Ifuatayo ni taarifa rasmi ya Michuzi ameomba niwafikishie wadau wote wa blog yake...
UANZIA SASA TUMIA isamichuzi.blogspot.com (angalia ni 's' moja na sio mbili) KUINGIA KWENYE BLOGU YENU MPYA. ILE YA MWANZO JAMAA WAMEIBA EMAIL ADDRESS YANGU YA GMAIL HIVYO MATUMIZI YAKE NITAREJESHA BAADA YA KUTATUA SUALA HILI MUDA SI MREFU UJAO
WADAU KUNRADHI KWA KUWAHAMISHA MTAA KWA MUDA. WAJANJA WAMEIBA EMAIL ADDRESS YANGU ILIYONIWEZESHA KU-LOG IN KWENYE 'MICHUZI' BLOG NA KUNITIA KILEMA CHA MUDA. NAOMBA TUVUMILIANE WAKATI MAMBO YAKIREKEBISHWA ILA NAWAHAKIKISHIA KWAMBA HATA HAPA LIBENEKE NI LILE LILE TU, KARIBUNI SANA.
KAMA NILIVYOANZA MTAANI KULE HAPA PIA NAANZA KWA KUPOSTI PICHA YANGU NA NDESANJO IWE KAMA ALAMA YA KUANZIA NYUMBA MPYA. NAOMBA WADAU WOTE WALIOKUWA WANAWASILIANA NAMI KWA KUTUMIA EMAIL YA GMAIL WAACHE KWANI IKO MIKONONI MWA TAPELI NA WATUMIE YAHOO.COM JINA LILE LILE LANGU.
HII KWANGU NI CHANGAMOTO YA KUWA MACHO NA PIA KUWATAHADHARISHA WADAU WOTE KWAMBA MATAPELI HAWA WAPO MACHO NA WATAFANYA LOLOTE KUATHIRI MAWASILIANO.
NAWASHUKURU WADAU WOTE WALIONIPA POLE KWA MKASA HUU AMBAO NAOMBA NISEME KWAMBA INGAWA UNANIRUDISHA NYUMA LAKINI HAUNISIMAMISHI WALA HAUNIKATISHI TAMAA. NITAENDELEZA LIBENEKE LILE LILE KAMA KAWA. MFAHAMISHE NA MWINGINE KUHUSU NYUMBA HII MPYA.
ILE GLOBU YETU YA KWANZA ITAKUWEPO KAMA REFERENCE NA NITAANZA KUI-UPDATE MARA MAMBO YATAPOKUWA SAWA. JAMAA WA GOOGLE WAMENIAHIDI KULIFANYIA KAZI JAMBO HILI HARAKA IWEZEKANAVYO
No comments:
Post a Comment