Ndugu zangu,
Muda mfupi uliopita nimemwona Jaji Lubuva akimtangaza John Pombe Magufuli kuwa ndiye mgombea urais aliyewashinda wenzake wote.
Afrika hakuna fungate ( Honeymoon) ya kuingia Ikulu.
Kuwatumikia watu zaidi ya milioni 40 si kazi nyepesi. Kuwatumikia waliochagua na ambao hawakumchagua. Wanaompenda na wanaomchukia. Wote ni watu wake.
Na siku zote, Rais ni mmoja lakini kazi ya urais si ya mtu mmoja. John Magufuli anatakiwa sasa kujichimbia kupanga kikosi chake cha kazi ( Mawaziri).
Itakumbukwa, kuwa Magufuli alishawaambia wapiga kura kuwa mawaziri wake watakuwa wachache lakini wachapa kazi.
Hongera Sana John Pombe Magufuli na Kila La Heri kwenye kuifanya kazi ya kuiongoza Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, na watu wake.
Maggid,
Iringa.
No comments:
Post a Comment