakielekea kuaga mwili wa marehemu Liundi.
Shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Liundi ikiendelea.
Waombolezaji wakimfariji mke wa marehemu.
Rais Kikwete akiongea na Mzee Mkapa baada ya zoezi la kuaga.
Rais Kikwete akiagana na Salim Ahmed Salim.
...Akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Mzee Mkapa (kati) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula (kulia).
...Mkapa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kulia). Kushoto ni Pius Msekwa na Kinana.
Kinana akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (kulia).
Mkapa akiongea na Pius Msekwa baada ya shughuli ya kuaga mwili wa marehemu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, leo ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Jaji George Liundi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Liundi ambaye alikuwa Msajili wa Kwanza wa Vyama vya Siasa nchini, alifariki dunia Januari 12 mwaka huu alipokuwa akipelekwa Hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu. Marehemu Liundi amezikwa katika makaburi ya Chang'ombe Maduka Mawili jijini Dar.
(PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)

No comments: