Saturday, July 28, 2007

FUMANIZI!!


Katika hali inayoonyesha kuwa dunia sasa imekwisha, mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Shomari alifumwa na mkewe katika makaburi akifanya ‘mchezo mchafu’ na shoga.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wetu, lilitokea Julai 26 mwaka huu saa 5.00 usiku katika makaburi ya Mabibo, jijini Dar Salaam baada ya mwanamke huyo kuweka mtego uliofanikisha kuwanasa.


Akiongea huku akiwa na hasira, baada ya fumanizi hilo, mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la mama Sele ambaye ni mkazi wa Mabibo alimtaja mumewe kuwa ni mfanyabiashara wa utumbo katika eneo la Pugu.

Mama huyo alisema kuwa, alitonywa muda mrefu kuwa mumewe huyo ana uhusiano wa kimapenzi na shoga, ndipo alipoanza kuwafuatilia bila mumewe kujua.

“Nilitonywa muda mrefu na rafiki wa mume wangu kuwa, baba Sele ana uhusiano wa kimapenzi na shoga, awali sikuamini lakini baadaye nikaja kubaini kuwa taarifa hiyo ilikuwa ya kweli,”

alisema mama huyo.


Aliongeza kuwa siku ya tukio, mume wake aliaga kuwa anakwenda magengeni kununua sigara na kwakuwa muda wenyewe haukuwa mzuri alimtilia mashaka, hivyo alimwambia rafiki yake mmoja amfuatilie kwa nyuma.

Mama huyo aliongeza kuwa, rafiki yake alimfuatilia hadi sehemu fulani ambapo Shomari alikutana na shoga kisha kuongozana naye hadi kwenye makaburi hayo.

Alisema walipofika eneo hilo, rafiki yake alimpigia simu na kumpasha kilichojiri, ndipo naye alipompigia simu mpiga picha wetu aliyekuwa eneo la Manzese na kumtaka afike haraka eneo hilo ili kupata picha za fumanizi, ambapo alifanya hivyo.

Katika fumanizi hilo, Shomari alikimbia na kuacha nguo zake ambazo zilikuwa na vitu kadhaa ikiwemo kijitabu kidogo (note book) ambacho kilikuwa na kumbukumbu zake.

Hata hivyo, shoga huyo alishindwa kutimua mbio kwani alikuwa uchi, jambo lililomfanya amkamate na kuanza kutwangana naye ambapo mpigapicha wetu alipata nafasi ya kupiga picha za varangati hilo.

Baada ya kupata picha hizo, mwandishi wetu aliondoka eneo hilo kwa kuogopa kuporwa kamera kutokana na mazingira yaliyokuwepo kwani vijana wa kihuni walianza kusogelea eneo hilo baada ya kusikia kelele.


WEMA SEPETU


Miss Tanzania 2006-07 Wema Sepetu, anayesadikiwa kuwa mrembo wa kwanza nchini kuwa na kashfa nyingi za ngono inadaiwa kuwa hata asafishwe vipi hawezi kutakata.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo nchini walisema kuwa, mrembo huyo anapoteza muda kutumia vyombo vya habari kujisafisha badala yake ajisafishe mwenyewe.

“ Unajua Wema hana mshauri, huwezi kutumia vyombo vya habari kujisafisha huku ukiendelea na tabia hizo hizo zilizokuchafua, eti anadai TID alitengeneza picha, hana lolote na Kanumba je?

“ Anataka kuudanganya umma, hivi kwanini waandishi wakusakame wewe tu kila kukicha? Nchi inaendeshwa kwa sheria na uandishi una zingatia hilo sasa kama kweli kwa nini asiwachukulie hatua wanaomchafua, njia ya muongo ni fupi!

“Huyu hata asafishwe vipi hatakati,” alisema mdau mmoja wa masuala ya urembo nchini Hammed Amanzi wa Masaki jijini Dar es Salaam.

Mdau huyo aliongeza kuwa hivi sasa Wema anapaswa kusahau yaliyopita na kuanza kujiosha kwa kufanya yalio mema kwani hakuna mtu atakayemuhukumu kupitia historia kwani kila mtu ana historia inayoweza kuwa safi ama chafu.

Aidha, habari zilizotufikia hivi karibuni zinaeleza kuwa, kuna watu ambao wamezinasa picha za Wema na Kanumba wakiwa katika mahaba mazito na wana orodha ya mabwana ‘maundergraund’ waliombonyeza kizenji ikiwa ni pamoja na waandishi waliompiga ‘promo’ enzi hizo anautafuta umalikia wa urembo nchini.

Gazeti hili linafanya jitihada za kuzitia mikononi picha hizo mapema iwezekanavyo na kuuonesha umma mambo ya mrembo huyo, hivyo endapo unajua lolote kuhusiana na suala hili, wasiliana nasi tutakuzawadia. donge nono.

2 comments:

Anonymous said...

Mmh kwa kweli hili fumanizi ni la aina yake,sasa hawa watu kwa nin walienda kufanya ufska wao makaburini?au kuna mambo ya kishirikina?Najua camera hii si mwingne bali ni Issa Mnally,wape hi kina Hamida,Marry na Shamim!!

Kingine sijui kwa nin hii blog yako kila nikitaka kuweka comment huwa inasumbua kufunguka,embu jaribu kucheki na wataalam.Nadhani ni tatizo ndo maana watu wengi wanashindwa kutoa comments zao.

Anonymous said...

nafikiri, kwa sababu mashoga hapo tz bado hawana haki za kutosha; hawana budi kufanya mambo yao siri siri hata katika maeneo ya makaburi! poleni nyie! je, mshapata kuiona filmu ya kimarekani "brokeback mountain"?