Sunday, July 22, 2007

JIDE KUZEEKEA KWENYE MUZIKI!




Msanii mkongwe katika game ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady Jaydee' (pichani juu) ameiambia Abby Cool & MC George Over The Weekend kuwa kwa upande wake hana mpango wa kuachana na sanaa ya muziki hata akifikisha umri kama alionao mwanamuziki mkongwe wa taarab, Bi. Kidude.

Akipiga stori zaidi na safu hii nyumbani kwake eneo la Hananasif, Kinondoni, Dar es Salaam, Jide a.k.a Komando, alisema kwamba wapo baadhi ya watu ambao huwa wanafikiria ameachana na game ya muziki pindi anapokuwa kimya, kitu ambacho siyo kweli.

'Kimya changu huwa ni kukaa na kufikiria vitu vipya vya kuimba, ndiyo maana huwa natoka na mashairi ambayo yanaigusa jamii, ambayo pia huiteka Afrika Mashariki, alisema.

Akiyazungumzia mabadiliko yake katika muziki, ikiwemo staili ya kwaito ambayo anaitumia hivi sasa, Jide alisema kwamba hiyo ni kutokana na kutembelea nchi mbalimbali kisha kupata mawazo kutoka kwa wanamuziki wengine wakiwemo wale ambao wamefanikiwa kupitia staili hiyo ya kwaito.

Msanii huyo ambaye anamiliki tuzo kumi na moja amesema kuwa nia yake ni kuongeza nyingine zaidi ili ndoto zake za kuwa mwanamuziki anayemiliki tuzo nyingi zitimie.

Hivi sasa Jide anamiliki bendi inayojulikana kama Machozi Band ambayo ina jumla ya wasanii kumi. 'Nina mpango wa kuipeleka Machozi nje ya nchi ili kwenda kujifunza mengi zaidi' alisema.

2 comments:

Unknown said...

Veeery nice blog man! Keep it up!!

Anonymous said...

kwani si tokea hapo si kishazeeka!!!!!!!!!!anataka azeeke vipi tena???